Tundu Lissu: Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Yatoka na Maazimio nane dhidi yake

Tundu Lissu: Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Yatoka na Maazimio nane dhidi yake

Hapo spika Job Ndugai ameachiwa zigo zito katika masuala ya kusikitisha yaliyomkumba Mh. Tundu Lissu na pia matamshi / kauli za wabunge wa CCM kina Bulembo na wenzake ktk kikao kinachoendelea Dodoma hivi sasa.

Hawa maCCM wanasahau serikali ya Tanzania imesaini mikataba mingi ya kimataifa inayowabana na pia kuwataka waizingatie na kuwajibika.

Spika anapopewa ushauri mhimili wa Bunge uwe huru, maana yake ilikuwa wanamsaidia akiepuke kikombe hiki cha siki. Lakini hakutaka kusikia sauti zenye hekima.

Sasa Spika atakuwa peke yake na kila mmoja atabeba mzigo wake mwenye siku ya siku ICC The Hague wakimuhitaji kama Gavana wa Dar es Salaam ambavyo serikali inaburuta na kukaa kimya kama vile katazo hawajalisikia au kuliona ktk mitandao.

February 6, 2020
Geneva, Switzerland

Mahojiano na Kamati Ya Ulimwengu ya Utetezi kwa Wabunge wanaofikwa na unyanyasaji na vitisho toka kwa serikali za nchi zao



Source: inter-parliamentart union
www.ipu.org
 
Fight for the rights of persecuted MPs

Fight for strong democratic parliaments serving the people "National Parliaments and citizens should operate in solidarity to put an end to abuses against MPs. It takes persistence. It means NEVER GIVING UP." - President of the IPU Committee on the Human Rights of Parliamentarians Help us to help MPs under threat.



Source: Inter-Parliamentary Union

www.ipu.org
 
Du hueleweki,yaani wewe unajifanya yote uliyosoma hujaelewa.Yeye kupitia huko kote sio kwa bahati mbaya.Kuna sababu maalum na zimeanza kuonekana.Subiri soon utaelewa na utaona matokeo.
Yeye aje tu kuendelea na kesi zake sheria ni msumeno na sheria haina huruma
 
Pole Lisu kwa unayopitia.Asante IPU na wadau wengine. Dunia inapambana kupunguza ama kutoka zama za giza ila shetani yupo anawatumia binadamu wachache kuturudisha gizani. #Hapana mvua risasi Lissu # Hapana kumpoka ubunge Lissu # Hapana dhihaka kwa Lissu # Hapana kumnyima stahiki ikiwemo matibabu Lissu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
'Pressure points' zinaongezeka.

Huku ndani nako ni wakati wa kuanza kushindilia sasa polepole, huku joto likiongezeka kadri Oktoba inavyosogea.

Tundu Lissu aliyeko nje kwa sasa hivi ni wa manufaa zaidi ya Tundu Lissu ambaye angekuwa nyumbani kwa wakati huu.

Haya yalionekana tokea zamani.
 
Corticopontine, Kwahiyo sheria za kimataifa hazifanyi kazi kwa Tanzania kwasababu ni nchi huru?

Shame on you!!

Hivi unajua hata rais hawezi kuingia kwenye ubalozi wowote uliopo Tanzania bila ruhusa ya balozi?

Unafahamu kwamba eneo la ubalozi wowote linahesabika kuwa ni ardhi /himaya ya nchi husika?
Yani ukitenda kosa ukaruhusiwa kuingia ubalozi wa Sweden uliopo Tanzania unahesabika upo Sweden, ukiingia ubalozi wa Marekani upo Marekani na hakuna yeyote anayeweza kuingia bila kibali na kukukamata.

Huo ni mfano wa sheria za kimataifa na Tanzania inatii.

Kama inatii sheria hii itadharauje sheria nyingine ya kimamtaifa iliyosaini kuiamini kuiheshimu na kuwajibika kwayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu hakukosea kuweka Mauti, laiti kifo kingekuwa hakipo, kuna watu wangejipa uMungu.
Hakuna kurudi nyuma, mdogo mdogo tutafika tu.
Pambana kiongozi wangu.
Namhurumia sana Tundu Lisu washauri wake si wazuri mwenzao ni mgonjwa wanamshauri vibaya sana. Anasahau kwamba Tanzania ni nchi huru yenye watu millioni 60+ anasahau kwamba Tanzania ina utawala wa Sheria, kuna mahakama ambayo ndiyo inashughulikia jinai binafsi namhurumia sana angekuwa ndugu yangu wa Karibu ningemuangukia miguuni nikimsihi arudi Tanzania aachane na Mambo ambayo kimsingi Mungu ndiye hupanga kwa mfano kuwa Rais wa nchi huwa ni mipango ya mwenyezi Mungu Tundu Lisu ni masikini asiye na cha kuwaachia watoto wake hata baada ya mauti kumkuta kitu pekee ambacho angeweza kuwaachia watoto wake ni Elimu bora na maadili ya kutii mamlaka za Duniani anayoyafanya Lisu kwa kweli yanasikitisha sana nadhani ashukuru tu kwamba anafanya haya kwenye nchi yenye Rais wenye huruma. Sidhani kama kuna kiongozi yeyote Duniani anaweza kubali nchi yake kuchezewa kiasi hiki
Dunia na Historia yake ni ya ajabu sana.
Miaka 30 ijayo Mbele watoto na wajukuu wa Tundu Lisu iwe akiwa hai au akiwa ameuawa vyovyote vile ,watakua wanajeshimika na kupewa nafasi kubwa sana kutokana na anayoyafanya Tundu Leo. Wale wanaohshimika na kujiona miungu watu Leo kwa kumwaga damu za watu kutetea matumbo yao watapotea kabisa na vizazi vyao.

Fanya kila kitu lakini epuka sana kumwaga damu ya binadamu asiye na hatia kwako.
Damu imwagike tu kwenye vita au wakati wa mapambano kama kuzuia ujambazi na majambazi lakini sio kumwaga damu ya MTU unayeweza kumjibu kwa hoja na ukaeleweka na kama hueleweki basi wewe ndio unakosa kibali kwa Mungu unalazimisha kwa kutumia damu za watu.

Dunia inajaa laana kubwa sana na majanga makubwa kutokana na Damu za watu wasio na hatia zilizotangulizwa na watu waovu kwa kujifariji kuwa wanasaka maisha bora.
Na bado dunia na wanadamu wa kizazi hiki cha uasi kitapata mapigo makubwa sana sana miaka michache sana ijayo,ikiwemo vita kubwa sana na mgonjwa yasiyo na tiba na mafuriko ,njaa Kali, kimbunga na matetemeko makubwa.
Dunia haitakua na amani kwa wenye nguvu kuwaangamiza wasio na nguvu. Ni kosa kubwa sana.

Tundu Lisu amefanyiwa jambo baya sana kwenye maisha yake kuliko kitu chochote. Pale alipo sala zake zote sio fedha wala Utajiri ni kuona waliomfanyia hivyo Mungu anawalipa kwa mapigo makali wao na vizazi vyao.
Tundu alianza kupigania maslahi ya nchi wakati wanaojipigania nafsi na nafasi zao walikua wakigawana nyara za ufisadi na wakajineemesha wao na familia zao na kujaza matumbo yao na Mali za kusaza.
Walioshiba kupitia Mali za umma ndio waliosoma upepo wa watanzania na kujigeuza kinadharia na midomoni mwao na kujiita wazalendo huku wakiwafunga midomo wazalendo wa kweli ili wasionekane machoni mwa wananchi kwa kuzuia Bunge live na vyombo vya habari kutoa nafasi sawa kwa wote.

Tundu Lisu atatetewa na wanadamu wenzetu waliojaa dunia nzima.
Tanzania sio Mali ya ya mtu mmoja wala kundi la watu Bali ni Mali ya Mungu.
Dunia na Tanzania iliwahi kuishi viumbe vingine na enzi zao zikapita na vikatoweka ikabaki historia na mabaki tu kama yale ya Mjusi mkubwa kule mtwara na mafuvu kule Olduvai Gorge. Kwa hiyo hakuna wa kujisifu kuwa hii nchi ni ya kwake na ana amri juu ya Hatma ya kiasili ya viumbe wa dunia hii mana hata maisha yake ni ya muda tuu.

Kuba mabilionea waliacha kila kitu wakaenda kulala mavumbini.

Tukiona tuna haki zaidi ya wengine na kuamua kumtupa Tundu basi Watakuja hata viumbe toka sayari nyingine kumtetea kama Mungu amepanga aishi hapa duniani kwa wakati huu na awamu hii.

Vita inaanza pale ambapo watu wawili ,kila mmoja anataka kumuua mwenzake.
Ukiona mmoja anafurahia na kujitamba kwa raha kuwa atamuua mwenzake ujue huyo mwenzake ni mpenda amani.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora aje afungwe bila hatia kuliko kuuawa bila hatia. Akifungwa Atatoka tu siku moja. Gerezani sio Jehanamu.

Hata Mandela alifungwa lakini alitoka.
Dunia ya Leo wazo halipigwi Rungu linajibiwa kwa wazo bora zaidi.

Mungu alivuomnusuru Tundu Lisu ni binadamu tu aliyelewa damu ya watu anayeweza kushika tena bunduki na kumlemga Tundu. Hiyo hata hela atakayoilipwa kwa tendo hilo itakua ni laana kubwa kwa kizazi chake chote huku waliomtuma wakiendelea kula bata na kujilimbikizia Mali kupitia madaraka.

Zamani wauaji wa watu wasio na hatia walifanyiwa Tambiko maalumu na kuangamia wao na koo zao zote.

Wako wapi mashehe wanaoweza kusoma Alba dir kwa wauaji??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo Barua ya maamuzi ya IPU iko wapi ?

Barua inasema "kama mtakavyoona kwenye maamuzi ya IPU" lakini kiambatanisho cha hayo maamuzi kutoka IPU hakipo jamani.

Naomba nasi tupate nakala hapa kama itawezekana kwa wahusika.
 
Back
Top Bottom