Uchaguzi 2020 Tundu Lissu kukosa pesa ya kampeni

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu kukosa pesa ya kampeni

Hakuna mkamilifu. Double standard hata wewe unayo huko uliko. Sema kwa vile hatuioni na iwapo wewe huwezi kujitambua basi bwabwaja ya mwenzako tu.

JPM kama binadamu anaweza akaamua kuacha kumuchukulia mtu hatua kulinga na mahitaji ya wakati huo.

Anaangalia mazingira au sheria? Kwani anaoongoza kwa utashi wake au katiba na sheria?
 
Wananchi tutamchangia Lissu tena ndiyo itatupa marali zaidi wa kuzilinda kura.

By the way, kulikoni CCM mbona nyie hili la Lissu kutokua na pesa linawasumbua zaidi kuliko wapinzani wenyewe? Mnaogopa nini hasa?
 
Rebeka 1,

Lissu akitoa account namba ya bank week moja tu mzigo unajaa hadi unamwagika tunachanga wenyewe pesa amini usiamini pesa nyingi za kampain zitachangwa na wana CCM, wengi wanamkubali sana Lissu sema wanaogopa kubambikwa kesi ndio maana wanajificha
 
Anaangalia mazingira au sheria? Kwani anaoongoza kwa utashi wake au katiba na sheria?
Wewe.. Unazania kila kitu kinasheria? Kisa mmepata mgombea mwanasheria unazania kila kitu kina sheria?
Ndio maana mnatutukana afu mnatuuliza iwapo sheria inakataza.
Mengine ni utashi wa kiongozi tu.
 
Tutachanga watupe bujeti Hilo liziwaumize
 
Hii ni takataka nyingine imeletwa tena humu.

Obama hakua na kitu lkn alichangiwa na watu hadi michango yake ikavunja rekodi ya uchangiaji kwa wagombea urais ktk historia ya Marekani.

Hivyo hata kwa Lissu hakutakuwa na shida tutakuwa tayari kuvunja benki tumchangie.

Nyie mnategemea zile 1.5 Tr mlizotupora halafu mnarudi tena kutusanifu eti kuomba kura kwa walewale mliowapora. Bugus kabisa nyie.
 
Habari haina ushahidi wowote huku Tundu Lissu mwenyewe akionekana kuendelea na shughuli zake.

Kama ni kweli Lissu hana pesa ya kampeni "tupo tutamchangia" na kampeni zitafanyika. Kawaambie waliokutuma.
Loooh hii ni hatari sana! Hata mwezi bado mambo yanakuwa hivi na hao wafadhili waliowapa hiyo ruzuku watataka mahesabu sahihi ili watoe pesa nyingine na Accounting Officer hatoi ushirikiano! Mtafanyaje itakapokuja ile marathon ya siku sitini za kampeni!?
 
Tatizo mnakuwa mnaongea tu kwani hujui pesa ya kampeni hutolewa kwa ruzuku ya serikali
 
Kwani ? Magu pesa za campaign atazipata wapi?
Tutachanga sisi wanachama na raia wenye mapenzi mema na Lissu

Wewe wala usiwe na pressure,it is on us not you!
You are right it is on us and not on them. Mh. Lissu na sisi wataka mabadiliko tuhakikishe anakamilisha mchakato wa kukusanya wathamini awakilishe orodha NEC aende zake Singida akakae mpaka siku ya Uchaguzi akapige kura yake angoje matokeo maana chema chajiuza kibovu chajitembeza. Sote pamoja na wao tunajua kila jitihada zitafanywa kumuengua asigombee, watambambikizia kesi, wasiojulikana watajaribu kukamilisha kazi, ikishindikana wataiba kura kama kawaidà yao na kumtangaza mshindani kuwa mshindi wa kishindo na yeye kushindwa kwa kupata kura moja yake.

Miaka 60 ya Uhuru ya utawala wa Chama hichohicho kimoja na wananchi ni haohao wamepitia Utawala huo na kushuhudia hizo mbinu chafu kweli Watanzania wenye akili zao hata waliomthamini hawatampigia kura mgombea anayefaa kwasababu hajafanya kampeini? Bado zaidi ya miezi miwili hadi siku ya Uchaguzi na mimi nimekwisha amua kura yangu nitampa Mh. Lissu kwa sababu kwangu sioni mbadala na hakuna wakunibadilisha. Swali kwenu wenzangu: Je ile kura moja ni yangu au yake na mimi nifanye nini kuhakikishiwa kura hiyo moja ni yangu?
 
Pole sana Lissu. Hukujua tu, kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya mafanikio ya kisiasa na ukwasi. Ilipaswa upime kabla kama wewe hauna pesa basi taasisi inayokudhamini iwe na pesa ila kama nyote hamna pesa basi tukushukuru tu kwa kushiriki na kuchangamsha genge. Achana na haya mambo jipange next time
Pesa ipo acha kukariri vya kudanganywa na watengeneza propaganda wanaoshinda gheto kwa cyprian Musiba
 
Back
Top Bottom