Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kamati Kuu itakaa kutoa msimamo rasmi juu ya Mbunge wa Nkasi, Aida Khenan

Usione huruma chadema
Ccm mumeshinda kwa kishindo
Kajengeni arusha iwe carlifonia
 

Usikute mbowe na Lissu hawajampa hongera dada
 
Aaweza kwenda bungeni under protest huku akiwa na msimamo wa chama chake bungeni.
Hii ya kupiga picha na bashiru au kwenda Dodoma kuspishwa Magufuli au kusema aliomba ubunge peke yake inaonekana wazi hajitambui na hana msimamo au kanunuliwa tayari au hio nafasi alipewa tu kwa malengo maalum ya ccm
 
Mkuu mbona unashindwa kujiongeza kidogo? Wizi wa kura mwaka huu haujawahi kushuhudiwa kokote ulimwenguni yaani walifanya wizi wa kitoto mno bora wangefanya wa kisayansi afadhali.

Mwaka huu naamini mwana ccm halisi amejisikia aibu sana kwa kilichotokea ingawaje hawezi kusema hadharani.
 
Naona buku7 wa Lumumba mnakiri waziwazi kwamba CCM ni wezi wa kura!
 
jamaa wananishangaza sana. Wanasema wanataka democrasia lkn kwanin hawatak kumpa mtu nafas ya kufanya maamuzi yake. Wanatak ku dictate kile wanachokiwaza wao ndio kiwe hiko. Muda huo wenye nguvu zaidi yao wakifanya hivo, wanaandamana.

Siasa ni uhun
 
Mbona hujajibu maswali yangu sasa?
 
Mbona hujajibu maswali yangu sasa?
Hawez kujibu , mtu amepata kura million 1 dhidi ya Mili 12 , hata kama umeibiwa ndo kura mil 11, mi niliwaambia kama walikuwa na mawakala , wachukue taarifa za mawakala wao watiifu toka kwenye vituo na watumie kama sample tuone kama Lissu alishinda.....
Mtu mwenyewe kwenye vituo kibao Tu kapata kura 0 alaf mijitu inaropoka ooh tumeibiwa
 
Lengo lao limekamilika wameachia jimbo moja ili kuleta haya yanayotokea sasa.
Naungana na wewe katika mengi lakini kwa hili nakukatalia. AIDA hakupewa ili kubalance game, CCM walitaka kusiwe na Mbunge hata mmoja wa upinzani, ila mbinu za wizi zilizotumika maeneo mengine kama vile vijana wa CCM kuingia na kura mifukoni zilidhibitiwa na vijana wa CDM Nkasi.

Fomu fake za matokeo zilikamatwa kwenye vituo vya majumuisho. Kule Mkuu wa wilaya aliingia kila Kituo lakini alifukuzwa na mawakala ambao waliwekwa kila Kituo, hakukuwa na Kituo kisichokuwa na Wakala wa CDM. Huko kuna Kituo Magufuli kapata kura 13 dhidi ya 200+ za Lissu. Huyu binti wamuache tu, aliwapanga vizuri watu wake na wlimtii na kufanya yanayostahili.
 
Mimi kuna ndugu yangu alisimamia huo uchaguzi na ni mwanachadema kindakindaki.
Nilimuuliza kuhusu hizi tuhuma za wizi alisema kura zimehesabiwa kihalali kabisa na ameyasimamia hayo mabox Hadi yamefikishwa mahali husika.. Anasema labda km sehemu nyingine wamefanya hivyo lakini alipokuwapo yeye mawakala wote walikuwepo.

Anasema upinzani tukubali kuwa safari hii tumedondoka.
 
Kweli aisee wanayumba ni kuwanyima haki wananchi wa nkasi
 
Chadema wanakuwa wajinga kila kuchwao, na hawataki kujifunza,akili yao ni akili ya Mbowe,wekeni vikwazo kwa huyu mdada nae ataenda CCM kwa raha zake na kurudi tena mjengoni. Huyu dada hata akienda chama cha mzee wa ubwabwa atapata kura kibao na kushinda tena.Endelea kujishau tu wakati munalala kwa balozi wa Ujerumani,utadhani hamna makwenu.
 
Nusara itumike .
Huyo dada aachwe mana amefanya kile alichotumwa na chama chake.
Hivi kwa mfano Mdee angeshindaje wakati alikua anaongea bangi majukwaani badala ya mikakati na mipango mizuri ya maendeo?

Hivi Lema angeshinda kwa hoja ipi aliyokuwa nayo?

Kama yupo mbunge wa Upinzani alieshinda na hakutangazwa sheria iko wazi aende Mahakamani?
Hawana ushahidi wowote wa kisayansi japo kweli kura zilipigwa kihuni .
Mdee msomi wa sheria mzima anakamata kielelezo cha kura feki halafu kwa bangi zake kichwani anazichoma moto kupoteza ushahidi tena kumsaidia mtuhumiwa asipatikane na hatia.

Sasa kama unakua na wagombea ubunge hopeless kama Mdee unategemea usiibiwe na wasanii kama Gwajima wanaofanya mazingaumbwe na kuwadanganya waumini kuwa wamefufua wafu kisha kukusanya mabilioni ya pesa ? Utamshindaje Mtu mdanganyifu kama Gwajima anayemdanganya mpaka Mungu na kuwaibia watu kwa ridhaa yao?

Wapinzani acheni kurushiana maneno kwenye mitandao na badala yake kusanyeni ushahidi mlio nao upelekeni hata mahakama ya kimataifa kisha mpeleke kwenye nchi wahisani ili wao waone kama kuna wanaloweza kulisemea au kuliwekea vikwazo.

Vinginvyo kama hamna ushahidi basi kaeni kimya uchaguzi umeisha . Aliyetangazwa ndiye aliyeshinda mana hana pingamizi la kisheria.

Kumfukuza Uanachama kutaleta mjadala mkubwa sana na kuwakatisha tamaa wananchi na wapiga kura wote wanaolinda kura na kuhakikisha ushindi unapatikana. Awe ni mfano wa namna ya kulinda kura.

Aachwe atakuja kujichanganya mwenyewe huko mbeleni na kujikuta anajawa na kiburi wakati huo wananchi watakua wameshasahau na jazba zao kupoa hapo ndipo atatimuliwa bila kupepesa macho.

Kwa sasa aachwe awe ni mbunge aliyepingana na maelekezo ya chama kidemokrasia.
Mkimfukuza mtawatoa wananchi kwenye Reli ya uchaguzi haramu badala yake waramjadili mtu mmoja kuwa ameonewa. Watu watamuunga mkono kuwa ameonewa na chama chake na sio tume.
 
Imagine scenario hii:

Aida ang’ang’anie kuingia Bungeni, CHADEMA wamfukuze uanachama, Aida ahamie CCM,
Uchaguzi mpya uitishwe na CCM wamsimamishe Aida.

CHADEMA wagome kushiriki uchaguzi kwa kuwa hawana imani na Tume, Aida apite bila kupingwa then arudi Bungeni kwa kishindo.

Tutakuwa tumeachieve nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…