Tundu Lissu kimataifa: Akutana na David Mcallister, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashauri ya Kigeni ya Bunge la Ulaya

Tundu Lissu kimataifa: Akutana na David Mcallister, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashauri ya Kigeni ya Bunge la Ulaya

..wananchi tunaweza kuikataa CCM lakini ikaendelea kubaki madarakani kwa msaada na kuungwa mkono na mabeberu.

..tunatakiwa tufanye kampeni za kuiondoa CCM ndani ya Tanzania na huko nje kwa ma-sponsor wao mabeberu.

kumbe unajua masponsor wa CCM ni mabeberu, nawewe unataka hao hao masponsor wa CCM wakusaidie kuitoa CCM...

La msingi ni watanzani wenyewe wakishaelimika vya kutosha wataitoa CCM tena kirahisi saaana...
 
Nisome vizuri, hata mimi naamini CCM haiwezi kutuletea maisha bora.... issue yangu iko kwenye kuitoa au kuilazimisha ilete hayo maisha bora ambayo ndio hitaji la kila mtu...

Kwenye kuitoa CCM ni watanzania wenyewe wanahitajika kuweka nguvu, kuelimishana ili watu wengi kama sio wote tukubaliane juu ya hili, kwa wingi wetu tukiikataa CCM haina pakutokea au kwa wingi wetu tukilazimisha jambo fulani litakuwa...
UtaoaJe elimu kwa wananchi , ikiwa hata makongamano ya kufanya wananchi wailewe vizuri katiba ni marufuku ?!
Na tunatii !! Ni serikali gani ya Tanganyika itaruhusu wananchi wake wapewe elimu ?!

Usiongee as if kuna mtu wa kutoa elimu hiyo na hawajibiki !!

Labda uasi
 
Ghadafi alikuwa shida na hao wazungi wakaja kuleta shida zaidi kwa maslahi yao kifupi walitumia mwanya wa ujinga wa Ghadafi kufanikisha maslahi yao...Ghadafi pia alikuwa kikwazo kwa maslahi yao lakini haikuwa kwa ajili ya raia wa Libya...

..Gaddafi alikuwa mbinafsi, na kiongozi aliyelewa madaraka na kupenda kutukuzwa.

..Kuna mambo ya kipumbavu alikuwa anayafanya na sidhani kama alikuwa ametumwa na Walibya.

..Kwa mfano, ni nani anaweza kusema kwamba Walibya walimtuma Gaddafi akatungue ndege ya abiria kule Lockerbie Scotland?
 
Usilolijua ni kama usiku wa giza...InshaAllah nakuombea kheri nawe usisite kuwaombea kheri wanaokaa kwa wazazi wao wapate nuru na kutoka maana waliowengi hawaipendi hiyo hali ni hali tu ya maisha...
Poa mkuu msalimie bi mkubwa hapo
 
USA aliwasaidia Mujahiddeen dhidi ya Urusi wakati huo adui yake akiwa ni Urusi, Mujahiddeen wakiwa vitani USA nyuma anapanga safu yake kuiongoza Afghanistan...Baada ya Mujahiddeen kushinda vita dhidi ya Mrusi akajikuta kwenye vita nyingine na USA kujikomboa mara ya pili.... USA akasurrender nakuwaachia nchi na yeye kujipanga upya, aliporudi mara ya pili akamtoa Mullah na Taleban akasimika utawala mwingine, kwa siri tena akanegotiate na Taleban kule Qatar akasepa kimyakimya na kuwaachia nchi Taleban.....its all about maslahi, tujifunze hapa..
 
Huwezi kuitoa CCM kwa kutegemea Wazungu ambao nao wanabenefit kwa CCM, kinachofuata watakutumia kuibana CCM kwa wao kupata maslahi zaidi... Nitajie nchi moja ambayo wazungu wameleta demokrasia na stabilization..

Wazungu walishindwa kuwasaidia weusi pale SA dhidi ya kaburu matokeo yake weusi wenyewe wakapambana kujikomboa huku wazungu wakipamban kimyakimya kusaidia kaburu..
Muda utaongea Mkuu.
 
Wazungu ni wakimbizi acha ufala. Huoni walivyo muassassinate gadafi kwa kuwa alikuwa anawanyanyasa sana wapinzani. Jpm ameua na kupiga risasi wapinzani na yeye wazungu wakatusaidia kumfyekelea mbali. Hivyo wazungu wanamsaada sana . Wazungu wasingekuwepo tungechinjana sana mana miafrika hatuna akili lazima tuwe regulated ili tuishi kwa kuheshimiana.
We ndo mjinga kabisa kwa fikra hizo za kitumwa, walimuua Ghadafi hilo limewasaidia nini Walibya, nchi inekuwa uwanja wa vita tangu wamuue. Interest yao ilikuwa ni rasimali mafuta na siyo maslahi ya wananchi wa Libya.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
..mbona wazungu hawachinjani kwa ajili ya demokrasia?

..Gaddafi alimpindua Mfalme halafu na yeye akajigeuza kuwa Mfalme.

..Gaddafi angeruhusu vyama vya siasa na kuandaa uchaguzi ulio huru Libya isingesambaratika.
Nani aliisamabaratisha Libya?
 
CDU kimeshindwa UCHAGUZI....

CDU kimeshindwa kumtoa KANSELA mpya......

CDU haina chake tena 🤣🤣🤣

Nini kukutana na kuongea naye?!!!

Awe anaishi naye kabisa huyo David Mc Alister 🤣

SIEMPRE JMT
 
kumbe unajua masponsor wa CCM ni mabeberu, nawewe unataka hao hao masponsor wa CCM wakusaidie kuitoa CCM...

La msingi ni watanzani wenyewe wakishaelimika vya kutosha wataitoa CCM tena kirahisi saaana...

..hapana.

..kinachotakiwa mabeberu waache kui-sponsor CCM ili ibakie ku-deal na wananchi.
 
Nani aliisamabaratisha Libya?

..walioisambaratisha Libya ni Gaddafi na mahasimu wake.

..Na chanzo cha yote ni upumbavu wa Gaddafi kutokuruhusu vyama vya siasa na kufanya uchaguzi wa kidemokrasia.

..Demokrasia inawafanya watu waache kufikiria kutumia silaha kutafuta madaraka ya kisiasa.
 
UtaoaJe elimu kwa wananchi , ikiwa hata makongamano ya kufanya wananchi wailewe vizuri katiba ni marufuku ?!
Na tunatii !! Ni serikali gani ya Tanganyika itaruhusu wananchi wake wapewe elimu ?!

Usiongee as if kuna mtu wa kutoa elimu hiyo na hawajibiki !!

Labda uasi

Hakuna urahisi mkuu kwenye kuikomboa jamii au watu....harakati hizi sio rahisi na ndio maana tunasisitiza umuhimu wa mapambano sio lelema ...na ndio hapo unapotaka msaada unakwenda sambamba na terms.....refer akina PK na M7 kuweza kuzitawala hizo nchi, msituni kumehusika, refer kutoka madarakani kwa Mobutu, refer kumtoa Alpha conde pale Guinea na akina Watara Ivory Coast....sio rahisi ndio maana wahuni wameweka hela kuendelea kuitawala Africa kwa style hii...
 
unawaoffer nini ili waache kuinsponsor CCM...?

..unawa-offer utawala utakaosimamia haki, utawala bora, na demokrasia, ambayo ndio masharti yaliyoelekezwa na wapiga kura/walipa kodi wao.
 
..unawa-offer utawala utakaosimamia haki, utawala bora, na demokrasia, ambayo ndio masharti yaliyoelekezwa na wapiga kura/walipa kodi wao.

Hivyo sio priority yao, priority yao ni rasimali zako ndio maana wako karibu na CCM na ukiwaoffer kupata zaidi ya hivyo basi kesho tu wanaitoa CCM na wakikuona hauna maslahi nao basi watakutumia kupata zaidi kwa CCM kwa kuitisha dhidi yako na wafuasi wako....kifupi kwa sasa mabeberu wanaitumia CDM kuitisha CCM na CCM inazidi kuwapa zaidi kutoka kwenye cake ya Taifa..
 
Ndio maana nakwambia wewe una akili yakitumwa!

Hivi Libya kabla ya wazungu wako kuketa democrasia watu walikuwa wana chinjana kama ilivyo sasa?

Kwa Kagame kuna watu wana chinjana?

Mkilishwa ujinga wa democrasia ya mzungu nasi mnajihisi mko mbinguni
Unaongea usiyoyajua. Nina uhakika uelewa wako katika mambo ya kimataifa ni duni sana au haupo kabisa.

Gadaffi alikuwa anaua kila anayehoji utawala wake. Wakati wa utawala wa Gadafi, maisha ungeyaona mazuri sana kama ukikubali kuishi kama perty animal. Ukitaka kuonesha kuwa na wewe ni binadamu, sawa na Gadati, ndiyo mwisho wako wa kuishi Duniani.

Hata wakati wa mapambano ya kuondoa utawala wa Gadafi, wapiganaji wote walipewa maelekezo ya kumkamata Gadafi, wasimjeruhi wala kumwua ili ashtakiwe, lakini yule mpiganaji ambaye hakuwahi kuwa askari alipokutana uso kwa uso na Gadafi, licha ya Gadafi kunyosha mikono ikiwa ishara ya kukubali kukamatwa, alimiminiwa risasi, na askari wengine walipofika walikuta amekwishauawa. Yule askari alikamatwa, alishtakiwa na kuhukumiwa kifo. Lakini katika maelezo yake alisema kuwa alifahamu wazi kuwa hakustahili kumwua lakini yeye aliamua kumwua kwa sababu yeye Gadafi hakuwahi kumpeleka ndugu yake mahakamani, alikamatwa alipelekwa gerezani, na usiku mmoja, yeye pamoja na wenzake waliyltolewa gerezani, wakauawa na kuzikwa kwenye kaburi moja watu 250. Alisema alijua kuwa atauawa lakini angalao ameweza kumwua mtu aliyemwua ndugu yake.
 
Kwa hiyo sasa hivi watu wako huru!

Democrasia imetawala maisha ni mazuri sana baada ya mzungu kuleta demcrasia?
 
Huwezi kuitoa CCM kwa kutegemea Wazungu ambao nao wanabenefit kwa CCM, kinachofuata watakutumia kuibana CCM kwa wao kupata maslahi zaidi... Nitajie nchi moja ambayo wazungu wameleta demokrasia na stabilization..

Wazungu walishindwa kuwasaidia weusi pale SA dhidi ya kaburu matokeo yake weusi wenyewe wakapambana kujikomboa huku wazungu wakipamban kimyakimya kusaidia kaburu..
Bila Warusi na Cuba Azania ingekuwa bado inatawaliwa na Makaburu wachache.
Tundu Lissu ni Jemadari.
 
..walioisambaratisha Libya ni Gaddafi na mahasimu wake.

..Na chanzo cha yote ni upumbavu wa Gaddafi kutokuruhusu vyama vya siasa na kufanya uchaguzi wa kidemokrasia.

..Demokrasia inawafanya watu waache kufikiria kutumia silaha kutafuta madaraka ya kisiasa.
Mabeberu walipopeleka makombora pale na kulipua hovyo ili kumua gadafi kuna utulivu wowote umerejea sasa?
 
Back
Top Bottom