Tundu Lissu kila nikijilazimisha nimuone wa maana, moyo unagoma tu, simpendi na sipendi awe kiongozi kokote kule!

Huyu lissu mtu wa ovyo sana hafai kuongoza hata mtaa hapa tz. Ni kibaraka mkubwa wanajitahidi mabwana zake wa ulaya aongeze nchi ili awakabidhi. Nashangaa unapoteza muda kumchambua kibaraka huyu.
Kuna nini cha kuwapa wazungu hapa nchini? Na ni kipi wazungu wanakikosa sasa hivi, hadi Lisu awe kiongozi ndio wakipate? Kama tuna hicho cha maana hadi wazungu wanakitaka, huu umasikini ni wa nini wakati tuna mali wazungu wanasubiri wapewe na Lisu? Kwanini nyinyi msikitumie kumaliza huu umasikini ulioshika kasi?
 
Sijapinga sifa zake zote za kuwapigania wananchi mkuu, shida yake moja ni kutoamini kwamba nchi yetu inauhuru na kwamba sisi tunaweza kumaliza mambo yetu bila mkono wa mzungu
Ni uhuru upi tuliokuwa nao kama watu walikuwa wanahoji wanashambuliwa kwa risasi, wanatekwa, wanauawa na kupotezwa?

Ni uhuru upi ulio nao wewe wakati asilimia 40% ya bajeti ya nchi yako inategemea wazungu? Kama unamchukia Lisu kwa sababu ya wazungu, basi utakuwa unamchukia kila mtu wa nchi hii. Utakuwa unamchukia Rais na Serikali yote kwa sababu wanaenda kuomba misaada na mikopo kwa wazungu kwaajili ya nchi hii unayoamini ni huru na ina uwezo wote. Utakuwa unawachukia watoto wote na wazazi wao kwa maana wanatumia chanjo za kupewa na wazungu wakati sisi ni Taifa huru. Utakuwa unawachukia wote wanaotumia barabara tulizojengewa na wazungu wakati sisi ni Taifa huru, tulitakiwa tujenge wenyewe. Utakuwa unawachukia wananchi wote wa vijijini waliopelekewa umeme kwa 80% kwa pesa ya MCC toka Marekani. Kwa nini tusambaziwe umeme na wazungu wakati sisi ni Taifa huru? Na utakuwa unawachukia waafrika wote na waarabu ambao nchini mwao kunapokuwa na mapigano, wanakimbilia nchi za wazungu badala ya kwenda kwenye nchi za waafrika wenzao na waarabu wenzao. Utakuwa unawachukia na wale vijana waafrika wa nchi za kaskazini mwa bara la Afrika ambao kila siku wanafia baharini wakati wakihangaika kuingia Italy badala ya kuja Tanzania kutafuta maisha.

Lakini kwa wanaojielewa, wanafahamu giza lililopo kwenye tawala za Afrika. Na hiyo ndiyo inayowafanya wawatafute wazungu kusaidia kutatua changamoto nyingi za ndani ya mataifa yao.
 

Kama hata hapa Kisamv, hataelewa, basi atakuwa ana shida sana.
 
"Mchawi hajawahi mpenda mpiga maombi" alisikika mzee mmoja aliyekuwa kwenye daladala ya kwenda chamanzi.
 
Ninaunga mkono hoja
Umenena kama yalivyo Mawazo yangu.
Huyu jamaa hakika ni mwanaharakati na hafai kabisa kuwa kiongozi yeyote
Iwe wa chama au kiongozi serikalini
 
Sawa mtu hawezi kupendwa na watu wote, Yesu alikua mwana wa MUNGU na aliwatendea watu wema lakini watu hawakumpenda, sembuse Lissu...??!! Mnyaturu wa singidani, nadhani uko sawa na ni kawaida, Wala hapatakua na kukulazimisha umpende Lissu awe kiongozi.

Pia umesema Lissu anawahusudu sana wazungu, bad enough umesema Lissu anadhani Yuko sawa/pamoja na wazungu. Ni kweli hata Mimi Niko na mtazamo huo huo.

Wazungu Kwa kasi walio nayo ya kimaendeleo, hekima Yao, busara zao, so why wamekuwa blessed na MUNGU, Nimebaini African people ni wabinafsi mno ndo maana MUNGU hajatubless.(kiukweli kumuwazia vibaya mtu aliekuzidi vitu fulani, kisa tu amekuzidi, huo sio wivu wa kimaendeleo ila ni uchawi)
Kwa nini nasema Ivo, Yako mema mengi mzungu ameyafanya kwetu, bila kujali intention Yake katika wema aliotutendeaa. (Siwezi kumaliza Kwa kutaja). labda let say wewe ni mkulima wa ndizi, Wala hujui matumizi ya ndizi zaidi ya kula, akatokea mtu akiomba ile ndizi Kwa kubageini nae bei, ukaridhika na ukamuuzia, badaye akatengeneza biskut, akakuuzia wewe Kwa bei kubwa mno, na wewe ukanunua Kwa kuridhika. Je utakua na sababu gani kumchukia mtu uyo?.
Ningekua Mimi ningenyenyekea kwake anifundishe na mengine nisiyoyajua.
Kipi tumekifanya Kwa uwezo wetu bila mzungu au mchina?. Hata useme Bora tungebaki na uprimitive wa kiafrika, sawa ila tusingeendana na nyakati, Kuna kabila la wafugaji hapa tz(jina limeifadhiwa) wanaishi kinyama hawana utu, ni WA ajabu, wananyanyasa wanawake, na iyo ndo hekima ya kiafrika,. Je tungekua Ivo ingekuaje? Ni wazungu waliotuambukiza ustaarabu katika nyanja zote.
Mwingine utamsikia bora JPM alianzisha urafiki na china, je mchina ndo angekupa bure bila kukufaidi? Je uyo mchina ndo unaunasaba nae?,
Note:
AKILI YAKO NA MTIZAMO WAKO, ULIVOTOFAUTI NA WENGINE SIO NDO KIPIMO CHA UZALENDO WA MTU KATIKA TAIFA HILI, TAIFA HILI NI LAKO, NI LANGU, NI LA LISSU, NI LA WATU WOTE WALIOWATANZANIA, NA NAAMINI WOTE TUNALITAKIA MEMA TAIFA LETU, MITAZAMO INATOFAUTIANA KUTOKANA SABABU MBALIMBALI IKIWEMO UPEO WA KIFIKRA. itoshe
 
Mkuu, umenifikirisha sana'

Mazuri mengi uloyasema acha yakae moyoni kwangu! Barikiwa kwa huu ushawishi bora kabisa
 
Mijitu mingine mko Duniani kwa bahati mbaya kabisa kwako huogopi cccm ilivyoua hii Nchi ila unaogopa mtu ambae hana madaraka umBWA kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…