Pre GE2025 Tundu Lissu: Mbowe alimtuma Wenje agombee nafasi yangu ili waniondoe, nikasema sasa nitagombea nafasi ya huyo aliyekutuma

Pre GE2025 Tundu Lissu: Mbowe alimtuma Wenje agombee nafasi yangu ili waniondoe, nikasema sasa nitagombea nafasi ya huyo aliyekutuma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu

Tundu Lissu "Ninajua kuwa Mbowe ndiye aliyemtuma Wenje agombee nafasi ya Makamu Mwenyekiti nikasema sasa nitagombea nafasi ya huyo aliyekutuma"

Pia, Soma:

Ezekia Wenje: Siwezi kununa Lissu akiwa Mwenyekiti CHADEMA

Lissu: Mbowe ni muongo, tulifanya kikao cha siri kwa siku 3. Alikataa nisigombee Urais na Uenyekiti huku yeye akisema hajaamua

View attachment 3194129
Wengi wamekuwa wakitamani kugombea uenyekiti, ila wakikutana na uso wa Mbowe unawasikia"mitano tena kwa mwamba" 😆 😆 😆 😆 😆 😆 😆 Ila huyu Jamaa amethubutu na meweza.
 
Wengi wamekuwa wakitamani kugombea uenyekiti, ila wakikutana na uso wa Mbowe unawasikia"mitano tena kwa mwamba" 😆 😆 😆 😆 😆 😆 😆 Ila huyu Jamaa amethubutu na meweza.
Lissu uoga umeisha muda mrefu hataki upuuzi
 
Sasa kumbe ndani ya CHADEMA kuna shida ya mgawanyiko. Mungu aepushie mbali chama hiki kisife. Kikifa CCM watatusumbua sana.
Jana Heche alisema "Natamka kwa kifupi sana, aliyetufikisha hapa ni Wenje" Udalali wa Wenje ndiyo umegharamia haya yote. Wenje asingevuruga mambo na Mbowe wake wala wasingefika humu.

Mtu hana msimamo kumbe walishakula dili siku nyingi.
 
Hata TL hakufaulu vizur O level... Ndio maana Advance akaenda Galanos 😂.

UDSM wala hakupata First class honors aache kutulisha u smart fake, hizo Upper second ni za watu aver
Hii iko personal sanaa Mh.lissu alikutenda kitu gani tujue mapema
 
Hivi ikitokea katibu mkuu Mnyika akajiuzulu, huo uchaguzi utakuwaje?

Anayeratibu huu uchaguzi si ofisi ya katibu mkuu au?
 
Kabisa Mkuu. Na haikupaswa kabisa kuwa hivyo. Mimi bado naamini kuwa wafuasi wa Lissu (bila shaka kwa baraka zake) wasingeanza kwa shari kampeni yake, Mbowe angestaafu. Sasa hivi yeyote atakayeshinda atakuwa na chama chenye majeraha makubwa. Labda wanaamini kuwa CDM ilipofika haiwezi kuwa kama TLP au NCCR Mageuzi.! Wanaweza kushangazwa.

Amandla...

Mbowe si ni mvumilivu, avumilie tu.Asichukue uamuzi kwa kutunisha misuli. Aonyeshe uvumilivu wake kwa kustaafu badala ya kuwa kinganganizi
 
Mbowe si ni mvumilivu, avumilie tu.Asichukue uamuzi kwa kutunisha misuli. Aonyeshe uvumilivu wake kwa kustaafu badala ya kuwa kinganganizi
Uvumilivu ni kuachia wenye mamlaka ya kuamua waamue hatma yake. Kustaafu kwa sababu watu wanamsema vibaya sio uvumilivu bali uoga. Akifanya hivyo watu watachukua uamuzi wake kama wa kukiri ukweli wa tuhuma hizo.
Wenje kasema Mbowe amechangia milioni 250 kukiwezesha chama kuweza kufanya huo uchaguzi. Leo Lissu anahoji hizo pesa amezitoa wapi maana hamna ushahidi wowote wa biashara anazofanya. Swali ni kwa nini wafuasi wa Lissu mnatumia nguvu za ziada kumtaka Mbowe ajitoe katika huu uchaguzi? Mnaogopa nini maana kila kukicha kuna matangazo ya wajumbe wa mikoani wakimuunga mkono mtu wenu?

Amandla...
 
Back
Top Bottom