Tetesi: Tundu Lissu kujiunga ACT Wazalendo, Abdul Nondo naye kuula!

Status
Not open for further replies.
Tetesi zina mambo mawili kuwa za uongo au ukweli, ila nachokumbuka ni kuwa walikuwa na mazungumzo ya mipango ya muungano wa vyama na kutoa tofauti zao ila la kuhamia chama ACT hilo mmesema nyinyi ngoja tuwe na subira kuona maamuzi ya baadae
 
Ukiwa kwenye siku zako huwa unapata tabu sana dawa yake ubebe mimba tu.
 
Huyo mbona sigara nyota, wewe tu.
 

Mkuu hamna la ajabu hapo kisiasa maana China ndio imewajengea ccm ukumbi wa mikutano hapo Dodoma. Hiyo dola ilikuwa likizo haikujali maslahi ya taifa kwa chama cha siasa kujengewa ukumbi wa mikutano? Au hilo jengo ndio ilikuwa fumba macho ili wachina wapate miradi mbalimbali ya serikali na kuishia kujenga substandard projects?
 

Hakuna la ajabu hapo maana hata Slaa yuko ccm na aliishia kwenda huko na mkewe. Hata Lissu anaweza kwenda popote na atapata support yetu iwapo tu ataongea lugha moja na sisi.
 

Ukumbi wa Ccm Dodoma haukujengwa na Serikal ya China

Umejengwa na Chama Rafiki Chama tawala cha China
 
Hujui siasa wala huwajui wanasiasa. Kwani maalim seif ambaye aliungana na chadema na akaungwa mkono urais kupitia ukawa mbona alihamia ACT kabla ya chadema? Kwani chadema walimfanya nini?

Maalim Seif kuhamia ACT ni bora kwa kudumisha upinzani kwa kukipa nguvu chama kingine cha upinzani.

CHADEMA walkwisha kuwa na wafuasi kiasi visiwani na ingeleta mvutano kati ya CDM wahamiaji na CDM asili. ACT ni kama mwari visiwani kwa hiyo wahamiaji hawakujiona wageni na kusimangwa.
 
Ninachokiona mimi ni Zitto kuwa mgombea mwenza wa Lissu come 2020

Hawezi kuwa mgombea mwenza wake maana wote wanatokea bara. Mgombea mwenza anapaswa kutoka Znz. Vyovyote iwavyo, Zito ndio anafaa zaidi kugombea urais kwani anamudu uchumi, mambo ya kijamii na demokrasia na ana misimamo ya wastani, shida yake haaminiki. Lisu pia anafaa lakini amejikita kwenye sheria zaidi kuliko uchumi na ana siasa za misimamo mikali. Lissu akiwa rais tunaweza kukutana na tatizo lililopo sasa hivi kuwa na rais anayesimamia jambo moja tu na kusahau maeneo mengine.
 
Ninachokiona mimi ni Zitto kuwa mgombea mwenza wa Lissu come 2020
Inaonesha huna kabisa habari ya kinachoendelea kwenye siasa. Zitto na Tundu wanatoka bara MGOMBEA MWENZA LAZIMA ATOKE UPANDE WA PILI WA MUUNGANO na kuna sheria kwamba ukihamia chama kipya kaa miaka miwli ndo ugombee cheo cha kisiasa.
 
Rubbish, waziri mzima unaandika "mavi" kiwango hiki. Acha utoto wewe ni mtu "mkubwa", tunategemea hekima toka kwako siyo utumbo wa hivi!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…