Unaongea usiyoyajua. Nina uhakika uelewa wako katika mambo ya kimataifa ni duni sana au haupo kabisa.
Gadaffi alikuwa anaua kila anayehoji utawala wake. Wakati wa utawala wa Gadafi, maisha ungeyaona mazuri sana kama ukikubali kuishi kama perty animal. Ukitaka kuonesha kuwa na wewe ni binadamu, sawa na Gadati, ndiyo mwisho wako wa kuishi Duniani.
Hata wakati wa mapambano ya kuondoa utawala wa Gadafi, wapiganaji wote walipewa maelekezo ya kumkamata Gadafi, wasimjeruhi wala kumwua ili ashtakiwe, lakini yule mpiganaji ambaye hakuwahi kuwa askari alipokutana uso kwa uso na Gadafi, licha ya Gadafi kunyosha mikono ikiwa ishara ya kukubali kukamatwa, alimiminiwa risasi, na askari wengine walipofika walikuta amekwishauawa. Yule askari alikamatwa, alishtakiwa na kuhukumiwa kifo. Lakini katika maelezo yake alisema kuwa alifahamu wazi kuwa hakustahili kumwua lakini yeye aliamua kumwua kwa sababu yeye Gadafi hakuwahi kumpeleka ndugu yake mahakamani, alikamatwa alipelekwa gerezani, na usiku mmoja, yeye pamoja na wenzake waliyltolewa gerezani, wakauawa na kuzikwa kwenye kaburi moja watu 250. Alisema alijua kuwa atauawa lakini angalao ameweza kumwua mtu aliyemwua ndugu yake.