Tundu Lissu: Kwa Sheria yetu hakuna Uhaini wa Maneno

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Leo Septemba 25, 2026, Tundu Lissu ameendelea kutoa majumuisho ya mwisho Mahakamani kufuatia Kesi ya Uhaini inayomkabili.

Katika wasilisho lake la leo, Tundu Lissu amesema kwa mujibu wa Sheria yetu iliyoundwa kutoka kwa Sheria ya Uingereza hakuna Uhaini wa maneno kama yeye anavyotuhumiwa kwa kwa maneno ya 'Tutakinukisha'

"From that time to this day, English law on treason is counted as Section 39 of our Penal Code.
Our Penal Code was enacted in 1930 by British law.

Kwa vile English law ilishafuta uhaini wa maneno, ndiyo maana sheria yetu vilevile haijawahi kuwa na uhaini wa maneno.

Na ndiyo maana, Waheshimiwa Majaji, Marehemu Jaji Mkuu Francis Nyarali kwenye kesi ya Khatibu Ghandi alisema kuwa maneno matupu hayafanyi uhaini.
Alikuwa anajua hii sheria imetoka wapi.

Waheshimiwa Majaji, nimesema hiyo sheria ya uhaini kama ilivyopendekezwa na Uingereza kwa Tanganyika, Uganda, Kenya na Nyasaland.

Isipokuwa nchi mmoja imeongeza uhaini wa maneno.
Uganda, katika Penal Code yao, wameongeza uhaini baada ya Mwingereza kuondoka.
Kwa sheria yetu, hakuna uhaini wa maneno.

Napendekeza uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Uingereza:
Regina v Her Majesty's Attorney General (Ex parte Rusbriger and another) [2003] UKHL.
Wanataka kuingiza kitu kwenye kesi hii wakati Waingereza waliotuletea sheria hii waliachana nacho tangu mwaka 1890; wao wanataka kukileta leo.

Pia, lengo la upande wa mashtaka ni kuingiza uhaini wa maneno katika sheria zetu ambao haujawahi kuwa katika sheria zetu milele.

Na tatu, hoja hii ya upande wa mashtaka inapinga msimamo wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwenye kesi ya Khatibu Ghandi, kwamba maneno matupu hayatengenezi uhaini."

Fuatilia zaidi Kinachojili Mahakamani leo 25 September, kesi ya Uhaini Tundu Lissu vs Jamhuri

1790322385378.png

Chanzo kutoka kwa WhatsApp Channel ya Twaha Mwaipaya
 
Ulitamka kwamba mtakinukisha, mtazuia uchaguzi mkuu na kuvuruga uchaguzi huo wa kikatiba nchini, kweli si kweli?

Ulisema mtakinukisha, mtazuia na kuvuruga uchaguzi mkuu upi? Je, nikisema mlikusudia kuyafanya hayo siku ya uchaguzi mkuu wa Oct 2025, ntakua nakusingizia?

Je,
hamkufanikiwa kwa vitendo mipango hiyo haramu kwa wakati muafaka kama mlivokubaliana kwenye kamati kuu ya chadema taifa na kusababisha uvunjifu wa amani, uharibifu na maafa kwa waTanzania?

mbona unasema uongo ndugu muhaini aise? Na mbona haukutamka kama hayo uliyoyasema yanaishia kua maneno tu until mmetenda kwa vitendo ndio unakuja tena kudai eti yalikua ni maneno matupu?🐒
 
alifanikiwa wakati mlimfunga UKONGA, sababu ya papara zenu mnaenda kushindwa kesi, mngesubiri akinukishe akiwa nje ndio mmunyonge, sas amechi umeweka marewa wewe na mnaenda kushindwa
 
Ulitamka kwamba mtakinukisha, mtazuia uchaguzi mkuu na kuvuruga uchaguzi huo wa kikatiba nchini, kweli si kweli?

Ulisema mtakinukisha, mtazuia na kuvuruga uchaguzi mkuu upi? Je, nikisema mlikusudia kuyafanya hayo siku ya uchaguzi mkuu wa Oct 2025, ntakua nakusingizia?

Je,
hamkufanikiwa kwa vitendo mipango hiyo haramu kwa wakati muafaka kama mlivokubaliana kwenye kamati kuu ya chadema taifa na kusababisha uvunjifu wa amani, uharibifu na maafa kwa waTanzania?

mbona unasema uongo ndugu muhaini aise? Na mbona haukutamka kama hayo uliyoyasema yanaishia kua maneno tu until mmetenda kwa vitendo ndio unakuja tena kudai eti yalikua ni maneno matupu?🐒
Unaandika kama unanyonya paipu mdomono
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 12.

1. Ni kumuua au kujaribu kumuua Rais — 39(1)(a).

2. Kuendesha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano — 39(1)(b).

Waheshimiwa Majaji, tunaingia 39(2). Kuna matendo manne ambayo ukitenda unakuwa umetenda uhaini.

3. Kutengeneza nia ya kuwezesha au kusababisha mtu au kikundi kumjeruhi Rais. Kumpiga Rais, kumjeruhi Rais, huo ni uhaini.

4. Kutengeneza nia ya kuwezesha au nia ya wengine kuwezesha au kusababisha Rais apinduliwe kwa njia zisizo halali kutoka katika nafasi yake ya Urais, au kumtoa katika nafasi yake ya Amiri Jeshi Mkuu — 39(2)(a).

5. Ukitengeneza nia ya kuwezesha mtu au kikundi kusababisha au kuwezesha kulimdukiwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano — 39(2)(c).

6. Ukitengeneza nia ya kuwezesha au kutengeneza nia ya mtu kuwezesha au kikundi cha watu kutishia Bunge au Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kosa mengine yapo kwenye 39(3).

7. Ukijiunga au kujishirikisha na maadui wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, au ukawapa kinywaji au chakula maadui wa Jamhuri — 39(3)(a).

8. Kuchochea mtu yeyote kuivamia nchi ya Jamhuri ya Muungano kwa silaha. Mfano, ukileta M23 Tanzania, ni uhaini — 39(3)(b).

9. Mtu yeyote atakayechukua silaha ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa lengo la kulazimisha mambo dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Tanzania — 39(3)(c).

10. Mtu yeyote aliye na utii kwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania akisaidia maadui wa Jamhuri ya Muungano kwa lengo la kuzuia shughuli za kijeshi au kuhatarisha maisha katika operesheni za kijeshi — 39(3)(d).

Sasa, Waheshimiwa Majaji, kama hayo ndiyo uhaini kama ilivyotafsiriwa na sheria.

Tuanze na “tutavuruga uchaguzi.”

Ipo wapi katika hayo yaliyofafanuliwa na Kifungu cha 39 cha Kanuni ya Adhabu?

Twende kwenye “tutazuia uchaguzi.” Haipo, siyo constructively.

Twende kwenye “tuhamasisha uasi.” Ipo wapi?

Kwa Kiingereza ni “rebellion”, ama kama ambavyo tulisomewa katika kamusi: “Kupinga jambo kwa nguvu.”

Twende kwenye “kukinikisha.” Ipo wapi?

Ili walau leo wanangu, wherever they are, wajue baba yao yupo gerezani kwa mwaka mmoja na nusu. Baba yao kuna kosa kafanya. Haipo.

Waheshimiwa Majaji, kwenye haya ya sheria yapo wapi? Hayapo.

Nimefungwa mwaka mmoja na nusu kwa uonevu.

Nimeonewa.

Nina ndugu hapa, wanakuja kila siku hapa nimefungwa.

Nina wanachama hapa, wanakuja kutoka kila mahali. Mwenyekiti wao nimefungwa, nipo gerezani.

(Watu wanalia.)

Nalindwa na askari kama vile ni muuaji. Kwa kosa gani?

Waheshimiwa Majaji, kama haya hapo, ugomvi hapa ni uchaguzi.

Tulitaka kuzuia uchaguzi, tulitaka kuvuruga uchaguzi.

Twende break.

Lissu: Sawa, Mheshimiwa.

Jaji Ndunguru: Upande wa mashtaka?

Job Mrema: Hatuna pingamizi, Mheshimiwa.

Jaji Ndunguru: Bado sana kuwasilisha.

Lissu: Siwezi kusema nikajifunga.

Nisije nikafanya mambo kwa hisia.

Jaji Ndunguru: Basi tutabreak kwa saa moja na nusu. Tutarudi hapa saa 8:30.

Majaji wanatoka.
 
Leo Septemba 25, 2026, Tundu Lissu ameendelea kutoa majumuisho ya mwisho Mahakamani kufuatia Kesi ya Uhaini inayomkabili.

Katika wasilisho lake la leo, Tundu Lissu amesema kwa mujibu wa Sheria yetu iliyoundwa kutoka kwa Sheria ya Uingereza hakuna Uhaini wa maneno kama yeye anavyotuhumiwa kwa kwa maneno ya 'Tutakinukisha'

"From that time to this day, English law on treason is counted as Section 39 of our Penal Code.
Our Penal Code was enacted in 1930 by British law.

Kwa vile English law ilishafuta uhaini wa maneno, ndiyo maana sheria yetu vilevile haijawahi kuwa na uhaini wa maneno.

Na ndiyo maana, Waheshimiwa Majaji, Marehemu Jaji Mkuu Francis Nyarali kwenye kesi ya Khatibu Ghandi alisema kuwa maneno matupu hayafanyi uhaini.
Alikuwa anajua hii sheria imetoka wapi.

Waheshimiwa Majaji, nimesema hiyo sheria ya uhaini kama ilivyopendekezwa na Uingereza kwa Tanganyika, Uganda, Kenya na Nyasaland.

Isipokuwa nchi mmoja imeongeza uhaini wa maneno.
Uganda, katika Penal Code yao, wameongeza uhaini baada ya Mwingereza kuondoka.
Kwa sheria yetu, hakuna uhaini wa maneno.

Napendekeza uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Uingereza:
Regina v Her Majesty's Attorney General (Ex parte Rusbriger and another) [2003] UKHL.
Wanataka kuingiza kitu kwenye kesi hii wakati Waingereza waliotuletea sheria hii waliachana nacho tangu mwaka 1890; wao wanataka kukileta leo.

Pia, lengo la upande wa mashtaka ni kuingiza uhaini wa maneno katika sheria zetu ambao haujawahi kuwa katika sheria zetu milele.

Na tatu, hoja hii ya upande wa mashtaka inapinga msimamo wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwenye kesi ya Khatibu Ghandi, kwamba maneno matupu hayatengenezi uhaini."

Fuatilia zaidi Kinachojili Mahakamani leo 25 September, kesi ya Uhaini Tundu Lissu vs Jamhuri

Chanzo kutoka kwa WhatsApp Channel ya Twaha Mwaipaya
Amefanya exploration ya Sheria zote husika
 
Kujua kwingi ye anaona jokes ila wanaweza kumfunga huyu na kumpoteza kimzamzaha tu.
Akihukumiwa ndo atajua kamwaga Michele kwenye kuku wengi.
Huyu atapigwa kifungo then itapita parole atolewe ila asishiriki shughuli za kisiasa.
Sasa imagine Heche ndio Mwenyekiti mrithi chandemo km Sambua.
Hakuna rangi mtakosa kuiona
 
Pamoja na Yote hakuna Ubishi kwamba Jamaa anajua
 
Uko third Word country my friend.
Hizo sheria anazopiga nazo makelele hapo nakujionyesha anajua.
Hao wataendelea kumpoteza tu ili washinde wao.
Kumbuka ana kesi ya kujibu.
 
Kujua kwingi ye anaona jokes ila wanaweza kumfunga huyu na kumpoteza kimzamzaha tu.
Akihukumiwa ndo atajua kamwaga Michele kwenye kuku wengi.
Huyu atapigwa kifungo then itapita parole atolewe ila asishiriki shughuli za kisiasa.
Sasa imagine Heche ndio Mwenyekiti mrithi chandemo km Sambua.
Hakuna rangi mtakosa kuiona
Kwani umesikia yeye anahofia hilo? Mbona ana amani muda wote
 
Amani iko kwako sikuiti mkuu.
Ukikaa mule ndani ndo utajua hujui,
Na kwa taarifa yako yule yuko mahabusu jina tu anakula bata iwe huko ndani au nje.
Anawatapeli tu minyumbu nyie.
 
Back
Top Bottom