Tundu Lissu: Kufuta kesi ya Mbowe sio kuingilia Uhuru wa Mahakama

Huu ndiyo ukweli kwenye hoja mbili! Leo Mahakama inatoa uamuzi kama Mbowe ana kesi ya kujibu au lah! Kipi hasa hawataki kusubr na kesi yenyewe imepelekwa haraka sana ili apate haki yake? Kwanini wanataka afutiwe kesi eti haina tija kwa Tanzania wala kwa CCM au Chadema? Wanaforce Rais aingilie mahakama alafu wakikaa tena wanakuja na gear yakwamba Rais haeshimu Katiba na Sheria za Nchi
 
Hao wanawake 19 sio wanachama wa chama cha Chadema kwani walishafukuzwa na kamati kuu unless wawe reinstated na Baraza Kuu kufuatia rufaa waliokata.
 
Mkuu mbona hapa wote wanapigania kitu kimoja, mbowe awe huru
... uko sahihi; hoja ya msingi huo uhuru unapatikanaje? Unyang'anywe uhuru wako kidhalimu halafu uwapigie magoti kuomba urudishiwe uhuru wako ambao ni haki yako? Dah; you better die than doing that.
 
Akifanya Lisu ana akili, akifanya Zitto ccm B. Acheni unafiki Zitto amewatangulia na hammuwezi.
Huyo Zitto mnayemtetea kiasi hicho ni nani katika nchi hii?Kati ya Zitto na Lissu nani kiongozi wa CDM?Je,baada ya Zitto kudaiwa kumwombea msamaha Mh.Mbowe,nini kilibadilika kuhusu kesi ya Mbowe?
Utetezi wa ccm kuhusu CDM kumpinga Zitto msingi wake nini?
 
Naam wanajaribu kumwingiza Rais ktk mtego ili mwisho wa siku aonekane kama kinara wa kuvunja katiba na sheria.

Kwa mtizamo wangu nadhani wasubiri tu mchakato wa Mahakamani kwa kuwa kesi ipo mahakamani na mahakama imejitahidi kwa kiasi kikubwa kusikiliza kesi hii haraka haraka
 
Ulaya hamna maisha ya ujanjaujanja na hivi passport tiss washapita nayo
 
Uko sahihi, ila kosa dogo tu ni pale unasema 'amemuagiza'. Sahihi ni 'amemuomba' au 'amemtaka' afute mashtaka hayo ya kubambikia.
We jamaa ni mental staff, hivi umemwelewa lissu?
elewa Lissu hajamuombea Mbowe msamaha bali amemuagiza rais afute mashtaka yasiyo na tija yaan ya mchongo tofauti na kibaraka wenu zitto
 
Wanasiasa wenye akili kama za lissu wamekuwa adimu sana siku hizi, wengi ni wachumia tumbo wasioweza kujenga hoja
ila Zitto alipoomba hilo akaonekana kiazi !

Watanzania tuna safari ndefu sana
 
Maccm mengi hayana akili ya kujua tofauti ya haya
 
BUNGE HALINA TAARIFA
Sio kweli, Magufuli ndio alikuwa engineer wa mradi huu ili awatumie hao wanawake kuhadaa wafadhili kwamba kuna wapinzani kwenye kamati mbalimbali za bunge ili iwe kigezo cha kupata Budget Support toka kwa hao wafadhili japo sidhani kama huu mpango umepata mafanikio yaliyokusudiwa.
 
Mahakama ikikuhukumu miaka 10 na ukakata rufaa,je kipindi unasubiri rufaa ianze kusikilizwa utakuwa nje kama raia huru au utaendelea kutumikia hukumu yako ya miaka 10 mpaka hapo rufaa yako itakapohitimishwa?Same na wale wabunge 19 maadamu wamefukuzwa uanachama hawapaswi kuwepo bungeni mpaka pale rufaa zao zitakapowarejeshea uanachama na chama kuridhia wakawe wawakilishi wake.
Kuhusu suala la Mbowe kuiachia na kuamini mahakama itafanya Haki,Unataka kutuambia mahakama hizi hazijawahi kuhukumu watu kwa kuonea?Rejea hukumu ya Sugu na Mwasonga mpaka mahakama ya rufaa iliposema walionewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…