Tundu Lissu: Kufuta kesi ya Mbowe sio kuingilia Uhuru wa Mahakama


Hata kama kitendo cha Rais kuamua kufuta kesi ya Mbowe au mtuhumiwa mwingine yeyote sio kuingilia uhuru wa mahakama, obviously, ni kinyume cha misingi ya Rule of Law. Ni kupoka madaraka yasiyokuwa ya kwake!

Mtu pekee mwenye mamlaka ya kufanya uamuzi wa kumshitaki au kutomshitaki mtuhumiwa yeyote ni DPP, na kikatiba, anapaswa kufanya hivyo bila kuingiliwa na mtu yeyote yule.

Tukishaanza kuweka exceptions uchwara za mazingira ambayo Rais anaweza kutoa maelekezo (straight au katika form ya ushauri) kwa DPP kufuta kesi fulani, basi lazima pia tukubali na tutarajie kwamba yatakuwepo mazingira ambayo DPP atafanya uamuzi wa kuwashitaki watuhumiwa fulani kwa maelekezo ya Rais.

Nipo tayari kubaki pekee yangu nikisema hii sio Rule of Law!
 
Serikali kufuata kesi siyo kuingilia mamlaka ya Mahakama. Hii imefanyika mara nyingi tu kila wakati serikali inapoona haina haja ya kuendelea na kesi.

Hata Maza majuzi kasema wamemfutia Lissu kesi zake zote.
 
Lissu hana mamlaka ya kumwambia rais nini cha kufanya kwahiyo tafsiri sahihi hapo ni kumuomba rais amfutie kesi Mbowe.
Jaribu kuwa mwelewa kidogo. Sijasema nani yuko sahihi kati ya Zito na Lissu. Nimebainisha tofauti yao kwa yale waliyozungumza/waliyoshauri.
 
Hakika wote tungependa taratibu zifuatwe ikiwa ni pamoja na kuona maamuzi ya mahakama inachukua nafasi na hata ikibidi rufaa ikatwe baadaye.
Lakini kwa mifumo ya tawala kandamizi za kidekteta kama hapa Tanzania; ni sawa na kusema the right delayed is equal to right denied.
Haikutegemewa kuona kwa kiongozi aliyepata kuwa Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni leo hii awe anasota gerezani kwa kesi za kubambika.
Hakuna asiyejua utawala wa Hayati JPM ulivyokuwa mbaya kiutawala, wizi wa kura, kubambikia watu kesi za michongo, watu kupotea na kuuawa bila kujulikana asili na sababu za mauaji na vikosi vya watu wasiojulikana.
Hivyo leo unapoona kiongozi anashitakiwa kwa makosa yaliyojengwa kipindi cha vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa 2020, mtu huwezi kukosa kuamini kwamba hizi zilikuwa ni moja ya kesi kisiasa tena zenye nia kupooza upinzani nchini.
Sasa hata serikali ya sasa itaonekana ya kikandamizaji,.kwa sababu misingi ya kesi imejengwa tokea kwenye vuguvugu la uchaguzi Mkuu uliopita.
Na bahati mbaya kuwekwa ndani kwa Mh FAM ni katika za:
a) Kuruhusu utawala wa sasa kujitanua bila ya kuwepo na mpinzani makini;
b) Kumdhoofisha Mh FAM katika harakati zake nyingi za kisiasa kama mwenyekiti wa CHADEMA, alizozipata kuzifanya kipindi hiki.
Kwa ujumla, inasikitisha sana hadi katika maendeleo jamii iliyopiga, bado inadhaniwa kwanza ili mtu ajitanue sawasawa ni kumfunga mpinzani wake korokoroni.
 
Naungana na comment yako, akiomba msamaha maana yake anakiri kosa indirect, tuache hili jambo limalizike mahakamani ili tujue mbivu na mbichi
 
We jamaa ni mental staff, hivi umemwelewa lissu?
elewa Lissu hajamuombea Mbowe msamaha bali amemuagiza rais afute mashtaka yasiyo na tija yaan ya mchongo tofauti na kibaraka wenu zitto
Wewe ndo bure kabisa, yaani tundu amuagize mh rais afute kesi ya Mbowe? Una akili kweli?
Nyumbu hovyo kabisa.
 
Lissu hajaomba mbowe asamehewe acha uzito wa kufikiri yeye ametaka kesi ifutwe. Kesi kufutwa na kusameheana ni vitu viwili tofauti. Kusamehewa ni mpaka ahukumiwe
Sasa wale pingapinga FC mliompinga zitto kuomba kwa rais gaidi amsamehewe njooni mpige makofi kwa tundu tafadhali.
 

..Halima na wenzake wamekata rufaa kufukuzwa uanachama.

..maana yake ni.kwamba sasa hivi sio wanachama wa Chadema.

..Na kama hawana chama hawapaswi kuwa bungeni.
 
Jaribu kuwa mwelewa kidogo. Sijasema nani yuko sahihi kati ya Zito na Lissu. Nimebainisha tofauti yao kwa yale waliyozungumza/waliyoshauri.
Hata mimi nimeeleza tu kilicho sahihi kwamba alichokifanya Lissu ni ombi tu hakina tafsiri nyengine.
 
Bunge halina taarifa

..Bunge walishapewa taarifa kuwa Halima na wenzake wamefukuzwa.

..Spika Ndugai alikataa kuchukua hatua stahiki baada ya kupokea taarifa toka kwa KM wa Chadema kwamba Halima na wenzake wamefukuzwa ktk chama hicho.
 
Taifa linahitaji kufanyiwa maombi ili Mungu aliponye maana limezungukwa na jitu ya Ovyo sana eg Lissu
 
Hao wanawake 19 sio wanachama wa chama cha Chadema kwani walishafukuzwa na kamati kuu unless wawe reinstated na Baraza Kuu kufuatia rufaa waliokata.
Chama kinachojinasibu kupigania haki za watu, leo mwaka wa pili hakijasikiliza rufaa za watuhumiwa 19. Kama si udikteta ni nini?
 
Ipo haja ya wote waliobumba kesi hii ya uongo wachukuliwe hatua. Wakiwemo siro, kingai, mahita jumanne gudlack majaji na mahakimu wote waliojiingizia pesa haramu kama posho mbalimbali za kushiriki kesi ya uongo na kuitia hasara kodi yetu.
Hio gharama ya kuendesha kesi si ingenunua hata madawati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…