Tundu Lissu: Kufa kwa Magufuli ni 'Poetic Justice'

Tundu Lissu: Kufa kwa Magufuli ni 'Poetic Justice'

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825
Kikomo cha kukosa ustaarabu ni kushangilia kifo cha kiumbe mwenzako hasa binadamu hata kama amekukosea kiasi gani. Alipofariki JPM makamu mwenyekiti taifa wa CHADEMA Mh. Tundu Lissu alikiita kifo cha JPM a poetic justice (a fitting or deserved retribution for one's actions).

Tunaamini huu pia ndio msimamo wa CHADEMA kwani hawajawahi kujitenga nao. Kwa vile sasa tuko kwenye maridhiano ni bora CHADEMA mliweke hili wazi na mna fursa hiyo 21.01.2023 kwenye mkutano wenu wa hadhara Mwanza na kanda ya ziwa- kanda ya kwao na JPM.
162033367_1330017047375929_831188534219967358_n.jpg
 
Lissu anayo haki ya kusema hivyo Kwani yeye anaamini kuwa chanzo cha yeye kutaka kuuawa ni Magufuli, ikumbukwe binadamu amezaliwa na roho ya kisasi hivyo kifo cha JPM kwake Lissu ni faraja na anguko la adui zetu ni faraja kwetu.

Hata Mimi kuna baba ndogo tunaendesha naye kesi anang'ang'ania nyumba ya baba yetu, kwangu Mimi huyu ni adui, nikisikia Leo hii kafa, wallah lazima nichinje mbuzi na kukesha baa nikikunywa bia, kwangu Mimi huyu baba ndogo ni adui yangu kifo chake furaha kwangu.

Maisha ndio yalivyo hapa dunia, mwacheni aseme ya moyoni
 
Mwaka 2016 mpaka 2020 Tanzania iligubikwa na makelele ya Tundu Lisu aloyejiona yeye tu ndiyo mwenye haki ya kumshauri rais wa nchi wa wakati huo na ni lazima ushauri wake ufuatwe!

Hata hivyo hayati Magufuli alisimama imara na kupuuza makelele yote ya wakala wa mabeberu Tundu Lisu.

Kama hayati raisi Magufuli asingekuwa imara na akasikiliza makelele ya Lisu, haya hapa yangetokea Tanzania.

1. Tanzania tusingekuwa na bwawa la kufua umeme ambalo ni moja ya mabwawa makubwa barani Afrika. Urefu wa bwawa la Nyerere ni km100 yani sawa na urefu wa kutoka Dar mpaka Chalinze.

Tundu Lisu kwa kutumiwa na mbabeberu kwa ahadi ya kumlisha yeye na familia yake pamoja na kumpa hifadhi Ubelgiji alipinga sana ujenzi wa bwawa hili kwa kisingizio kwamba litasababisha uharibifu wa mazingira na mvua hazitanyesha tena Tanzania!. Leo mwaka 2023 bwawa linajazwa maji na Tanzania imegubikwa na mafuriko kila sehemu kwani mvua zinanyesha sana kinyume na utabiri wa Tundu Lisu.

2. Tanzania isingekuwa na ujenzi wa SGR.
Tundu Lisu alipinga sana ujenzi wa reli hii ya umeme na yenye kasi zaidi Afrika yote.

3. Serikali isingehamia Dodoma.
Tundu Lisu na Mbowe walipinga sana serikali kuhamia Dodoma wakisema huko ni kutesa watumishi na kwamba serikali ibaki tu Dares salaam kwa ndoto za mwl Nyerere zimepotwa na wakati. Hayati Magufuli aliziba masikio na leo serikali yote ipo Dodoma.

4. Kampuni ya madini ya Acacia ingekuwepo.
Licha ya kwamba Lisu amesoma kwa kodi za watanzania lakini aligeuka kuwa mwanasheria wa Acacia na akasema ataisaidia kutushitaki MIGA, kama tukiendelea kuwadai hela za wizi wa makinikia. Hayati Magufuli aliendelea mbele hadi kampuni ya Acacia ikafutwa na kuzaliwa kampuni mpya ya Twiga ambayo watanzania wapo kwenye management na Tanzania yakafunguliwa masoko ya madini kila sehemu, na watanzania wakanufaika na madini yao.

5. Kenya na India zingeendelea kuongoza kwenye uuzaji wa madini ya Tanzanite .
Kutokana na ukweli madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania tu. Hayati Magufuli alichukua hatua kali sana za kudhibiti madini ya Tanzanite ikiwemo kujenga ukuta wa kuzunguka mgodi huo, hatua hizo zilipingwa mno na Lissu na akaita ni udikteta mkubwa kufanya hivyo
 
Kikomo cha kukosa ustaarabu ni kushangilia kifo cha kiumbe mwenzako hasa binadamu hata kama amekukosea kiasi gani. Alipofariki JPM makamu mwenyekiti taifa wa CHADEMA Mh. Tundu Lissu alikiita kifo cha JPM a poetic justice (a fitting or deserved retribution for one's actions).

Tunaamini huu pia ndio msimamo wa CHADEMA kwani hawajawahi kujitenga nao. Kwa vile sasa tuko kwenye maridhiano ni bora CHADEMA mliweke hili wazi na mna fursa hiyo 21.01.2023 kwenye mkutano wenu wa hadhara Mwanza na kanda ya ziwa- kanda ya kwao na JPM.
162033367_1330017047375929_831188534219967358_n.jpg
Wapi kuna kushangilia kwenye post yako.. au huelewi maana ya kushangilia? Kutoa maoni si kushangilia. Is narrating the fact/truth.

Ukiiba ukakamatwa ukaadhibiwa kisha nikasema unastahili adhabu, nakuwa nimeshangilia au hujui maana ya poetic justice?
 
wapi kuna kushangilia kwenye post yako.. au huelewi maana kushangilia? Kutoa maoni si kushangilia. Is narrating the fact/truth
Unatoaje maoni kwenye kifo?! Ukitaka kujua hebu fikiria kila kwenye maziko ya waislam hutolewa tangazo la nani ana mdai marehemu- ulishaona watu wanijitokeza? Unadhani ni ujinga au uoga?
 
Unatoaje maoni kwenye kifo?! Ukitaka kujua hebu fikiria kila kwenye maziko ya waislam hutolewa tangazo la nani ana mdai marehemu- ulishaona watu wanijitokeza? Unadhani ni ujinga au uoga?
position yourself katika mazingira ya lisu au kaka/mdogo wa watu waliopotezwa enzi za jamaa kama ben saa nane na wengine wengi, achilia mbali walioteswa na jpm as mfariji mkuu alipotezea tu.

Kwa Lissu hata ibada za kumuombea polisi waliwafuata watu katika nyumba za ibada wasimuombee lisu apone.

Kimsingi utawala wa jpm ulitaka Lisu afe tu.....then try to adjust your lame argument
 
Does that justify his celebration upon the death of JPM?
 
Mwaka 2016 mpaka 2020 Tanzania iligubikwa na makelele ya Tundu Lisu aloyejiona yeye tu ndiyo mwenye haki ya kumshauri rais wa nchi wa wakati huo na ni lazima ushauri wake ufuatwe!
Hata hivyo hayati Magufuli alisimama imara na kupuuza makelele yote ya wakala wa mabeberu Tundu Lisu.

Kama hayati raisi Magufuli asingekuwa imara na akasikiliza makelele ya Lisu, haya hapa yangetokea Tanzania.

1. Tanzania tusingekuwa na bwawa la kufua umeme ambalo ni moja ya mabwawa makubwa barani Afrika. Urefu wa bwawa la Nyerere ni km100 yani sawa na urefu wa kutoka Dar mpaka Chalinze.
Tundu Lisu kwa kutumiwa na mbabeberu kwa ahadi ya kumlisha yeye na familia yake pamoja na kumpa hifadhi Ubelgiji alipinga sana ujenzi wa bwawa hili kwa kisingizio kwamba litasababisha uharibifu wa mazingira na mvua hazitanyesha tena Tanzania!. Leo mwaka 2023 bwawa linajazwa maji na Tanzania imegubikwa na mafuriko kila sehemu kwani mvua zinanyesha sana kinyume na utabiri wa Tundu Lisu.

2. Tanzania isingekuwa na ujenzi wa SGR .
Tundu Lisu alipinga sana ujenzi wa reli hii ya umeme na yenye kasi zaidi Afrika yote.

3. Serikali isingehamia Dodoma.
Tundu Lisu na Mbowe walipinga sana serikali kuhamia Dodoma wakisema huko ni kutesa watumishi na kwamba serikali ibaki tu Dares salaam kwa ndoto za mwl Nyerere zimepotwa na wakati. Hayati Magufuli aliziba masikio na leo serikali yote ipo Dodoma.

4. Kampuni ya madini ya Acacia ingekuwepo.
Licha ya kwamba Lisu amesoma kwa kodi za watanzania lakini aligeuka kuwa mwanasheria wa Acacia na akasema ataisaidia kutushitaki MIGA ,kama tukiendelea kuwadai hela za wizi wa makinikia. Hayati Magufuli aliendelea mbele hadi kampuni ya Acacia ikafutwa na kuzaliwa kampuni mpya ya Twiga ambayo watanzania wapo kwenye management na Tanzania yakafunguliwa masoko ya madini kila sehemu, na watanzania wakanufaika na madini yao.

5. Kenya na India zingeendelea kuongoza kwenye uuzaji wa madini ya Tanzanite .
Kutokana na ukweli madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania tu. Hayati Magufuli alichukua hatua kali sana za kudhibiti madini ya Tanzanite ikiwemo kujenga ukuta wa kuzunguka mgodi huo, hatua hizo zilipingwa mno na Lisu na akaita ni udikteta mkubwa kufanya hivyo
Lissu ni much know, ogopa sana watu wanaopenda kujikweza!
 
Back
Top Bottom