Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kamati Kuu itakaa kutoa msimamo rasmi juu ya Mbunge wa Nkasi, Aida Khenan

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kamati Kuu itakaa kutoa msimamo rasmi juu ya Mbunge wa Nkasi, Aida Khenan

Leo yamewakuta then wanasema tume si huru wenzao wakilalamika kuibiwa waliweka pamba maskioni hawaskii Ila baada ya kukosa wanataka wote wasiende, hicho ni kiwango Cha juu Sana Cha ubinafsi, tena wanaume wanalazimisha Aida na viti maalumu wasiende bungeni so selfish na aibu wallah, waache ubinafsi bwana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wao walienda na mishahara wakapata.
Wanataka dada wa watu asiende kuwawakilisha wananchi wake.
Dunia ina mambo hii[emoji1787]

Ila huyo dada anajua kujiongeza,kwa namna yoyote aende bungeni akale mahela yake hayo.

Ni wabinafsi mno, hawa hata wakija kushika dola watakuwa Kama CCM tu!

Wajanja sana,
Mbowe tar 26 allikuwa anapiga hesabu saa kuwa PM
Ingetokea yeye na Lisu wameshinda na Aida na wengine wote wameshindwa..angeuachia kweli huo uwaziri mkuu aliokuwa anaweweseka nao ?[emoji1787]
 
Walichojadili bungeni ndio kiliwafanya watu wachague ccm, wakati wale wazee wa akili kubwa wakitoka bungeni na kususia vikao ndipo wenzao wakapitisha budget.

1/3 ndio walipiga kura, jiulize kwanini 2/3 hawakujitokeza kupiga. Na hiyo 1/3 imefika kutokana na kura za wizi na idadi ya kupika. Fuatilia vizuri kura za ubunge hazitally na za uraisi, wakati watu wanapiga kura tatu. Ule haukuwa uchaguzi, bali uhayawani kama uhayawani mwingine wowote. Hiyo ndio sababu hata ccm wanaona aibu kushangilia ushindi wa vyombo vya dola na tume ya ubaguzi.
 
1/3 ndio walipiga kura, jiulize kwanini 2/3 hawakujitokeza kupiga. Na hiyo 1/3 imefika kutokana na kura za wizi na idadi ya kupika. Fuatilia vizuri kura za ubunge hazitally na za uraisi, wakati watu wanapiga kura tatu. Ule haukuwa uchaguzi, bali uhayawani kama uhayawani mwingine wowote. Hiyo ndio sababu hata ccm wanaona aibu kushangilia ushindi wa vyombo vya dola na tume ya ubaguzi.
Kura kuiba maana yake unajiongezea kura ... sio kupunguza sasa assume hajaibiwa ... inamana Tundu lissu angekua rais kwa kura mil 1
 
Yaani mtu apate kazi tena mshahara mnono asusie? Hampo serious nyie watu

Wewe unaefikiria kwa kutumia tumbo ndo hauko serious. Kama sio chadema kumpa dhamana hio kazi unayodai angeitoa wapi?
 
Sasa si atahatarisha uhai wake? Au wajerumani watamsindikiza?
Tundu buana😀😀
Aaah aliyemuokoa na risasi atamuokoa,pia kifo ni sehemu ya maisha kuuwa mwenzako sababu ya tumbo sio Kinga ya nae kutokufa.
Usimkomboe masikini unahatarisha maisha yako,awaache masikini wapambane na Hali zao.
 
Jamaa wabinafsi sana

Lowassa 'alipoibiwa'kura hawakususa kwenda Bungeni kwa kuwa wao walipata Ubunge

Slaa 'alipoibiwa' kura wao hawakususa kwenda Bungeni kwa kuwa wao walipata Ubunge

Safari hii kwa kuwa wao binafsi 'wameibiwa' wanataka hata 'wasioibiwa' wasuse
Naona kama unawazidi sana Chinua Achebe na William Shakespare kwa kuweka uwazi ndani ya jamii kwa kutumia lugha rahisi sana.
 
Unajiskiaje unamfanyia Mchongo demu apate kazi ofisin kwenu halafu wahuni wanampa Kazi hiyo halafu wanakufanyia figisu wanakutema wewe,

unamshauri Demu wako aache hiyo kazi anakataa

Ndio kinachowauma 'Kamati kuu' ya jamaa flan
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Jamaa wabinafsi sana

Lowassa 'alipoibiwa'kura hawakususa kwenda Bungeni kwa kuwa wao walipata Ubunge

Slaa 'alipoibiwa' kura wao hawakususa kwenda Bungeni kwa kuwa wao walipata Ubunge

Safari hii kwa kuwa wao binafsi 'wameibiwa' wanataka hata 'wasioibiwa' wasuse
Upuuzi mtupu, wanajiona wao ndo kila kitu
 
Ila Magufuli kiboko..yani Lisu ndio kawa mpole hivyo?
Ushabiki unatia watu upofu japo akili wanazo ila hawataki kutumia. unajiuliza kwa nini Magufuli anazungukwa na jeshi na silaha nzito za moto?hofu ya kudhuliwa aliyonayo Magufuli ndio aliyonayo Lissu
 
Ila Magufuli kiboko..yani Lisu ndio kawa mpole hivyo?
Yani kiboko kabisa,sio Lissu tu,Mbowe,Zitto wote milenda tu saa hii,JPM kagonga palepale wasipotegemea warudi mtaani huku kwanza tucheze wote sebene lake.
 
Maisha mafupi jamani, wamuache dada wa watu na yeye nae ale mema ya nchi.
Sasa mema ya nchi ale pekeyake maana wananchi wake hawatapewa maendeleo hawamu hii.

Mkiniletea mtu wa chama kingine sileti maendeleo
 
Sasa hivi wanaolia-lia ni wapinzani.

Hilo siyo jambo jema katika taifa.

..siyo jambo ambalo chama tawala kinatakiwa kujivunia.

..kwani kuna shida gani kuunda tume ya uchaguzi itakayokidhi matakwa ya wadau wengi zaidi wa siasa?
Mbona unazidi kulialia huku

Pilipilpil ya shamba yakuwashia nini
 
Lakini mbunge hawezi kufanya kazi za kibunge kule bungeni bila kusaidiwa na chama, akienda peke yake atakuwa ana hudhuria tu kuokea posho siyo vinginevyo.
Chama ni muhimu sana.
 
Aida Khenan mbunge mteule wa Nkasi amesema, yeye ni mbunge pekee aliyetangazwa na katika mkoa wake amepata madiwani 10.

Lakini amesema amesikia kwenye mitandao kuhusu msimamo wa chama chake lakini yeye hajapewa taarifa rasmi eidha ya simu au barua, anadai anaamini chama chake ni taasisi kubwa hivyo anategemea atapewa taarifa rasmi.

Amesema jimboni kwake na mkoani kwake mpaka sasa kuna taharuki kubwa, wananchi wana taharuki kubwa.

Amesema mpaka sasa ametishiwa maisha na wananchi kwa kuwa wao waliamua kuvunja rekodi ya kutoa Mbunge mwanamke kwa mara ya kwanza hivyo wanadai yeye akifuata msimamo wa chama atakuwa kawasaliti wananchi ambao wapo walioumia ili yeye ashinde, pia amesema kuna kesi kama 18 za watu waliokamatwa walipokuwa wanapigania yeye ashinde.

Amedai wananchi wanamwambia kuwa machozi yao hayawezi kwenda bure asipokwenda kuwatumikia bora maisha yake wananchi wayamalize hapo.

Amedai kuwa anaomba chama chake warudie upya kutazama maamuzi yao, na kama waliyatoa kwa jazba kulingana na yaliyotekea kwenye uchaguzi basi waangalie upya na waelewe kuwa yeye hana amani anatishiwa maisha na amedai hawezi kuhama Rukwa na hawezi kuhama Nkasi.

Amedai kuwa kwa mara ya kwanza kwenye jimbo lao wamepata Mbunge mwanamke na Mbunge wa kutoka upinzani hivyo asipokwenda kuwawakilisha wananchi madhara yake ni makubwa sana kwake aidha hata kama viongozi wake hawatayaona.

Amesema alisharipoti Polisi kuhusu kutishiwa maisha na pia msimamo huo si wake peke yake bali ni wake na viongozi wa mkoa wa chama cha CHADEMA.

Amesema katika ngazi ya taifa hakuna kiongozi yeyote aliyemtafuta hata kwa simu aweze kujua amani yake au usalama wake.

Amedai kuwa alipoomba nafasi ya Ubunge aliomba peke yake na wala hawakuomba 2 wala 3 hivyo atakwenda bungeni kama yeye Aida na atakwenda kuwasilisha sauti yake yeye peke yake kwa niaba ya wananchi wa Nkasi japo atakuwa mpweke ndani ya bunge. Anasema alipokuwa mbunge wa viti maalum alijifunza kutoka kwa wabunge waliomtangulia lakini kama wabunge wa Viti Maalum watakwenda kipindi hiki atapata faraja lakini wasipokwenda itakuwa mpweke lakini faraja atapata kwa wananchi waliomchagua anaowawakilisha.

Tundu Lissu nae anena haya
Tundu Lissu anena kuwa, keshokutwa watakaa kamati kuu na ndio itatoa msimamo wa jumla wa chama, msimamo ambao waliusema wiki iliopita ni msimamo wa viongozi wakuu wa chama, lakini lazima kamati kuu itoe baraka zake au ikatae kutoa baraka zake.

Tundu Lissu amedai kuwa wao hawakua na wajibu wa kuuliza yeye Aida anafikiriaje kwa kuwa wao viongozi wakuu wana majukumu mengine ndani ya chama, amedai kuwa wao walitoa msimamo wao kuwa huo haukuwa uchaguzi.

Amedai kuwa kama chama kikisema kuwa huo ndio msimamo wa chama basi itabidi atafute utaratibu mwingine wa kuwatumikia wananchi wa Nkasi kwa kuwa Tanzania hakuna mbunge binafsi bali ni wabunge wa chama hivyo wabunge ni lazima wafuate utaratibu wa chama.
Ajira zenyewe hakuna,mwacheni dada wa watu akijitafutie maisha huko,asipoenda mtakuwa mnamuonea tu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wao walienda na mishahara wakapata.
Wanataka dada wa watu asiende kuwawakilisha wananchi wake.
Dunia ina mambo hii[emoji1787]

Ila huyo dada anajua kujiongeza,kwa namna yoyote aende bungeni akale mahela yake hayo.

Ni wabinafsi mno, hawa hata wakija kushika dola watakuwa Kama CCM tu!

Wajanja sana,
Mbowe tar 26 allikuwa anapiga hesabu saa kuwa PM
Ingetokea yeye na Lisu wameshinda na Aida na wengine wote wameshindwa..angeuachia kweli huo uwaziri mkuu aliokuwa anaweweseka nao ?[emoji1787]
Wanasiasa wa binafsi Sana binafsi sionagi tofauti ya ccm na CDM maana wako ka mamba Ila kwenye mito tofauti ya maji.
 
Back
Top Bottom