Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kamati Kuu itakaa kutoa msimamo rasmi juu ya Mbunge wa Nkasi, Aida Khenan

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kamati Kuu itakaa kutoa msimamo rasmi juu ya Mbunge wa Nkasi, Aida Khenan

Huyo binti hajitambui! Anachofuata hapo ni pesa tu! Na ajue kuwa amepitishwa si kwa "kushinda" kwa Imani ya CCM bali kupitishwa tuuu! Anaamini yeye ni bora kuliko wote ambao kura zao zilipokwa? Peke yake huko ataenda kutetea nini kama siyo kutumika na chama dola?
Kwani kina Mbowe walikuwa wanatetea nini bungeni huko, na kwa uchache wao walishawahi kupitisha nini?
Acheni ubinafsi nyie
 
Samahani wapinzani wa tz
Hivii mligetemea wabunge gani wa upinzani ambao wangeweza kuibuka kidedea?

Hai kashindwa kihalali
Arusha pia kashindwa kihalali
Mbeya nako kihalali
Tarime nako vilevile
Musoma hivo hivo
Sijui mikumi
Kawe
Kibamba hali ni ile ile
Kwa maana kama ni wizi umetendeka kwa kuonewa wapinzani
Vibe lingeanzia majimboni kwao
Lakn cha kushangaza watu wapo cool kwa maana wamelizka na matokeo hayo na ni halali kabisaaa

Sasa kwanini mlipanga kuja kulinukisha jiji la Dar ili hali sio jimbo lenu?'
Halafu mlijionea wenyewe kabisa kwenye kampeni za Mh TAL jinsi raia wa Dar es salaam hawana time naye?
Acheni lawama zisizo kuwa na mashiko.kabisa
Maana dalili ya mvua ni mawingu
Na imenyesha kweli kweli hadi mmeanza kutafta pa kujibanza kwa aibu

Hapakuwa na mbunge yeyote yule aliekuwa na uwezo wa kuingia bungeni uchaguzi huu 2020, kutoka upinzani na jinsi JPM alivojinadi kupitiankazi yake na hatimaye kuwabeba wagombea ubunge wake,

Na kila aliyejuwa amelitambua toka mapema kuwa 2020 akipata upenyo tu wa kupitishwa na NEC ya CCM lazima atatinga bungeni iwe jua iwe mvua na ndio maana watia nia walikuwa wengi kama nn kupitia CCM

hivyo CCM imejitahidi na kujibeba yenyew kama yenyew kuupata ushindi huu wa kishindo

Maeneo mengine siwezi kusema kwa kuwa sikuwa on the ground lakini kwa Hao Constituency kwa kaka Mbowe sina shaka na nasema Mbowe kapigwa kweupe na hakupiga kura sababu wananchi ndio waliokuwa hawamtaki.

Nimepita tarafa zifuatazo: Uroki, Nkira, Aishi, Uswaa, Nshara, Mamba, Kalali,Uraa, Kisiki, Nkoraya, Sonu, Kyeeri, Nkuu, Kisereni, Mwowe, Nkwarungo, Nkweseko.Matikoni, N'guni,Masama Magharibi, Masama Kusini, Kashinsha, Ivaeny, na kituo changu kikuu kilikuwa Lyamungo Sinde na Mwowe msikitini huku nikinywa chai na Bii mkubwa.

Na nimetembelea usiku ule mpaka asubuhi yake vijiji karibu 162.
 
Wangejua namna uyu dada ana pambana na game yake ilivo tight wangemuacha tu awahudumie wananchi walomchagua..other wise wanaonesha ubaguzi wa hali ya juu. We all know CCM lost the war.
 
1/3 ndio walipiga kura, jiulize kwanini 2/3 hawakujitokeza kupiga. Na hiyo 1/3 imefika kutokana na kura za wizi na idadi ya kupika. Fuatilia vizuri kura za ubunge hazitally na za uraisi, wakati watu wanapiga kura tatu. Ule haukuwa uchaguzi, bali uhayawani kama uhayawani mwingine wowote. Hiyo ndio sababu hata ccm wanaona aibu kushangilia ushindi wa vyombo vya dola na tume ya ubaguzi.
Tofauti ya kura za Wabunge na Urais labda sijui majimbo mengine ambayo I was not on the ground, lakini kwa Jimbo la Hai ambako nilikuwepo siku tatu kabla ya Uchaguzi na siku tatu baada ya Uchaguzi, sikuliona hilo.

Hai ni moja ya Majimbo ya wajanja na walalamishi, sula hilo lingeibuka kule kule Hai, na hapa mtandaoni pangekuwa hapatoshi.
 
Tofauti ya kura za Wabunge na Urais labda sijui majimbo mengine ambayo I was not on the ground, lakini kwa Jimbo la Hai ambako nilikuwepo siku tatu kabla ya Uchaguzi na siku tatu baada ya Uchaguzi, sikuliona hilo.

Hai ni moja ya Majimbo ya wajanja na walalamishi, sula hilo lingeibuka Hai kule kule Hai, na hapa mtandaoni pangekuwa hapatoshi.
Kutaka kujua hiyo tofauti ni mpaka uwepo kila jimbo, au ni kupitia figure za tume? Hao watu wa Hai si ndio huko wapinzani walikuwa wanapigwa kwa maagizo ya DC chini ya uratibu wa OCD? Mitandao ipi wakati imefungwa na ushahidi mwingi unaowekwa hapa mnasema ni uzushi wa mitandaoni?
 
Kutaka kujua hiyo tofauti ni mpaka uwepo kila jimbo, au ni kupitia figure za tume? Hao watu wa Hai si ndio huko wapinzani walikuwa wanapigwa kwa maagizo ya DC chini ya uratibu wa OCD? Mitandao ipi wakati imefungwa na ushahidi mwingi unaowekwa hapa mnasema ni uzushi wa mitandaoni?
Tafadhali usipotoshe, nilikuwa Hai na interest yangu ilikuwa ni Uchaguzi na mimi ni mwanachama na sio shabiki wa Chadema.
1) Zilihesabiwa kura zote.
2) Kura alizo pata mshindi na zilibandikwa.
3) Kura alizo pata Mbowe na zilibandikwa.
4) Na kura za Rais zilibandikwa, tena Mbunge mteule Saasisha alilazimisha kura za Rais zitangazwe na akiwepo kwanza ndipo asaini form yake ya ushindi na kuondoka.

UCHAGUZI HUU HAI ULIKUWA NA MSISIMKO WA KIVYAKE NA KARIBU KILA MWANA HAI ALIJUHUSISHA NA UCHAGUZI HUU.

KWA HAI , HAKUNA CHA WIZI WALA BABAYAKE MWIZI. BINGWA KAPIGWA HANDS DOWN.

Uchaguzi umekwisha, sasa tuangalie jinsi gani mkate utafika juu ya meza. Ni jukumu lako kuifanyia mema Serikali na sio Serikali ikufanyie nini.
 
yale yale ya corona, wabunge wameenda bungeni wakafutwa uanachama, kwa kifupi chama cha kipuuzi sana hiki
 
Halafu akihamia CCM watasema kanunuliwa

Hapana..

Shida yake ni ubunge. Kama shida ni ubunge anaweza kuwa nao kwa kupitia forum yoyote..

In my opinion, CHADEMA hawana tatizo na Aida Khenan as a person..

CHADEMA wanatambua kuwa "ubunge" ni ajira tena inayolipa vizuri sana..

CHADEMA inatambua kuwa Aida Khenan anaihitaji ajira hiyo..

Shida iko kwenye mfumo unaotoa riziki kupitia ajira hiyo..

CHADEMA inapambana na mfumo huu..

Na kwa kuwa vita ni ya kimfumo zaidi, basi matokeo yake yatawaathiri individuals on the way...

Na hawa wanaoutawala mfumo huu wa dhuluma (yaani CCM na serikali yao), they know exactly what they are doing..

Mimi naamini, CHADEMA watakuwa na akili ktk kuamua hili jambo..

Binafsi nataka huyu mama asiwe mwathirika wa vita hii. Ni vyema akaitumikia ajira yake aliyoipata kwa jasho na damu...

Hata ikibidi ajisajiri CCM, wamwache afanye hivyo. Itafika wakati haya mambo yatafikia mwisho na kila kitu kitakuwa wazi...

Pia, hata hawa wabunge wa viti maalumu wateuliwe tu kisha waende..
 
Wewe unaefikiria kwa kutumia tumbo ndo hauko serious. Kama sio chadema kumpa dhamana hio kazi unayodai angeitoa wapi?
Amechaguliwa na wananchi. We unadhani mbowe angeshinda angesusa?
 
Wanasiasa wengi wa Tanzania wako hivyo (kama wewe). Wengi tu wanampigia dikteta makofi kwa mawazo kama haya yako. Siyo kwamba wanampenda. Na hata huyo Aida anafikiria kama wewe. Ndio maana analazimisha kwenda. Ushenzi wote uliofanyika, ameshasahau!
Mimi sio mwanasiasa, siwezi kuwa na fikra kama zao
 
Jamaa wabinafsi sana

Lowassa 'alipoibiwa'kura hawakususa kwenda Bungeni kwa kuwa wao walipata Ubunge

Slaa 'alipoibiwa' kura wao hawakususa kwenda Bungeni kwa kuwa wao walipata Ubunge

Safari hii kwa kuwa wao binafsi 'wameibiwa' wanataka hata 'wasioibiwa' wasuse
 
Sasa nchi mmepewa,bado mnahangaika nao,kunani?Bado mmefunga mitandao ya kijamii,hofu yenu nini?
Acheni maisha yaendelee,sisi wapenzi wa upinzani tumeshakubali mchukue kila kitu kwa 100%!Kwanini bado hamridhiki?
Mna matatizo,sio bure!
Acheni kulia lia,tekelezeni ahadi mlizowaahidi watanzania!
Tulisema kuwa mtakimbiana
 
Back
Top Bottom