Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kamati Kuu itakaa kutoa msimamo rasmi juu ya Mbunge wa Nkasi, Aida Khenan

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kamati Kuu itakaa kutoa msimamo rasmi juu ya Mbunge wa Nkasi, Aida Khenan

Wamfukuze tu, aende CCM. Hata wasimpomfukuza, itafika wakati ataunga juhudi. Kwanza lazima ni mwenzao. Wawe makini sana naye. Kwa nini pamoja na wizi wote uliotokea na Wakurugenzi kuagizwa kuwatangaza wagombea wa CCM kushinda, Nkasi ikawa tofauti? Mkurugenzi wa Nkasi hapendi kazi yake?
Tukiendelea na ubinafsi huu chadema hatutafika mbali.

Hivi hatusomi alama za nyakati kwa utawala huu?

Kwa nn dada wa watu anyimwe ajira yake aliyoipata?

Unazungumzia habari ya wabunge na madiwani kukatwa,ni kweli ni hujuma,sasa kwa nn hatukujitoa?

Tulishasema hoja iwe katiba mpya itakayokuja na NEC huru,watu wakapiga kimya kwa sababu walikuwa na ajira,sasa wamekosa na mwenzao kapata imekuwa hoja,huu ni upuuzi.

Muacheni akawapambanie watu wake bungeni hata kama hataongea mwacheni apate posho.
 
Kama ni ajira tu kama kuuza dukani basi aunge mkono juhudi. Ataendelea kuwa Mbunge huko CCM. Lakini mimi naongelea kitu ambacho ni zaidi ya ajira. Wale wote waliokuwa wanatafuta ajira - Waitara, Katambi, Kafulila, Mollel, Silinde nk wako CCM.
Kwa nn dada wa watu anyimwe ajira yake aliyoipata?
 
Kama ni ajira tu kama kuuza dukani basi aunge mkono juhudi. Ataendelea kuwa Mbunge huko CCM. Lakini mimi naongelea kitu ambacho ni zaidi ya ajira. Wale wote waliokuwa wanatafuta ajira - Waitara, Katambi, Kafulila, Mollel, Silinde nk wako CCM.
Mjadala wa chama ujikite kwenye vitu vyenye mantiki tuachane na vitu vidogo.
Acheni dada akawawakilishe raia wake na apate posho.
Hatuwezi kumlazimisha aende Ccm wakati wananchi waliomchagua walimpenda akiwa chadema.
Mitego midogo kama hii tunatakiwa kuivuka salama bila kutetereka.
 
Mapambano ya kutafuta haki siyo mapambano ya kutafuta posho. Unajaribu kuchanganya mafuta na maji.
Mjadala wa chama ujikite kwenye vitu vyenye mantiki tuachane na vitu vidogo.
Acheni dada akawawakilishe raia wake na apate posho.
Hatuwezi kumlazimisha aende Ccm wakati wananchi waliomchagua walimpenda akiwa chadema.
Mitego midogo kama hii tunatakiwa kuivuka salama bila kutetereka.
 
Aida hata sura yake tu inaonyesha, ataunga mkono juhudi muda si mrefu.Jiandaeni kumfukuza uanachama wa saccos.
 
Busara ni kumuachia Aida aapishwe na kuwa mbunge kamili na kuendelea na kazi za kibunge na chama kuendelea na msimamo wa kutokuutambua uchaguzi!
Hili jambo litaleta mvutano sana, chadema wakimuacha aapishwe kuwa mbunge kamili, maana yake ni kwamba atakuwa mbunge wa JMT kwa tiketi ya chadema. Na hapo azimio la chadema kutoutambua uchaguzi nitakuwa limefutika rasmi. Je chadema watamuacha ale kiapo kama mbunge kwa maana yakuutambua uchaguzi? Ama kamati kuu itakubaliana na msimamo wa viongozi na huyu dada abaki peke yake na mwisho wa mchezo afukuzwe uanachama?
 
Hapana..

Shida yake ni ubunge. Kama shida ni ubunge anaweza kuwa nao kwa kupitia forum yoyote..

In my opinion, CHADEMA hawana tatizo na Aida Khenan as a person..

CHADEMA wanatambua kuwa "ubunge" ni ajira tena inayolipa vizuri sana..

CHADEMA inatambua kuwa Aida Khenan anaihitaji ajira hiyo..

Shida iko kwenye mfumo unaotoa riziki kupitia ajira hiyo..

CHADEMA inapambana na mfumo huu..

Na kwa kuwa vita ni ya kimfumo zaidi, basi matokeo yake yatawaathiri individuals on the way...

Na hawa wanaoutawala mfumo huu wa dhuluma (yaani CCM na serikali yao), they know exactly what they are doing..

Mimi naamini, CHADEMA watakuwa na akili ktk kuamua hili jambo..

Binafsi nataka huyu mama asiwe mwathirika wa vita hii. Ni vyema akaitumikia ajira yake aliyoipata kwa jasho na damu...

Hata ikibidi ajisajiri CCM, wamwache afanye hivyo. Itafika wakati haya mambo yatafikia mwisho na kila kitu kitakuwa wazi...

Pia, hata hawa wabunge wa viti maalumu wateuliwe tu kisha waende..

If the problem is a system - we have a defferent way to solve the problem.

If the problem is systemic - the way to solve the problem is ought to be different.

We must allow her to be part of Parliament, meanwhile we learn about how best to run political issues while we are in the peculiar setuation of having very few Members of Parliament from Chadema in the chamber like we are in today.
 
Mapambano ya kutafuta haki siyo mapambano ya kutafuta posho. Unajaribu kuchanganya mafuta na maji.
Chadema haitafuti haki, Chadema inatafuta kushika Dola. Katika safari ya kushika dola mazingira kama haya hutokea na lazima tujifunze kuishi nayo na kunatokea nini.
 
Huo ubunge kapewa na CCM wanaomtishia maisha ni CCM asisingizie wanachi bora chama kimfukuze kisibebe lawama bora abebe na CCM waliomteua.
 
Kuanzia mwenyekiti wao na viongozi wote chadema Wana roho mbaya na hili ndilo linalowaponza Kama hawamtaki wamwache kachaguliwa na wananchi usinch wao huo
 
Mwenye kipato ndo boss popote pale duniani. Ndani ya chadema ya sasa Aidah ndo mwenye kazi ya kueleweka hadi pale viti maalum watakapochaguliwa, so sioni ni vipi mwenye kipato(Aidah) anapaswa kuwasikiliza wazee wa misheni town kwa sasa Mbowe, Lissu na wapiga kelele wa bavicha Jf kama Salary Slip, @erythrocite, brazaj, tindo, technically, OKW BOBAN SUNZU na ndege wengine.
 
Aida Khenan mbunge mteule wa Nkasi amesema, yeye ni mbunge pekee aliyetangazwa na katika mkoa wake amepata madiwani 10.

Lakini amesema amesikia kwenye mitandao kuhusu msimamo wa chama chake lakini yeye hajapewa taarifa rasmi eidha ya simu au barua, anadai anaamini chama chake ni taasisi kubwa hivyo anategemea atapewa taarifa rasmi.

Amesema jimboni kwake na mkoani kwake mpaka sasa kuna taharuki kubwa, wananchi wana taharuki kubwa.

Amesema mpaka sasa ametishiwa maisha na wananchi kwa kuwa wao waliamua kuvunja rekodi ya kutoa Mbunge mwanamke kwa mara ya kwanza hivyo wanadai yeye akifuata msimamo wa chama atakuwa kawasaliti wananchi ambao wapo walioumia ili yeye ashinde, pia amesema kuna kesi kama 18 za watu waliokamatwa walipokuwa wanapigania yeye ashinde.

Amedai wananchi wanamwambia kuwa machozi yao hayawezi kwenda bure asipokwenda kuwatumikia bora maisha yake wananchi wayamalize hapo.

Amedai kuwa anaomba chama chake warudie upya kutazama maamuzi yao, na kama waliyatoa kwa jazba kulingana na yaliyotekea kwenye uchaguzi basi waangalie upya na waelewe kuwa yeye hana amani anatishiwa maisha na amedai hawezi kuhama Rukwa na hawezi kuhama Nkasi.

Amedai kuwa kwa mara ya kwanza kwenye jimbo lao wamepata Mbunge mwanamke na Mbunge wa kutoka upinzani hivyo asipokwenda kuwawakilisha wananchi madhara yake ni makubwa sana kwake aidha hata kama viongozi wake hawatayaona.

Amesema alisharipoti Polisi kuhusu kutishiwa maisha na pia msimamo huo si wake peke yake bali ni wake na viongozi wa mkoa wa chama cha CHADEMA.

Amesema katika ngazi ya taifa hakuna kiongozi yeyote aliyemtafuta hata kwa simu aweze kujua amani yake au usalama wake.

Amedai kuwa alipoomba nafasi ya Ubunge aliomba peke yake na wala hawakuomba 2 wala 3 hivyo atakwenda bungeni kama yeye Aida na atakwenda kuwasilisha sauti yake yeye peke yake kwa niaba ya wananchi wa Nkasi japo atakuwa mpweke ndani ya bunge. Anasema alipokuwa mbunge wa viti maalum alijifunza kutoka kwa wabunge waliomtangulia lakini kama wabunge wa Viti Maalum watakwenda kipindi hiki atapata faraja lakini wasipokwenda itakuwa mpweke lakini faraja atapata kwa wananchi waliomchagua anaowawakilisha.

Tundu Lissu nae anena haya
Tundu Lissu anena kuwa, keshokutwa watakaa kamati kuu na ndio itatoa msimamo wa jumla wa chama, msimamo ambao waliusema wiki iliopita ni msimamo wa viongozi wakuu wa chama, lakini lazima kamati kuu itoe baraka zake au ikatae kutoa baraka zake.

Tundu Lissu amedai kuwa wao hawakua na wajibu wa kuuliza yeye Aida anafikiriaje kwa kuwa wao viongozi wakuu wana majukumu mengine ndani ya chama, amedai kuwa wao walitoa msimamo wao kuwa huo haukuwa uchaguzi.

Amedai kuwa kama chama kikisema kuwa huo ndio msimamo wa chama basi itabidi atafute utaratibu mwingine wa kuwatumikia wananchi wa Nkasi kwa kuwa Tanzania hakuna mbunge binafsi bali ni wabunge wa chama hivyo wabunge ni lazima wafuate utaratibu wa chama.
Chadema kuteua Wabunge wa Viti maalumu ni kubariki Uchaguzi kuwa ulikuwa Huru na Haki
 
Jamaa wabinafsi sana

Lowassa 'alipoibiwa'kura hawakususa kwenda Bungeni kwa kuwa wao walipata Ubunge

Slaa 'alipoibiwa' kura wao hawakususa kwenda Bungeni kwa kuwa wao walipata Ubunge

Safari hii kwa kuwa wao binafsi 'wameibiwa' wanataka hata 'wasioibiwa' wasuse
"Safari hii kwa kuwa wao binafsi 'wameibiwa' wanataka hata 'wasioibiwa' wasuse".

Nilidhani utasema wameshindwa kihalali, lakini umekiri kwamba wameibiwa, sasa mbinafsi ni aliye iba ama aliye ibiwa?
 
Kajifunze kwanza maana ya funga na fungua nilizotumia kwny maneno hayo otherwise comment yangu sikuiandaa kwa watu wa level yako kuisoma na kuielewa
"Safari hii kwa kuwa wao binafsi 'wameibiwa' wanataka hata 'wasioibiwa' wasuse".

Nilidhani utasema wameshindwa kihalali, lakini umekiri kwamba wameibiwa, sasa mbinafsi ni aliye iba ama aliye ibiwa?
 
Uyo dada hajamsinda kesy najua siasa za huko ni mchezo tu umetenegnezwa unajifanya kujitoa akili na kuposti upumbavu wako.
Yaani wewe unachekesha sana.

Mkishindwa mnasema mmeibiwa,
Mkishinda mnasema hamjashinda.

Upumbavu unao wewe
Katangaze basi mshindi unayemjua wewe
 
Wanasiasa wengi wa Tanzania wako hivyo (kama wewe). Wengi tu wanampigia dikteta makofi kwa mawazo kama haya yako. Siyo kwamba wanampenda. Na hata huyo Aida anafikiria kama wewe. Ndio maana analazimisha kwenda. Ushenzi wote uliofanyika, ameshasahau!
Mbona 2015 mlisema pia mmeibiwa kwenye Urais?
Kwanini akina mbowe na lisu walienda bungeni?
Kwanini wasisuse ili kuonyesha msimamo??
Kumbe umejua kwamba na wao wapo kinaslahi eeh??
Yaani wao ni waroho wa hizo posho ila wanataka mwenzao asiende kisa wao wameshindwa.

Huu ni ujinga sana
 
Back
Top Bottom