Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
Mkuu tunatambua kuwa Lissu alipata madhila makubwa sana toka utawala wa Jiwe. Mtu asidhani kama tunapuuza yaliyomfika. Ni muujiza tu umemrejesha duniani akiwa na akili zake timamu na ujasiri aliokuwa nao. Ana uelewa mkubwa wa kitaaluma na uzoefu mkubwa wa katiba, sheria na siasa za Tanzania. LAKINI ana jazba kama alizokuwa nazo Hayati. Hatulii na kuona mambo muhimu ya msingi ya kusimamia kitaifa. Bado anashabikia mipasho isiyo na tija.Sijui kama watakusoma wakuelewe hao walioshikiwa akili na Lissu, since 2018 anampigia kelele Magufuli mpaka leo 2021 Magufuli is no more still bado anapayuka tu, hawezi kuwa mzima huyu mtu!
Angetufaa sana angeamua kubeba dhamana KUU ya kuisaidia nchi kujijenga upya kwa mifumo na michakato makini ya kisiasa, kitaasisi, kiuongozi, kiuchumi na kijamii. Zile risasi 36 alizo"survive" ni mhanga tosha wa kufanya asikilizwe na kutiliwa maanani akiongea mambo yenye "substance" kwa taifa. Jiwe tayari kawa historia tusiyopenda kuirudia. Hatuhitaji mipasho kumhusu Jiwe wakati huu. He needs to assume statesmanship or end up irrelevant.