Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kamati Kuu itakaa kutoa msimamo rasmi juu ya Mbunge wa Nkasi, Aida Khenan

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kamati Kuu itakaa kutoa msimamo rasmi juu ya Mbunge wa Nkasi, Aida Khenan

Watashiriki na kipigo kipo pale pale, hata wakisusa kipigo kipo pale pale
We nguchiro kama unadhani kipigo kitaishia kwa upinzani tu basi unajidanganya. Nchi inapoingia kwenye mkwamo wa kisiasa wanaoumia sio viongozi bali wananchi wa kawaida
 
Jakaya alitaka aunde hiyo Tume kabla hajamaliza muda wake watu wakasusia Mchakato wa kuunda hiyo Tume wakamwambia asituzingue aende zake Rais ajae atamalizia, so tuvute subra Rais 'ajae' wa Katiba Mpya yupo njian kwenye foleni
Lijalo litatufurahisha
 
We nguchiro kama unadhani kipigo kitaishia kwa upinzani tu basi unajidanganya. Nchi inapoingia kwenye mkwamo wa kisiasa wanaoumia sio viongozi bali wananchi wa kawaida
Huo ndio ukweli, hata kama ni mchungu na mgumu kumeza. Angalia uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 wapinzani walisusa, wakapigwa. Uchaguzi mkuu 2020, wameshiriki wakapigwa.

Na hakuna cha tofauti kilichofanyika an unataka tudanganyane kwa kauli za kutupa moyo eti uchaguzi ujao kuna jambo jipya Waikato refa ni yule yule na taratibu ni zile zile?
 
Dhambi kubwa mi chadeama unataka kumfanyia dada wa watu mlitaka ashinde mbowe
Mambo ya CHADEMA iachieni CHADEMA. Kama mnampenda Aida, CCM mchukuweni ili kuongeza % zenu Bungeni. Nyie mko juu ya katiba/sheria. Bunge lililopita Mwambe alikuwa mbunge bila chama kwa hisani ya Spika. Hata Aida ikiwapendeza, anaweza kuwa Mbunge bila chama.

Kwani kuna uchaguzi upi kwenye chaguzi za nyuma wapinzani waliwahi kukiri ni uhuru na haki?
Lakini mbona waliingia bungeni chaguzi zote za nyuma ambazo pia hazikuwa huru na haki kama kawaida yao wanavyodai marazote.
Ilitakiwa lau Mbowe na lema ndo washinde huyu dada anadharau sana
 
Ndio maana watu wengine wanakosa Imani katika vyama vya upinzani. Inaonakena watu wanatafuta maslahi tu. Mazingira ya uchaguzi huu hayaruhusu kabisa mbunge na madiwani wa CHADEMA kukaa meza moja na CCM. Mtaka mabadiliko yeyote hawezi kabisa. Mtaka kipato hatojali...
Ok lakini haya pia mlilalamikia 2010,2015 mkasema mnaenda kushtaki The Hague inatofauti gani na huyu dada?
 
CHADEMA muacheni huyu Dada aliyechaguliwa na Wananchi wake akawatumikie. Kumuwekea vikwazo litakuwa jambo la ajabu na hovyo sana na itaonesha chuki ya wazi kabisa, na hiyo itakuwa hatua ya awali kabisa kuonesha kwamba CHADEMA hampo kwa ajili ya Wananchi bali kwa maslahi ya watu wachache ndani ya Chama.
 
Kwanini mpambane na huyo dada tuu mbona madiwani walio shinda mmewaacha au wao uchaguzi ulikuwa haki.
 
Yaani wakishindwa mnasema wameibiwa,walishinda

Wakishinda mnasema tena hawajashinda.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Uyo dada hajamsinda kesy najua siasa za huko ni mchezo tu umetenegnezwa unajifanya kujitoa akili na kuposti upumbavu wako.
 
CHADEMA muacheni huyu Dada aliyechaguliwa na Wananchi wake akawatumikie. Kumuwekea vikwazo litakuwa jambo la ajabu na hovyo sana na itaonesha chuki ya wazi kabisa, na hiyo itakuwa hatua ya awali kabisa kuonesha kwamba CHADEMA hampo kwa ajili ya Wananchi bali kwa maslahi ya watu wachache ndani ya Chama.
Huyu mdada hakuchaguliwa na wananchi ila ni kwamba ametangazwa za msimamizi kwamba ameshinda.
Kwenye uchauzi huu watangaza matokeo walikuwa na maelekezo maalumu
 
Aida Khenan mbunge mteule wa Nkasi amesema, yeye ni mbunge pekee aliyetangazwa na katika mkoa wake amepata madiwani 10.

Lakini amesema amesikia kwenye mitandao kuhusu msimamo wa chama chake lakini yeye hajapewa taarifa rasmi eidha ya simu au barua, anadai anaamini chama chake ni taasisi kubwa hivyo anategemea atapewa taarifa rasmi.

Amesema jimboni kwake na mkoani kwake mpaka sasa kuna taharuki kubwa, wananchi wana taharuki kubwa.

Amesema mpaka sasa ametishiwa maisha na wananchi kwa kuwa wao waliamua kuvunja rekodi ya kutoa Mbunge mwanamke kwa mara ya kwanza hivyo wanadai yeye akifuata msimamo wa chama atakuwa kawasaliti wananchi ambao wapo walioumia ili yeye ashinde, pia amesema kuna kesi kama 18 za watu waliokamatwa walipokuwa wanapigania yeye ashinde.

Amedai wananchi wanamwambia kuwa machozi yao hayawezi kwenda bure asipokwenda kuwatumikia bora maisha yake wananchi wayamalize hapo.

Amedai kuwa anaomba chama chake warudie upya kutazama maamuzi yao, na kama waliyatoa kwa jazba kulingana na yaliyotekea kwenye uchaguzi basi waangalie upya na waelewe kuwa yeye hana amani anatishiwa maisha na amedai hawezi kuhama Rukwa na hawezi kuhama Nkasi.

Amedai kuwa kwa mara ya kwanza kwenye jimbo lao wamepata Mbunge mwanamke na Mbunge wa kutoka upinzani hivyo asipokwenda kuwawakilisha wananchi madhara yake ni makubwa sana kwake aidha hata kama viongozi wake hawatayaona.

Amesema alisharipoti Polisi kuhusu kutishiwa maisha na pia msimamo huo si wake peke yake bali ni wake na viongozi wa mkoa wa chama cha CHADEMA.

Amesema katika ngazi ya taifa hakuna kiongozi yeyote aliyemtafuta hata kwa simu aweze kujua amani yake au usalama wake.

Amedai kuwa alipoomba nafasi ya Ubunge aliomba peke yake na wala hawakuomba 2 wala 3 hivyo atakwenda bungeni kama yeye Aida na atakwenda kuwasilisha sauti yake yeye peke yake kwa niaba ya wananchi wa Nkasi japo atakuwa mpweke ndani ya bunge. Anasema alipokuwa mbunge wa viti maalum alijifunza kutoka kwa wabunge waliomtangulia lakini kama wabunge wa Viti Maalum watakwenda kipindi hiki atapata faraja lakini wasipokwenda itakuwa mpweke lakini faraja atapata kwa wananchi waliomchagua anaowawakilisha.

Tundu Lissu nae anena haya
Tundu Lissu anena kuwa, keshokutwa watakaa kamati kuu na ndio itatoa msimamo wa jumla wa chama, msimamo ambao waliusema wiki iliopita ni msimamo wa viongozi wakuu wa chama, lakini lazima kamati kuu itoe baraka zake au ikatae kutoa baraka zake.

Tundu Lissu amedai kuwa wao hawakua na wajibu wa kuuliza yeye Aida anafikiriaje kwa kuwa wao viongozi wakuu wana majukumu mengine ndani ya chama, amedai kuwa wao walitoa msimamo wao kuwa huo haukuwa uchaguzi.

Amedai kuwa kama chama kikisema kuwa huo ndio msimamo wa chama basi itabidi atafute utaratibu mwingine wa kuwatumikia wananchi wa Nkasi kwa kuwa Tanzania hakuna mbunge binafsi bali ni wabunge wa chama hivyo wabunge ni lazima wafuate utaratibu wa chama.
Nawashauri Hawa jamaa Kama wataamua kukubaliana na Maalim Seif aukwae umakamu wa Rais basi na wabunge na wadiwani wote wa upinzani waende kuwafanyia kazi wananchi..wasiwe bias...naona Maalim Seif kawatega ACT, eti wataamua wakati anajua rohoni mwake kabisa kuwa anautaka umakamu..hahahah
 
Jamaa wabinafsi sana

Lowassa 'alipoibiwa'kura hawakususa kwenda Bungeni kwa kuwa wao walipata Ubunge

Slaa 'alipoibiwa' kura wao hawakususa kwenda Bungeni kwa kuwa wao walipata Ubunge

Safari hii kwa kuwa wao binafsi 'wameibiwa' wanataka hata 'wasioibiwa' wasuse
Hivi angekuwa amepita Mbowe, Lema,Sugu ama Msigwa nani angesusia ubunge...Chadema waache siasa za Kijinga.

Kwanza wanasisa wengi wapo kimaslahi tu, acha mama wa watu akawatumikie wananchi wake.
 
Mbunge pekee angekuwa Lema ama Mbowe mngemnyima nafasi hiyo ya kwenda kuwawakilisha wananchi waliomchagua?

Unaambiwa kwenye jimbo hilo kuna madiwani 10 wa chadema,kwa nn muwanyime watu haki yao ya kuwakilishwa?

Ukiacha uwakilishi kwa watu wake bado ubunge ni ajira,kwa nn anyimwe ajira aliyopewa na wapiga kura wake?

Naona ubinafsi mkubwa kwa viongozi wa chadema Taifa.
Vyama vya siasa navyo ni vidikteta fulani hivi
 
Back
Top Bottom