Pre GE2025 Tundu Lissu: Ili tuweze kushinda uchaguzi lazima tuwe na bunduki kama wao. Ikulu ndio inaamua wizi wa Kura!

Pre GE2025 Tundu Lissu: Ili tuweze kushinda uchaguzi lazima tuwe na bunduki kama wao. Ikulu ndio inaamua wizi wa Kura!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hoja nzur,

Tatizo unazuia vipi uchaguzi?

Watu wana ndoto zao..., suo kujiunga na chama tu ili kupiga makofi..

Lakini zaidi , Huo ukata wa fedha anaouona hapo chama kisipo shiriki uchaguzi kitageuka chama fukara na watahongwa mwanzo mwisho na ndio end of the good days ya CDM .
Ni afadhali cdm ife, kuliko iwe hai kwa kijipendekeza kwa ccm huku wafuasi wake wakigeuzwa wahanga utawala wa mabavu wa ccm.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu akizungumzia harakati za 'No Reform No Election' amedai kuwa "Ilituweze kushinda uchaguzi lazima tuwe na bunduki kama wao. Ikulu ndio inaamua wizi wa kura"

"Watu wetu wa leo ni welevu kuliko miaka 10 iliyopita, mwaka jana muliweka wagombea wa nafasi zote zinazogombaniwa hapa Kibamba na sehemu kubwa walienguliwa, mkatumia nguvu kubwa kuwarudisha, wakarudishwa baadhi alafu siku ya tarehe 27 mkashughulikiwa vizuri zaidi, matokeo yakatangazwa kwa mitutu ya bunduki ndio maana hamna Mwenyekiti wa mtaa hata mmoja, sio kwasababu mmekuwa wajinga kuliko mlivyokuwa miaka 10 iliyopita ni kwasababu sasa hivi ilitushinde uchaguzi inabidi tuwe na bunduki kama wao"

Lissu ameendelea kwa kusema: "Katika mazingira ya uchaguzi wa sasa ili tushinde uchaguzi inabidi tuwe na bunduki kama wao, ili wasiweze kutumia bunduki zao kuingia vituoni kwa nguvu na kuchukua masanduku ya kura kwa nguvu,"

Lissu amehoji: "kama na sisi tukiwa na bunduki hiyo nchi itakuwaje?, patakua na pakukaa hapo?, ndivyo wanavyotaka?

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa:
Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Hizi sasa ndio siasa za kuwaweza CCM tulizokuwa tunasubiri kutoka TAL. Embu tendelee hivyo hivyo hadi kieleweke.
 
Reforms kwa njia za amani zimeshindikana, namna pekee ndio hiyo ambayo wote tutaheshimiana.
Hii Strategy ya kubeba mitutu sio, mimi naunga mkono Maandamano yasiyo na kikomo kuliko kuliingiza Taifa langu nilipendalo kwenye Civil War na kama lengo ni kuliingiza Taifa kwenye civil war basi nitaachana na Vyama nitasimama na Taifa.
 
Hii Strategy ya kubeba mitutu sio mimi naunga mkono Maandamano yasiyo na kikomo kuliko kuliingiza Taifa langu nilipendalo kwenye Civil War na kama lengo ni kuliingiza Taifa kwenye civil war basi nitaachana na Vyama nitasimama na Taifa.
Mkuu simama na taifa, ila sisi wengine tumechoka kutawaliwa kwa shuruti na ccm, na hawako tayari kwa mabadiliko.
 
Mi ikipatkana SMG,Ak47,SAR,M16 nipewe moja wapo….Am more than ready.
Watanzania hawa hawa ambao wakisikia tairi ya gari imepasuka wanajificha uvunguni, watathubutu kuingia front ? Pili. Tanzania kila pori linajulikana, watasakwa kote kote. Kwangu hiyo ni ngumu kutokea. Ni ndani ya jeshi tu hili likitokea nchi itapona. Bahati majeshi yote yamevaa rangi za Yanga.
 
Back
Top Bottom