Pre GE2025 Tundu Lissu: Kuna Rushwa inatuvuruga ndani ya CHADEMA

Pre GE2025 Tundu Lissu: Kuna Rushwa inatuvuruga ndani ya CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama amevuruga na wahusika wamerugika inaonesha Chadema ni chama dhaifu

..Chadema ni dhaifu.

..lakini ndio chama kikubwa kuliko vyote vya upinzani.

..Ccm wanapokea ruzuku ya billion 13 kila mwezi.

..sasa utawapambanisha vipi na vyama vingine, ambavyo ruzuku yao haifiki hata milioni 10?
 
Wewe jamaa unanichekesha unamlindaje mtu anayekubali kupokea rushwa kwa hiyali yake

..haiwezekani kuwazuia au kuwaadhibu wanaotoa rushwa?

..kwanini siku zote wanaohongwa ni wapinzani tu?

..kwanini haitokei kwamba Ccm nao mara mojamoja wakahongwa na wapinzani?

..au kwanini miaka yote wanaoenguliwa ni wagombea wa upinzani, hakuna mgombea wa Ccm ameenguliwa na Tume toka mfumo wa vyama vingi uanzishwe?
 
..Chadema ni dhaifu.

..lakini ndio chama kikubwa kuliko vyote vya upinzani.

..Ccm wanapokea ruzuku ya billion 13 kila mwezi.

..sasa utawapambanisha vipi na vyama vingine, ambavyo ruzuku yao haifiki hata milioni 10?
Kwa hii comment yako kama nchi tunasafari ndefu sana, hivi mkuu huu ushabiki wenu wa vyama unawanufaishaje
 
..haiwezekani kuwazuia au kuwaadhibu wanaotoa rushwa?

..kwanini siku zote wanaohongwa ni wapinzani tu?

..kwanini haitokei kwamba Ccm nao mara mojamoja wakahongwa na wapinzani?

..au kwanini miaka yote wanaoenguliwa ni wagombea wa upinzani, hakuna mgombea wa Ccm ameenguliwa na Tume toka mfumo wa vyama vingi uanzishwe?
Hapo nilichoona kwako haupo kutengeneza hoja kwa maslahi ya Taifa zaidi ni kutetea upande wako wa kushabiki chama but nataka nikwambie tu hakuna mwanasiasa ambaye atakuletea mabadiliko kwenye maisha yako unapoteza muda wako bure wakati viongozi wako wanakula maisha, aina ya watu kama wewe mnafanywa kama ngazi ya wanasiasa kufikia malengo yao.
 
..mimi ninachotaka ni demokrasia yenye usawa kwa vyama vyote.

..Na wanaotuzuia tusifike kwenye demokrasia hiyo ni Ccm.

..au labda wewe unataka ibaki Ccm peke yake halafu wananchi wakabiliane nayo bila utaratibu?

..kwa maana nyingine unataka machafuko nchini.

..ujinga wa mwanasiasa unaweza kuleta mabadiliko hasi, mabaya sana, ktk maisha yetu.

..Kwa msingi huo, usiwachukulie poa, au tusiwaendekeze, wanasiasa wanaochezea demokrasia yetu.
 
Kwa hii comment yako kama nchi tunasafari ndefu sana, hivi mkuu huu ushabiki wenu wa vyama unawanufaishaje

..bila vyama nchi itaongozwa nanna gani?

..usilaumu tu bali toa mapendekezo ya mfumo unaotaka utuongoze.

..mimi natamani tuongozwe na demokrasia ya vyama vingi vilivyo na HAKI sawa.
 
Tuliwaonya kuwa laana ya kushangilia kifo cha Magufuli ni kubwa.

Baada ya miaka 3 mnayo hiyo amani mliyosema mtapata? Hamtekwi tena? Hamshindwi tena kwenye chaguzi? Watu hawakimbii chama chenu tena?

Na laana iwatafune milele nyie
Bora laana hiyo mara 1000 kuliko kuwa na yule nduli.
 
Huyu zile risasi hazikumpa alarim nini??

Shauri yake anaanza kuwacholonoa maadui zake waliomshambulia wakijua atasingiziwa mwingine.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara Tundu Lissu akizungumza katika mtandao wa kijamii wa Clubhouse amenukuliwa akisema

"Kuna tatizo la rushwa ya uchaguzi, yeyote anayesema hakuna tatizo anatudanganya, kuna tatizo la rushwa ya uchaguzi na rushwa ya uchaguzi ya mtu yeyote yule ni adui wa demokrasia na ni adui wa haki, kiongozi yeyote anayepatikana kwa kununua wapiga kura huwauza siku ikifika, kwa hiyo nilichokisema Iringa ninakisimamia kama nilivyokisema, kuna tatizo la rushwa linatuvuruga CHADEMA.

Tuangalie sisi wapika kura tuwe macho na wagombea wanaokuja kwa sababu wamenununua kugombea kwao, kwa sababu wamehonga ili wateuliwe wagombea, kwa sababu wamechafua ili waje wapate nafasi za kugombea na kuchaguliwa, Ninasimamia katika kile nilichokisema Iringa na tuwe macho"-

JAMBO TV
Muñgu wabariki wazungu.
By Erythrocyte
 
Khe! Hakuna mwenye nafuu 🤣🤣🤣
 
Lisu kwanini unazunguuuka sana ilhali ukweli unaujua? mla RUSHWA namba 1 ndani ya chadema ni huyo mwenyekiti wako Mbowe mwenyewe.. acha kujipotezea muda mw/kiti wako ni ndumi la kuwili, panya buku anaeng'ata na kupuliza. acheni UTOTO JAZZ BAND basi.
 
Bado unaamini CHADEMA ya Mbowe inafika 2026 salama kwa mwendo huu ?​
Kwa bahati nzuri Mbowe ana historia ya kukiongoza na kukijenga chama chake wakati kinapita katika wakati mgumu. Sidhani kama Lissu ana huo uwezo. Kwangu mimi jinsi anavyoendesha kampeni yake ni bendera nyekundu. Sidhani kama atakuwa na uvimilivu kwa wale watakao tofautiana nae. Nadhani atakimbilia kutaka kuwa bomoa in public. Mbowe toka ametangaza kugombea hajasema kitu in public kuhusu mpinzani wake pamoja na provocation zote. Hii ni kwa sababu anajua ni vigumu sana vidonda vinavyotokana na maneno. Ndio maana namuunga mkono Mbowe.

Amandla...
 
Kwann isitafutwe pesa nzuri tu apewe Mhe L? Ili iwe rahisi sisi kupenya uchaguzi Mkuu? Maana tuna makando kando sio poa
 
Back
Top Bottom