Pre GE2025 Tundu Lissu: Mchungaji Peter Msigwa ni rafiki yangu, lakini nitamkabili Kisiasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Tundu Lissu, amesema kuwa pamoja na kuwa na urafiki wa muda mrefu na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mchungaji Peter Msigwa, kwa sasa hawezi kumkwepa kumkabili kisiasa, kwani Msigwa amehamia chama pinzani na si mwanachama mwenzie tena.

Lissu amekiri kuwa hawezi kukana urafiki wake na Msigwa, akisisitiza kuwa hata aliposhambuliwa, Mchungaji Msigwa alishika chupa ya damu hadi wakati yeye anapelekwa hospitali.
 
MIMI SIO CHADEMA

Nimesoma gazeti la mwananchi la jana inasema kwamba msigwa ndio anaopanga mikakati ya LISSU yote,
Msigwa ndio anawapigia simu viongozi wa chadema ili wamunge mkonko Lissu, Msigwa huyu wa CCM hapa ndio Lissu kajimaliza kisiasa. Lissu hatoboi tena chadema na kila hatua mbele tutakoenda Lissu ndani ya chadema haaminiki tena na mbele yake ngumu kuliko nyuma yake.

Lissu licha ya kuwa mwanasiasa machachari lkn yaliomkuta Baada kumiminiwa risasi na jinsi Mbowe Mwenyekiti alivyochukua jitihada za kumnusuru maisha yake hii pekee inamjengea Mbowe credit kubwa ndani ya chadema kwa Lissu.

Ukweli ni kwamba wengi tunamuunga mkono lissu ni Act wazalendo ya ZITTO, NCCR ya Mwambukusi na wachache ndani ya CCM na kidugu ndani ya chadema akiwemo Askofu mwana mapinduzi.

Ijumaa lkareem
 
Tulia, ku deal na Lissu ni sawa sawa na Kusema Nyerere ndo Rais wa Tanzania kwa sasa, Lisu ni chimbuko la mageuzi, nyie walonzi hamuwezi kabisa kupredict moves za Chadema na Lisu, mtapigwa nje ndani hamtaamini!
 
MIMI SIO CHADEMA

Nimesoma gazeti la mwananchi la jana inasema kwamba msigwa ndio anaopanga mikakati ya LISSU yote,
Msigwa ndio anawapigia simu viongozi wa chadema ili wamunge mkonko Lissu, Msigwa huyu wa CCM hapa ndio Lissu kajimaliza kisiasa. Lissu hatoboi tena chadema na kila hatua mbele tutakoenda Lissu ndani ya chadema haaminiki tena na mbele yake ngumu kuliko nyuma yake.

Lissu licha ya kuwa mwanasiasa machachari lkn yaliomkuta Baada kumiminiwa risasi na jinsi Mbowe Mwenyekiti alivyochukua jitihada za kumnusuru maisha yake hii pekee inamjengea Mbowe credit kubwa ndani ya chadema kwa Lissu.

Ukweli ni kwamba wengi tunamuunga mkono lissu ni Act wazalendo ya ZITTO, NCCR ya Mwambukusi na wachache ndani ya CCM na kidugu ndani ya chadema akiwemo Askofu mwana mapinduzi.

Ijumaa lkareem
Gazeti la Mwanachi limekuwa kipeperushi cha CCM na limetumika sana kuchochea mgogoro hewa ndani ya Chadema. Leo limeandika kuwa jana Lissu aliisifia sana CCM kuwa inaendeshwa kidemokrasia jambo ambalo ni uongo. Mwananchi limejiondolea heshima yake kwa jinsi linavyoripoti habari za Chadema.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Tundu Lissu, amesema kuwa pamoja na kuwa na urafiki wa muda mrefu na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mchungaji Peter Msigwa, kwa sasa hawezi kumkwepa kumkabili kisiasa, kwani Msigwa amehamia chama pinzani na si mwanachama mwenzie tena.

Lissu amekiri kuwa hawezi kukana urafiki wake na Msigwa, akisisitiza kuwa hata aliposhambuliwa, Mchungaji Msigwa alishika chupa ya damu hadi wakati yeye anapelekwa hospitali.
Hizo habari za Msigwa kuwapigia simu viongozi wa CHADEMA eti kumpigia kampeni Lisu kuwa mwenyekiti, ni uwongo mkubwa. Hao wanaosema hivyo ni mamluki wa CCM wanaotafuta sababu usiku na mchama kuivuruga CHADEMA, lakini hawatafanikiwa. Kwa maneno kama hayo watawaokota wasio na akili.

Lisu kama ilivyo dhamira yake, na awaye mwingine yeyote, atagombea hiyo nafasi. Mwenyekiti wa sasa anaweza kugombea au anaweza asigombee, maana haki zote anazo kikatiba.

Na mwenyekiti Mbowe siku zote amesisitiza kuwa CHADEMA siyo ya Mbowe, siyo ya Lisu wala Mnyika, ni ya watanzania wote. Yeyote anaweza kuwa mwanachama, na yeyote anaweza kuwa kiongozi alimradi anazo sifa. Machawa na maharamia ya CCM ndiyo yanayotaka kuwaaminisha watu kuwa kugombea cheo chochote ndani ya CHADEMA, maana yake umetangaza vita na mshindani wako!!

Subirini, Mbowe atawashangaza kwa hekima, machawa watabakia midomo wazi.
 
Gazeti la Mwanachi limekuwa kipeperushi cha CCM na limetumika sana kuchochea mgogoro hewa ndani ya Chadema. Leo limeandika kuwa jana Lissu aliisifia sana CCM kuwa inaendeshwa kidemokrasia jambo ambalo ni uongo. Mwananchi limejiondolea heshima yake kwa jinsi linavyoripoti habari za Chadema.
Gazeti la mwananchi kwa sasa, halinalizidi gazeti la uhuru. Yumkini mhariri wake atakuwa amefikiwa na Abdul. Wanaandika vitu utadhani huyu Lisu alihutubia akiwa amejifungia chumbani na mwandishi wao. Wanaandika uwongo ulio dhahiri wakati wanajua kuwa hotuba ya Lisu ilikuwa public kwa watu wote, na kila aliyetaka kusikiliza, alisikiliza live.

Gazeti la mwananchi, kama yalivyo mengine, kwa sasa halina mauzo, watendaji wameamua kujisalimisha kwa Abdul ili waendelee kuishi na kupata uwezo wa kyendelea kulichapisha.
 
Hizo habari za Msigwa kuwapigia simu viongozi wa CHADEMA eti kumpigia kampeni Lisu kuwa mwenyekiti, ni uwongo mkubwa. Hao wanaosema hivyo ni mamluki wa CCM wanaotafuta sababu usiku na mchama kuivuruga CHADEMA, lakini hawatafanikiwa. Kwa maneno kama hayo watawaokota wasio na akili.

Lisu kama ilivyo dhamira yake, na awaye mwingine yeyote, atagombea hiyo nafasi. Mwenyekiti wa sasa anaweza kugombea au anaweza asigombee, maana haki zote anazo kikatiba.

Na mwenyekiti Mbowe siku zote amesisitiza kuwa CHADEMA siyo ya Mbowe, siyo ya Lisu wala Mnyika, ni ya watanzania wote. Yeyote anaweza kuwa mwanachama, na yeyote anaweza kuwa kiongozi alimradi anazo sifa. Machawa na maharamia ya CCM ndiyo yanayotaka kuwaaminisha watu kuwa kugombea cheo chochote ndani ya CHADEMA, maana yake umetangaza vita na mshindani wako!!

Subirini, Mbowe atawashangaza kwa hekima, machawa watabakia midomo wazi.
Gazeti la Mwananchi ndiyo linaeneza hizo habari. Wasichojua ni kuwa suala la Lissu kugombea uenyekiti lina baraka zote za Mbowe, kwani barua ailishaandikwa kwa Katibu Mkuu, hata juzi kwenye press waliyokuwa pamoja jambo hili walishalimaliza.Ngoja hao vibaraka wa CCM waendelee kujipa matumaini kuwa Chadema inapasuka.
 
Back
Top Bottom