Tundu Lissu: Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Yatoka na Maazimio nane dhidi yake

Tundu Lissu: Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Yatoka na Maazimio nane dhidi yake

Hapo spika Job Ndugai ameachiwa zigo zito katika masuala ya kusikitisha yaliyomkumba Mh. Tundu Lissu na pia matamshi / kauli za wabunge wa CCM kina Bulembo na wenzake ktk kikao kinachoendelea Dodoma hivi sasa.

Hawa maCCM wanasahau serikali ya Tanzania imesaini mikataba mingi ya kimataifa inayowabana na pia kuwataka waizangatie na kuwajibika.
Hivi wewe unajua Tabia ya fisi kwenye chakula alivyo halafu unasema naenda mikumi mbuga za wanyama kutembea unapanda basi la kwenda Sumbawanga likifika Mikumi katikati unaomba kushuka eti umefika. Abiria wenzako wanakuonya hapa ni hatari, unalazimisha unashuka - ghafla unakutana na fisi unaiuliza eti hapa Mikumi Hotel ipo wapi? Ndipo fisi ananyanyua kichwa kama anasema ipo hapo mbele wewe unamuambia tena fisi naomba nisindikize nisishambuliwe na Simba unageuka unaanza kwenda hotelini. Fisi yupo mgongoni anakufuata tu nyuma yako. Hujafika hotelini, alhamdililah Simba huyu hapa unageuka kumwangalia Mlinzi wako fisi unakuta patupu kumbe amefichama anasubiria alichotegemea mabaki yako.

Kwa hiyo fisiemu(CCM) sio wa kuwaamini kwenye mikataba nadhani umeona mikataba walioingia.

(1) Waziri wa Polifisiemu amesaini mkataba wa TZS tirioni 4 ili tusiwe tunaibiwa yeye mwenyewe kaiba kabla mkataba hujaanza kazi na kwenye mkataba tu kaiba tayari

(2) Huku tena Waziri wa Fedha kaingia mkataba na watu wametupa pesa tutokomeze Malaria tununue vyandarua wafadhili wanamuuliza hela yetu mmefanyia nini na ipo wapi maana vyandarua hatuvioni yeye anajibu kirahisi tu eti Mimi nimesomea na Nina PhD 4 za debit na kredit haya mambo ya madawa mimi siyajui labda tuwaulize kwenye PhD za maralia kama wamenunulia piriton watanzania walale salama

(3) Nasubiri majibu ya Ndugai kuhusu huo mkataba na IPU alioingia na michango ya kina mheshimiwa Bulembo na mheshimiwa Mama Rwakatare nitaona kumbe kwenye mihimili hii nako kuna kukanyigishana mafuta na waumini ndiyo hao kina mheshimia Rwakatare na Bulembo na Ndugai ni mshereheshaji mkuu
 
Serikali ya CCM Mpya inapitia katika wakati mgumu sana. Yote hii ni kutokana na maovu mengi waliyoyafanya.

Mbali na mbinyo wa Jumuiya za Kimataifa (IPU, Dalili za vikwazo, Sweden, World Bank n.k) CCM Mpya hayajiulizi pia hizi mvua zisizo isha zinazoharibu miundombinu na kutishia baa la njaa na kutoboa matundu makubwa ktk fuko la TRA linalosemekana kufanya makusanyo ya ki-rekodi ya 'serikali tajiri dona kantri' ni mtihani mwingine mkubwa toka wapi?!



Source: TRC Reli TV
CCM Mpya ijitafakari, itubu na kuacha njia zake ovu ili iepukane na gharika ya aina zote za mitihani hii yote. Ama sivyo anguko kubwa lipo njiani na linakuja kwa kasi.
 
majitu haya kama kweli hayakuhusika,kwanini hawaruhusu uchunguzi huru wa jaribio la mauaji ya lissu?.
 
Lissu anatafuta sababu ya kurudi Tz, alisema harudi Tz hadi ahakikishiwe usalama wake, je saivi IPU ndio imemuhakikishia usalama wake? IPI ina mamlaka gani Tz ? Hakuna mtu anayeweza mrudishie ubunge tena, aje apambane upya Oct 2020 tu .
 
Lissu anatafuta sababu ya kurudi Tz, alisema harudi Tz hadi ahakikishiwe usalama wake, je saivi IPU ndio imemuhakikishia usalama wake? IPI ina mamlaka gani Tz ? Hakuna mtu anayeweza mrudishie ubunge tena, aje apambane upya Oct 2020 tu .
Wala hiyo si agenda yake lakini kwakua Tanzania tumezoea kupoteza facts subirini matokeo.
 
Mkuu Infomer siku nyingine sahihisha matumizi ya neno"dhidi" katika sentensi zako.
Hapo umelitumia neno vibaya,Heidi(AGAINST) ni kupingana,badala yake ilibidi useme"JUU" ,au pia ungeweza kutumia neno"KUHUSU".
Samahani lakini.
 
Huyu jamaa arudi kugombea urais tu, sioni mtu mwingine ambaye anaweza mpa wakati mgumu kidogo jiwe, huyu angalau ataleta challenge kidogo.
 
Namhurumia sana Tundu Lisu washauri wake si wazuri mwenzao ni mgonjwa wanamshauri vibaya sana. Anasahau kwamba Tanzania ni nchi huru yenye watu millioni 60+ anasahau kwamba Tanzania ina utawala wa Sheria, kuna mahakama ambayo ndiyo inashughulikia jinai binafsi namhurumia sana angekuwa ndugu yangu wa Karibu ningemuangukia miguuni nikimsihi arudi Tanzania aachane na Mambo ambayo kimsingi Mungu ndiye hupanga kwa mfano kuwa Rais wa nchi huwa ni mipango ya mwenyezi Mungu Tundu Lisu ni masikini asiye na cha kuwaachia watoto wake hata baada ya mauti kumkuta kitu pekee ambacho angeweza kuwaachia watoto wake ni Elimu bora na maadili ya kutii mamlaka za Duniani anayoyafanya Lisu kwa kweli yanasikitisha sana nadhani ashukuru tu kwamba anafanya haya kwenye nchi yenye Rais wenye huruma. Sidhani kama kuna kiongozi yeyote Duniani anaweza kubali nchi yake kuchezewa kiasi hiki

Hapo mkuu kuna kisehemu Umesema UONGO Huenda ni kwa kutokujua. Duniani Mamlaka zinaweza kuwekwa na SHETANI, si mamlaka Zoote za kiserikali /Kiutawala zimewekwa na Mungu ...,zipo zilizowekwa na "vimungu"

Mungu huwa hachakachui Anaweka jambo kwa HAKI na UHALALI. hivyo ukiona jambo limefanyika ki-UCHAKACHUZI hapo ni USHETANI na MUNGU MUUMBAJI HAUSIKI.

Jingine si mara zote tunapaswa kutii mamlaka zote. Kama nilivyosema hapo juu Kuna mamlaka zimewekwa na SHETANI ama KISHETANI. na mamlaka hizi wakati mwingine hutoa Amri zenye Mlengo wa kumtukuza SHETANI,
HITIMISHO :- Tunapaswa kutii Mamlaka katika kweli na Haki si katika Ukengemfu mbele za Bwana.
Kaa chonjo Acha kutisha na kuhadaa watu Huo ni Usheikhtwani. KUWA MAKINI Usitumike kama ZANA.
 
Kweli mfa maji haishi kutapatapa.

Ushauri tu Lissu: Kama bado unautaka ubunge muda wa miezi kadhaa tu umebaki, gombea tena sio kulialia tu!
 
Bado ni maombi! Je! Yatakubaliwa? - for your information: Tundu Lissu is not a parliamentarian any longer!
Msifurahi mwanzoni.
Kwa nini Kapeleka Malalamiko na yamefanyiwa kazi kwa kiwango hicho kilicho elezwa.
Kasikilizwa kama Mbunge alietenguliwa kwa fitina , Haya mambo yanazidi kutuvua nguo. ni bora kusimamia Kweli na Haki na tukarudi kwnye Tanganyika ilee yenye uzalendo wa kweli kuliko hizi blablaa.
 
Back
Top Bottom