Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kamati Kuu itakaa kutoa msimamo rasmi juu ya Mbunge wa Nkasi, Aida Khenan

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kamati Kuu itakaa kutoa msimamo rasmi juu ya Mbunge wa Nkasi, Aida Khenan

Tatizo huyu dada hana msimano imara, siku ya kwanza yeye ndiye alikua wakwanza kusema kua "kutokana na uchaguzi ulivyorubuniwa sijafurahishwa na ushindi wangu hata kama nimeshinda hivyo nitafata kile kitacho amriwa na wakubwa wa chama changu"
 
Hii issue ya huyu dada iko complicated, maamuzi ya kamati kuu lazima yaheshimiwe, kama kamati kuu wakiamua hawautambui ule uchaguzi maana yake hata huyo dada ubunge wake utakuwa batili, lakini kama kamati kuu wakisema hawautambui uchaguzi halafu tena wapeleke viti maalum bungeni nayo kamati kuu itakuwa feki kwa maamuzi yake, hapa lazima wakose wote (huyo dada na viti maalum).

Huyo dada akiambiwa asiende bungeni maana yake atahesabiwa vikao na Ndugai, vikitimia idadi inayotakiwa atavuliwa ubunge kwasababu ya utoro (refer Nassari), sasa hap sijui Ndugai atafanya hivyo, au ataamua kumlinda kama alivyofanya kwa kina Silinde na wenzake (hii nayo itakuwa movie nyingine).

Lakini pia kuna maamuzi ya wananchi wa Nkasi- Kaskazini, hawa nao muhimu wafikiriwe, wamefanya maamuzi ya kishujaa kumchagua huyu dada awe muwakilishi wao bungeni, uamuzi wa kumkataza kuhudhuria vikao vya bunge vinaweza sababisha Chadema kupoteza wapiga kura kwenye hilo jimbo mbele ya safari.

Another option, wamuache huyo dada aende bungeni, hao wabunge wengine wa CHADEMA wanaoamini wameonewa waende mahakamani, japo mahakama ni za CCM, wakajaribu huko tuone itakavyokuwa.

Sasa hapa kamati kuu kazi kwao, mkiususia uchaguzi mjue nanyi kuna uwezekano mkasuswa na wana Nkasi.
 
Ikitokea wakamfukuza CHADEMA huyo dada, basi na mimi Kadi yangu ya CHADEMA naichoma moto. Mwache dada wa Nkasi aendelee kuwawakilisha Wafipa
 
Ndio maana watu wengine wanakosa Imani katika vyama vya upinzani. Inaonakena watu wanatafuta maslahi tu. Mazingira ya uchaguzi huu hayaruhusu kabisa mbunge na madiwani wa CHADEMA kukaa meza moja na CCM. Mtaka mabadiliko yeyote hawezi kabisa. Mtaka kipato hatojali...
Tatizo huyu dada hana msimano imara, siku ya kwanza yeye ndiye alikua wakwanza kusema kua "kutokana na uchaguzi ulivyorubuniwa sijafurahishwa na ushindi wangu hata kama nimeshinda hivyo nitafata kile kitacho amriwa na wakubwa wa chama changu"
 
Unataka kutuaminisha kuwa CHADEMA wameshindwa pote isipokuwa Nkasi tu? Mtu mzima yeyote mwenye akili ameona kilichotokea. Maamzi ya kibunge ni maamzi ya kijumla. Mtu mmoja kwenye wengine zaidi ya 200 wa CCM atafanya nini? Ama unazungumzi uwakilishi wa aina gani. After all, umeambiwa kuwa kwenye wabunge wa upinzani hawatapeleka maendeleo.
Lakini pia kuna maamuzi ya wananchi wa Nkasi- Kaskazini, hawa nao muhimu wafikiriwe, wamefanya maamuzi ya kishujaa kumchagua huyu dada awe muwakilishi wao bungeni, uamuzi wa kumkataza kuhudhuria vikao vya bunge vinaweza sababisha Chadema kupoteza wapiga kura kwenye hilo jimbo mbele ya safari.
 
Kila chaguzi mliiba lakini 2020 ilikuwa record breaking! Hata watoto wadogo wameyaona makaratasi ya kura yakizagaa mtaani!
Hivi angekuwa Mbowe tu ndo pekee aliepita kwenye Ubunge angeletewa zengwe kama anvyoletewa huyu dada Khenan?
 
Binafsi huwa napendekeza kama upinzani haukufikisha akidi kwenye bunge wawe wanaachia tu ngazi hata kama uchaguzi ukiwa wa huru na haki.

Kuwakilisha wananchi pekee hata hao wa chama tawala wanaweza.

Upinzani usiodhibiti chombo chochote cha maamuzi ni useless tu kwa hizi nchi zetu.

Kuisimamia serikali unahitaji akidi ili u negotiate nayo kwenye kila kitu bungeni.

Swali:Kwa hiyo wakimpiga pin huyo Aida Khenani maanake hata wale wa viti maalumu hawatapeleka majina?
 
Unataka kutuaminisha kuwa CHADEMA wameshindwa pote isipokuwa Nkasi tu. Mtu mzima yeyote mwenye akili ameona kilichotokea. Maamzi ya kibunge ni maamzi ya kijumla. Mtu mmoja kwenye wingine zaidi ya 200 wa CCM atafanya nini?
Ndio maana nikasema hii issue ni complex, ina majibu mengi, CHADEMA kushinda Nkasi inaweza kuwa ni first step ya chama kuenea kwenye majimbo mengine ya jirani depending on how huyo dada ata perform bungeni, now anaangaliwa kama role model, sasa wakisema asiende bungeni sioni shida ni maamuzi yao, lakini wajue watakuwa wanarudi nyuma kwenye hilo jimbo na mengine ya jirani.

Lakini kubwa zaidi, kama wakisema hawautambui ubunge wa huyo dada, basi hata viti maalum navyo wasivitambue, nadhani hapo ndio watakuwa wanamaanisha vizuri, lakini km viti maalum wataenda bungeni, basi na huyo dada aende pia, na automatically watakuwa wameyakubali matokeo ya jumla ya ubunge nchini.

Kazi kwao.
 
CHADEMA kwanza kabisa wampongeze kwa jitihada zake za kupambana na Chama dhalimu cha CCM na kushinda kwa kishindo pamoja na madiwani 10. CHADEMA kiendelee kufuatilia kilichompata Msimamizi ambaye hakutii agizo toka juu akamtangaza mwanachama wao mshindi pekee licha ya kuwa analipwa mishahara, amepewa Gari zuri na nyumba kubwa. Akifukuzwa kazi utakuwa ushindi wa pili wa Mh. Mbunge!
 
Umekuja TZ lini? CHADEMA imekwisha enea. Tatizo ni NEC, polisi, Msajili, TISS, JW.Kwa nini unafikiri kura zikapigiwa majumbani na kupelekwa vituoni kwenye vikapu nchi nzima? Ingekuwa siyo tishio, hilo lingefikiriwaje na CCM?
Ndio maana nikasema hii issue ni complex, ina majibu mengi, Chadema kushinda Nkasi inaweza kuwa ni first step ya chama kuenea kwenye majimbo mengine ya jirani depending on how huyo dada ata perform bungeni, now anaangaliwa kama role model, sasa wakisema asiende bungeni sioni shida ni maamuzi yao, lakini wajue watakuwa wanarudi nyuma kwenye hilo jimbo na mengine ya jirani.

Lakini kubwa zaidi, kama wakisema hawautambui ubunge wa huyo dada, basi hata viti maalum navyo wasivitambue, nadhani hapo ndio watakuwa wanamaanisha vizuri, lakini km viti maalum wataenda bungeni, basi na huyo dada aende pia, na automatically watakuwa wameyakubali matokeo ya jumla ya ubunge nchini.

Kazi kwao.
 
2025 watashiriki tena kana kwamba wamesahau ya nyuma...

Tatizo watu hawaelewi na wanajitahidi kukumbuka ulichokiandika.

Unapolalamika na kudai kuibiwa kura huku ukienda mbali zaidi kwa kudai katiba moya na tume huru, unatakiwa uingie kwenye uchaguzi baada ya hayo mambo kutokea, vinginevyo hadithi itakua ni ile ile kila uchaguzi.
 
Umekuja TZ lini. CHADEMA imekwisha enea. Tatizo ni NEC, polisi, Msajili, TISS, JW... Kwa nini unafikiri kura zikapigiwa majumbani na kupelekwa vituoni kwenye vikapu nchi nzima? Ingekuwa siyo tishio, hilo lingefikiriwaje na CCM?
Hilo jimbo la Nkasi miaka yote lilikuwa mali ya CCM, siwezi kuthibitisha moja kwa moja km walikuwa wanaibiwa au vipi, nachoamini this time CHADEMA wamelichukua kihalali kwasababu ya nguvu waliyonayo, sasa ni vyema kuitunza hiyo nguvu for future use.
 
Aunge juhudi fasta, ili ahamie CCM na ubunge wake. Abakie mwenzao wa CUF
 
Akiingia bungeni aungane na CCM kusema ndio ili mkono uende kinywani
 
Wamegawiwa jimbo kama vile unavyompa mtu karanga... Unafikiri nguvu ya NEC, TISS, JW, polisi nk iliyotumika nchi nzima ilishindwa Nkasi? Usijidanganye. Hata kama wangeshinda kwa kura, unafikiri mkurugenzi alilazimishwa kumtangaza huyo dada na wapigakura? Wangetaka, mkurugenzi angetangaza CCM ni mshindi. Nkasi wamepewa kama unavyompa rafiki karanga 2-3 ili naye atafune.
Hilo jimbo la Nkasi miaka yote lilikuwa mali ya CCM, siwezi kuthibitisha moja kwa moja km walikuwa wanaibiwa au vipi, nachoamini this time Chadema wamelichukua kihalali kwasababu ya nguvu waliyonayo, sasa ni vyema kuitunza hiyo nguvu for future use.
 
Back
Top Bottom