Ukiwa na serikali dhaifu na ya hovyo, tena isiyojali usalama na uhai wa raia wake hayo yote yanaweza kutokea.
Jiulize na nani alipaswa kufanya uchunguzi wa matukio yote?
Je, yalifanyika? Majibu yakoje?
Kama serikali hiyo hiyo ilizuia hata wale waliotaka kufanya maombi kwa waliokumbwa na majereha unaisemeaje? Huoni kuwa ni dhalimu dhidi ya raia wake!
Tumia kichwa chako kufikiri sio kufugia chawa na wewe kuwa chawa.
Penda haki, na itimize kwa kufuata mikondo ya kutoa haki. Sio kuchukua sheria mkononi na kujeruhi ama kutoa uhai kwa wale wasiungana nanyi.
Naona umezaliwa kwa ajili ya kufanywa jalala au gunia la kutupiwa uongo wa viongozi wako wa chama.
Ni aibu kijana kama wewe kukubali kila unachoambiwa na hawa wanasiasa uchwara.
Mwaka 2008 hadi 2014 viongozi wako walikwambia kuwa Lowasa ni fisadi namb 1 nchini, hafai hata kupewa ticket ya kugombea udiwani au uenyekiti wa serikali za mitaa ukakubali na kukenua meno.
Mwaka 2015 baada ya Lowasa kuwahonga vijisenti vya kuendea Dubai kula bata viongozi wako hao hao wa upinzani wakakwambia kuwa Lowasa sio fisadi na wala hakuwahi kuwa fisadi bali ni mtu mwenye maono na mzalendo wa kweli wa Tanzania, kwahiyo mfagilie barabara na umchague awe raisi wako, wewe tena ukakenua mijino na kuamka asubuhi mapema siku ya uchaguzi kwenda kumpigia kura Lowasa.
Sasa kwa aina hii ya kichwa chako viongozi wako watakosaje kukitumia kichwa chako kama jalala la kutupia uongo wao?
Mimi sio wa aina hiyo, kwamba unidanganye leo afu kesho unidanganye tena! Never sikubaliani na ujinga huo kamwe.
Kuhusu swala la usalama wa raia hiyo kauli yako haina msingi. Kama raia wangekuwa hawana usalama wewe leo usingeshinda na msuli wako huku unaandika upupu namna hii bila mtu yoyote kukubughuzi.
Unafikiri ni raia wangapi wanakufa kwa kupigwa risasi Marekani aidha na polisi au raia wa kawaida, hata jana kuna watu wamepigwa risasi huko California, sasa unataka kusema kuwa serikali ya Marekani ni dhaifu?
Je kati ya Marekani na Tanzania ni wapi ambapo kuna ongoza kwa mauaji?