Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Katika miaka hii mitano kila Mtanzania awe ni tajiri au maskini ana hadithi yake ya maumivu

Hujui kina lissu ndio Wasaliti wa Nchi? Wanatumiwa na Mabeberu kuiba raslimali zetu
Umeonyesha udhaifu wa akili hapa. Nakumbuka muswada wa Gas na petroleum . Mpaka kina Lissu na wapinzani kwa ujumla wao walitoka nje ya bunge usiku wa manane ili usipitishwe kwa hati dharura. Nini kilitokea ulipitishwa na Leo Mzee analalamika kuwa Gas na petroli si yetu !!.

Mikataba mibovu imeingiwa na waroho wa Ccm si kina Lissu.
 
Lissu hajui sheria kuongea kwa sauti ya juu mahakamani na kuropoka sio kuwa gwiji wa sheria
Ugwiji wa sheria ndiyo umemfikisha Lissu hapo alipo. Wewe piga debe lakini huwezi kumfikia . Kumchukia mwenye uwezo wake siyo kumfikia [emoji23][emoji1787]
 
Sisi Watanzania wazalendo tunafurahi uongozi wa Rais Magufuli

Wanaotumika na Mabeberu wamezibiwa mirija ndio hao wanalia
Mkuu mabeberu unamaanisha wale wazungu waliohaidi kuwapa mkopo wa mamilioni ya dola baada ya kukubaliana na masharti yao mkashangilia km zile hela mliokota, au tayari mshapewa hizo helaa?!!
 
Bado najaribu kuwaza hivi J.P.M atawambia nini watu wa Kilombero akija kwenye kuomba kura ikiwa alitoa ahadi mwaka 2016 kuwa atahakikisha barabara ya Mkamba-Ifakara inajengwa kwa kiwango cha lami. Lakini tokea 2016 mpaka leo bado hata harufu ya lami lami hakuna. Barabara ya kipande kifupi imemchukua miaka zaidi ya mitatu kuikamilisha
 
Wanaccm wakiambiwa ukweli hawataki kusikia wala kuamini
 
Maumivu yangu ni kuongezewa asilimia ya makato bodi ya mikopo elimu ya juu.Tumefanyiwa ukatili sana
 
Sisi Watanzania wazalendo tunafurahi uongozi wa Rais Magufuli

Wanaotumika na Mabeberu wamezibiwa mirija ndio hao wanalia
Hatujalipwa pesa za korosho huku Lindi,mimi mkulima natumikia beberu?wewe jike au beberu?
 
Hadithi kutokupandishiwa mshahara kwa miaka mitano while bidhaa zinapanda bei kwa kasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…