Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kamati Kuu itakaa kutoa msimamo rasmi juu ya Mbunge wa Nkasi, Aida Khenan

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kamati Kuu itakaa kutoa msimamo rasmi juu ya Mbunge wa Nkasi, Aida Khenan

Watu wa Nkasi wanajua kilichotokea uchaguzi huu TZ. Msifikiri watu wa huko mashambani hawana akili.
Hilo jimbo la Nkasi miaka yote lilikuwa mali ya CCM, siwezi kuthibitisha moja kwa moja km walikuwa wanaibiwa au vipi, nachoamini this time Chadema wamelichukua kihalali kwasababu ya nguvu waliyonayo, sasa ni vyema kuitunza hiyo nguvu for future use.
 
Mkuu bila kupinga maelezo wala mapendekezo yako, kwahiyo unaona ni sawa uchaguzi kwa sasa kufanyika kwa wizi, na yoyote atakayepata katika mazingira ya wizi watu wasichukue hatua yoyote.

Mimi kwangu nadhani huyo dada aachwe aende bungeni kutafuta kipato maana maisha ni magumu. Lakini hakuna lolote linaenda kujadiliwa humo ndani zaidi ya kumsujudia Magufuli, na kutaka kumuongezea muda wa kukaa madarakani.
Hatua gani wachukue mkuu wakati tuliambiwa tuandamane tumegoma sasa wao wafanyeje Kama nguvu ya umma imegoma?
(Maana yake wanamuunga mkono Magufuli)

Hao wapinzani kwenye bunge lililopita walijadili nini Cha maana? zaidi ya kususia vikao vya bunge, kujifunga midomo na kuondoka bungeni.
Tuwaache tu hao ccm wakajadili mana hao wapinzani hata wakienda huko bungeni hawana msaada wowote zaidi ya hasara tu kwenye majimbo yao.
 
Usijidanganye. Mkurugenzi wa Nkasi asingetangaza CHADEMA kushinda bila maagizo toka juu. CHADEMA wamepewa tu hicho kiti cha Nkasi.
CHADEMA kwanza kabisa wampongeze kwa jitihada zake za kupambana na Chama dhalimu cha CCM na kushinda kwa kishindo pamoja na madiwani 10. CHADEMA kiendelee kufuatilia kilichompata Msimamizi ambaye hakutii agizo toka juu akamtangaza mwanachama wao mshindi pekee licha ya kuwa analipwa mishahara, amepewa Gari zuri na nyumba kubwa. Akifukuzwa kazi utakuwa ushindi wa pili wa Mh. Mbunge!
 
Watu wa Nkasi wanajua kilichotokea uchaguzi huu TZ. Msifikiri watu wa huko mashambani hawana akili.
Kwahiyo wewe ndio una akili kuliko watu wote wa Nkasi walio mchagua huyo Mbunge?
 
Kila kitu kinawezekana. Mna TISS, JW, Bunge, Mahakama, NEC, Mamlaka ya Anga, TCRA, polisi, Msajili... Amuweni tu mnavyotaka.
Acheni uongo mambo ya Trump hatuyataki toeni ushahidi vinginevyo ni uzushi
 
Not my political maturity, but seems my contribution on this matter didn't hurt your expectations, as used to be on other issues.
We have lost election, nights turn to days, and days turn to nights but we want to remain where we were on 2rd of November.

We need to move on but more carefully, organise our party, seal efficiently all the loopholes which made us get the same negative results in all major political contest we participate.

We need to re-organise our party's systems, organisations and leadership particularly the upper echelon tandem and partinent to our countrys' electoral requirements.

We should also forster unity among rank to file of our members for 2025 General election contest.
 
Acha ujinga. Trump anaingiaje hapa? Mimi nimemjibu mchangiaje alisema 2025 vyama vingi vitafutwa. Wewe unaleta habari ya Trump. Una akili hata ya kutawaza bila kubaki na uchafu mkononi wewe?
Acheni uongo mambo ya Trump hatuyataki toeni ushahidi vinginevyo ni uzushi
 
Hii issue ya huyu dada iko complicated, maamuzi ya kamati kuu lazima yaheshimiwe, kama kamati kuu wakiamua hawautambui ule uchaguzi maana yake hata huyo dada ubunge wake utakuwa batili, lakini kama kamati kuu wakisema hawautambui uchaguzi halafu tena wapeleke viti maalum bungeni nayo kamati kuu itakuwa feki kwa maamuzi yake, hapa lazima wakose wote (huyo dada na viti maalum).

Huyo dada akiambiwa asiende bungeni maana yake atahesabiwa vikao na Ndugai, vikitimia idadi inayotakiwa atavuliwa ubunge kwasababu ya utoro (refer Nassari), sasa hap sijui Ndugai atafanya hivyo, au ataamua kumlinda kama alivyofanya kwa kina Silinde na wenzake (hii nayo itakuwa movie nyingine).

Lakini pia kuna maamuzi ya wananchi wa Nkasi- Kaskazini, hawa nao muhimu wafikiriwe, wamefanya maamuzi ya kishujaa kumchagua huyu dada awe muwakilishi wao bungeni, uamuzi wa kumkataza kuhudhuria vikao vya bunge vinaweza sababisha Chadema kupoteza wapiga kura kwenye hilo jimbo mbele ya safari.

Another option, wamuache huyo dada aende bungeni, hao wabunge wengine wa Chadema wanaoamini wameonewa waende mahakamani, japo mahakama ni za CCM, wakajaribu huko tuone itakavyokuwa.

Sasa hapa kamati kuu kazi kwao, mkiususia uchaguzi mjue nanyi kuna uwezekano mkasuswa na wana Nkasi.
Sasa wananchi wa Nkasi walimcaguaje mkuu kama tumeshakubaliana uchaguzi ni batili?

Naomba maelezo kidogo mkuu umeniacha.
 
Sasa wananchi wa Nkasi walimcaguaje mkuu kama tumeshakubaliana uchaguzi ni batili?

Naomba maelezo kidogo mkuu umeniacha.
Nadhani angesema kuwa wananchi wamemchagua.. Na wakampambania atangazwe.. Maana show haikuwa rahisi.. Mpka kutangazwa..
 
Wamegawiwa jimbo kama vile unavyompa mtu karanga... Unafikiri nguvu ya NEC, TISS, JW, polisi nk iliyotumika nchi nzima ilishindwa Nkasi? Usijidanganye. Hata kama wangeshinda kwa kura, unafikiri mkurugenzi alilazimishwa kumtangaza huyo dada na wapigakura? Wangetaka, mkurugenzi angetangaza CCM ni mshindi. Nkasi wamepewa kama unavyompa rafiki karanga 2-3 ili naye atafune.
Madiwani 10 waliopatikana Nkasi ,nao wanalitangazwa kwa maagizo kutoka juu?

Huna akili kabisa kenge wewe.
 
Nadhani angesema kuwa wananchi wamemchagua.. Na wakampambania atangazwe.. Maana show haikuwa rahisi.. Mpka kutangazwa..
Oouh...

Mkuu wananchi wa Nkasi walitumia mbinu gani kupambana hadi akatangazwa?

Unaweza kufafanunua mkuu majimbo mengine upinzani walishinda ila wakashindwa kutangazwa....wananchi walishindwa wapi kupambana.
 
Viongozi wa CHADEMA wabinafsi sana. Kwahiyo mnapaswa kupata wabunge wangapi ili ionekane hamkufanyiwa rafu?
 
Wewe ndio hauna akili. Kama umekwishasahau yaliyotokea juma 1 tu lililopita, utakuwa na akili ya kuku. Kuku ndio anafukuzwa halafu mara hiyo anasahau na kurudi. Kwa hiyo unataka kusema wapigakura walimlazimisha Mkurugenzi kuwatangaza hao madawani? Akili yako ni chini ya akili ya kuku.
Madiwani 10 waliopatikana Nkasi ,nao wanalitangazwa kwa maagizo kutoka juu?

Huna akili kabisa kenge wewe.
 
Madiwani 10 waliopatikana Nkasi ,nao wanalitangazwa kwa maagizo kutoka juu?

Huna akili kabisa kenge wewe.
Unamaanisha huyu🐊
Nimecheka sana ulivyomalizia😂😂😂
 
Maisha ni magumu sana jamani CHADEMA muacheni tu huyo mama aingie bungeni kwani hana anachoenda kufanya zaidi ya kula posho

Wakimzuia watakuwa wamewazuia wananchi
 
Jamaa wabinafsi sana

Lowassa 'alipoibiwa'kura hawakususa kwenda Bungeni kwa kuwa wao walipata Ubunge

Slaa 'alipoibiwa' kura wao hawakususa kwenda Bungeni kwa kuwa wao walipata Ubunge

Safari hii kwa kuwa wao binafsi 'wameibiwa' wanataka hata 'wasioibiwa' wasuse
Ila kweli [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa wabinafsi sana

Lowassa 'alipoibiwa'kura hawakususa kwenda Bungeni kwa kuwa wao walipata Ubunge

Slaa 'alipoibiwa' kura wao hawakususa kwenda Bungeni kwa kuwa wao walipata Ubunge

Safari hii kwa kuwa wao binafsi 'wameibiwa' wanataka hata 'wasioibiwa' wasuse
Kweli kabisa ,hata mimi nimewashangaa , nimeamini CHADEMA ni wabinafsi, hata huruma nao Kwa walichofanyiwa inaanza kuniondoka

Wanamuonea wivu Aida sababu wao wamekosa , Je Mbowe angeshinda wangesusa ?
 
Back
Top Bottom