Tundu Lissu: IGP Sirro ni Jeshi la Polisi, hawajawahi kunipigia simu wala kunihoji, Waliagizwa wanipoteze baada ya Uchaguzi

Tundu Lissu: IGP Sirro ni Jeshi la Polisi, hawajawahi kunipigia simu wala kunihoji, Waliagizwa wanipoteze baada ya Uchaguzi

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
Mwanasiasa machachari wa Tanzania anayeishi mamtoni baaada ya kufanyiwa unyama amekanusha taarifa na kauli ya Igp Sirro kuwa alipigiwa simu na jeshi la polisi ili ahojiwe juu ya madhila yaliyompata.


Kupitia ukurasa wake wa Twita Lissu amedai kuwa taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote.

Soma >IGP Sirro: Kipindi cha kampeni nilimtafuta Tundu Lissu aje kuhojiwa lakini hakuja
====

IGP Sirro ni mwongo asiyefaa kuvaa sare ya Jeshi la Polisi, let alone kuwa Mkuu wake. For the record:

1) Hajawahi kunipigia simu au kuniita kwenye mahojiano yoyote.

2) Nikiwa Nairobi Hospital niliambiwa polisi watakuja kunihoji hospitalini. Niliwasubiri lakini hawakuonekana.

3) Polisi hawajahoji mtu yeyote wala kutoa taarifa yoyote juu ya uchunguzi wao, zaidi ya kudai wahusika ni watu wasiojulikana na hakuna hata mtu wanayemshuku.

4) Polisi walisema wana footage ya CCTV camera iliyokuwa kwenye jengo nilikoshambuliwa. Hadi leo wako kimya juu ya hilo.

5) Polisi hawajawahi kusema ni nani aliyeondoa walinzi wote kwenye makazi ya viongozi wa serikali ili kuwaruhusu wauaji waingie ndani na kunishambulia kwa risasi.

6) Nilisema hadharani kwamba nilikuwa nafuatiliwa kwa gari na watu waliotumwa na IGP Sirro na Mkuu wa TISS Kipilimba.

Niliwataja IGP Sirro na DG-TISS Kipilimba specifically na kuwataka waingilie kati, na nilitaja gari iliyokuwainanifuata fuata. Majibu yalitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba aliyepuuza taarifa yangu na kudai gari iliyokuwa inanifuata fuata iko Arusha, sio Dar.

Baada ya shambulio, Jeshi la Polisi lilifanya jitihada kubwa kuzuia wananchi kunipa msaada wowote. Waliojaribu kuniombea makanisani na misikitini walipigwa marufuku. Waliojaribu kujitolea damu walikatazwa. Waliovaa Tshirt zenye picha yangu walikamatwa na kuwekwa mahabusu.

6) Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, chini ya Mwenyekiti wake Balozi Adadi Rajabu (DCI mstaafu), ilifanya uchunguzi wa shambulio dhidi yangu na kuandaa taarifa rasmi. Taarifa hiyo ilizimwa na uongozi wa Bunge masaa machache kabla ya kuwasilishwa rasmi bungeni. Kwa nini?

7) Nilinyimwa haki ya kutibiwa kwa fedha za Bunge kama sheria inavyotaka. Baadae Katibu wa Bunge aliniandikia barua kwamba Rais Magufuli hakutoa idhini ya matibabu hayo.

8) Ni Magufuli aliyesema, saa 2 kabla sijashambuliwa, kuwa wanaopinga vita yake ya uchumi hawastahili kuishi!

9) Mwaka jana nilienda Polisi Dodoma kudai gari yangu ambayo iko polisi tangu niliposhambuliwa. Jibu la RPC Muroto lilikuwa sitapewa gari yangu mpaka nitakapohojiwa juu ya shambulio. Lakini polisi hawakuwa na interest ya kunihoji zaidi ya kupiga mabomu mikutano yangu ya hadhara.

10) Nilikimbia nchi baada ya kupata taarifa kuwa Rais Magufuli alikuwa ametoa amri kwa 'watu wasiojulikana' kuwa niuawe mara baada ya uchaguzi. Nilikamatiwa na polisi wa IGP Sirro nje ya Ubalozi wa Ujerumani na isingekuwa wanadiplomasia wa Kijerumani kuingilia kati ningepotezwa.

IGP Sirro anasema sistahili kupewa ulinzi wowote kwa sababu mimi ni Mtanzania sawa na Watanzania wengine. Lakini sio Watanzania wote waliowahi kushambuliwa kwa risasi 16 wala kutendewa kama nilivyotendewa mimi. Majibu yake ni utetezi wa wauaji wasiojulikana na wale waliowatuma!
 
..Waziri wa mambo ya ndani, wakati huo Mwigulu Nchemba, alisema kwamba gari yenye namba ambazo Tundu Lissu alidai inamfuatilia ilionekana Arusha.

..Na waziri wa mambo ya ndani akadai kwamba wamewahoji wahusika na wamejiridhisha kwamba gari hiyo haikuwahi kufika D'Salaam.

..IGP Sirro anadai Lissu hakuwahi kutoa taarifa kituo cha polisi kuhusu kufuatiliwa. Vilevile IGP anadai polisi hawana taarifa zozote kuhusu Lissu kufuatiliwa na " watu wasiojulikana. "

..Sasa katika mazingira kama hayo tumuamini nani? Je, Waziri wa mambo ya ndani alidanganya? Je, IGP anadanganya?
 
Kitendo cha yule Mama kuendelea kumtumia huyu mzee kama IGP nikapoteza imani naye kabisa.

Alipaswa awekwe pembeni maana uovu mwingi Wa Polisi enzi za jiwe hakuna namna hili zee linakwepa lawama.

Isitoshe hoja zake kuhusu shambulio la Lissu ni za kipuuzi sana. Lissu alivyorudi Tanzania alikwenda Polisi kufuatilia gari lake. Mbona hawakumwomba nafasi wamuhoji juu ya shambulio lililopelekea gari lake kuwa mikononi mwao?
 
Jamaa anajua hatuwezi kupata ushahidi kuhusiana na hiyo simu aliyopigiwa hivyo anacheza na akili zetu tu.
Utakuwa mjinga sana ukatae kupigiwa simu kama ulipigiwa. Record zote zinaweza kupatikana kutoka kwenye record ya mtandao uliotumika.

Lisu kutoa kauli hiyo, ni dhahiri ana uhakika. Kwa record ya jeshi letu hili la kubambikia watu kesi, ni vigumu sana kuwaamini polisi.
 
IGP alivuka hadhi ya nafasi yake. Angeishia kusema alimpigia Lissu simu hakwenda wenye akili wangemwelewa lakini alipoongeza kwamba Lissu anafurahia/anatumia hali aliyonayo kujipatia fedha, hata wasio na akili wakaona IGP ni ndugu yao.
 
Utakuwa mjinga sana ukatae kupigiwa simu kama ulipigiwa. Record zote zinaweza kupatikana kutoka kwenye record ya mtandao uliotumika.

Lisu kutoa kauli hiyo, ni dhahiri ana uhakika. Kwa record ya jeshi letu hili la kubambikia watu kesi, ni vigumu sana kuwaamini polisi.
Kwani rekodi za simu zinakaa muda gani??
 
Mtu anakwambia anafatiliwa wewe unapuuza

Walinzi wanaondolewa kwenye makazi yake alafu anapigwa risasi eneo ilo ilo.

Baada ya tukio CCTV zinaondolewa kwenye eneo la tukio

Badae baadhi ya wema serikalini waungwana wanamshauri Mbowe wampeleke nje

Unazuia makanisa na misikiti wasimuombee

Unapiga marufuku watu wasivae tisheti zake zilizoandikwa pray for lissu.

Ananyimwa pesa ya matibabu bila sababu

Anazuiliwa pesa zake za ubunge

Anavuliwa ubunge kinyume cha sheria

Anarudi kugombea urais anaibiwa kura na anataka kuuwawa tena baadhi ya vigogo serikalini wanamshauri kuondoka nchini!

Huyu mtu utasema hataki uchunguzi wa shambulio lake?

Kwanini uchunguzi usianzie kwenye walioondoa walinzi na CCTV?

Magufuli, Ndungai na Siro mtalipa huu uhuni!!
 
Nimeanza kupata mashaka na hii issue ya Tundu Lissu iweje CHADEMA wako kimya juu ya kuishinikiza serikali kuanzisha uchunguzi huru?..iweje wanaharakati wa tweeter hawaweki pressure kwa serikali ili ukweli ueleweke na haki ipatikane?....Au tunaisubiri serikali yenyewe iamue kufanya uchunguzi?

Nilitegemea mambo mazito yalitoikuta CHADEMA kama watu kupotea, kufa na kushambuliwa wanachama na wapenzi wahamasishwe umma ujue ukweli na hatua zichukuliwe kwa wahusika..Sioni harakati zozote zaidi ya mchezo wa paka na Panya CHADEMA na Serikali....kuna vilivyojificha bila shaka..
 
Back
Top Bottom