Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Mkimchagua Magufuli, ana lengo la kubadili Katiba kuondoa ukomo wa vipindi vya kutawala


Umeandika maelezo marefu, lakini ukweli ni kuwa vyombo vya habari kwa sasa chini ya Magufuli haviko huru. Hayo uliyosema eti vyombo vya habari enzi za Slaa vilikuwa vinatoa habari maana vilijua ni kweli asemacho, si kweli bali vyombo vya habari vilikuwa vina uhuru wa kuridhisha wakati huo kuliko sasa. Kuna siku Slaa alisema kuwa kuna container lina kura zilizopigiwa ccm tayari, lakini ilifahamika baadae kuwa sio kweli, na habari ile ilitangazwa.

Ni hivi, vyombo vya habari kwa sasa haviko huru chini ya dictator, hivyo sio rahisi kwa mkosoaji wa dictator kuruhusiwa habari zake za kweli kutangazwa. Hilo la kuwa Magufuli ana mpango wa kubadilisha katiba ili akae madarakani zaidi, hilo wala halina kificho. Liko wazi peupe.
 

Uza ubongo huo maana unakaa nao kwa hasara.
 
Mkimpitia Magufuli mtalimia meno. Watumishi wengine wa umma nafasi zenu haziwapi hata fursa ya kupata elfu kumi kwa siku nje ya mshahara. Twende na Magu mpaka nimalizie Nyumba yangu ya pili. Huu wakati una upepo wa pesa sana
 
Gadafi alikua dikteta lakin libya waliishi kwa raha

Waliishi kwa raha, hakuna maisha ya raha chini ya dictator, zaidi ya maisha ya ukondoo. Ukitaka uishi kwa raha chini ya dictator unatakiwa uweke mkia matakoni na kumsifia basi. The same applies to here.
 
Uhuru wa vyombo vya habari ni kuandika ukweli sio uongo

Tatizo chadema ni kudhani uandishi wa habari kazi yake tu ku report kama kasuku bila kuangalia ukweli wa hiyo habari
 
Tatizo Lissu hajui vizuri siasa za majukwaani,laiti angefanya tathimini ya hotuba zake kabla ya kuzitapika.
Wapo wasaidizi wake wanammaliza haraka kwa kill me quick pills
Akiendelea kusema sema mbovu wapiga kura watamrarua bila huruma kwenye sanduku la kura.
 
Hii ni dalili tosha ya mfa maji. Hana sera. Badala ya kusema atawafanyia nini Watanzania anakuja na mambo ya kufikirika. Mwaga sera TL kama huna basi kaa kimya.

Amemwaga Sera kibao, ila mleta mada kaleta kipande hiki tu. Ukitaka nenda mwenyewe kwenye mikutano yake ukasikie kila kitu.
 
Lissu anakosa hoja, yeye aseme akiwa raisi atawafanyia nini watanzania kupitia kodi wanazolipa. Yeye amekuwa prophet kusema yajayo?
 
Uhuru wa vyombo vya habari ni kuandika ukweli sio uongo

Tatizo chadema ni kudhani uandishi wa habari kazi yake tu my report kama kasuku bila kuangalia ukweli wa hiyo habari

Uko sahihi kuwa uhuru wa habari ni kuandika ukweli na sio uongo. Ila hapa kwetu kwa sasa, tatizo ni kuandika ukweli unaomkera Magufuli na serikali yake. Hili liko wazi, hatusemi hakuna uhuru wa habari kwakuwa tunataka habari za uongo, bali tunataka habari za ukweli bila kujali zinamuumiza nani. Tatizo la sasa ni habari ziwe zile zinazoiufurahusha serikali tu.
 
Lissu anakosa hoja, yeye aseme akiwa raisi atawafanyia nini watanzania kupitia kodi wanazolipa. Yeye amekuwa prophet kusema yajayo?

Lisu ameongea hoja nyingi sana kwenye huo mkutano, ila ww unajadili kipande hiki. Dalili ya mvua ni mawingu, kwani ukisema mvua itanyesha ni makosa kwakuwa wewe sio prophet?
 
Kumsema mtu wako kuwe na ukweli sio tu kumsema mfano mimi nasema mkutano wa hadhara kuwa Lisu ni kichaa unataka vyombo vya habari viandike hilo wakati havijaona cheti cha daktari na ushahidi wa hilo nililosema?

Waandishi wetu wa sasa ni wasomi sio makasuku wa kuripoti chochote anachosema mtu
 
Baada ya kiki za miujiza kubuma, amebaki kuwa mtabiri kama nabiii Tito.
Aaache kuweweseka , kipigo chake kiko palepale.
 
View attachment 1565776
ukilinganisha na kauli zake,jibu unapata. Huu ukorofi na kutisha watu huwezi kuondoka kizembezembe tu halafu nani atakulinda. Hawa kina M7 wanapenda wapumzike ila wanaogopa maisha baada ya uraisi

Exactly.. lazma aogope maisha baada ya kudhulumu, kunyanyasa watu. Huyu haki ya Mungu lazima ang’ang’anie tena kuongoza. Na hapo atamtumia huyo huyo Speaker uchwara.
 
Nyumbu ni nyumbu tu,kila analosema Lissu mnalibeba.
 
Lissu ndiye Rais wetu. Hiyo October ifike tumalize mambo. Mwandalieni Mzee wa Chato makao huko kijijini.
 
Lisu ameongea hoja nyingi sana kwenye huo mkutano, ila ww unajadili kipande hiki. Dalili ya mvua ni mawingu, kwani ukisema mvua itanyesha ni makosa kwakuwa wewe sio prophet?
Toka lisu akiwa bungeni mpaka Leo, zaidi ya kutengeneza maigizo na KIKI ,kunalolote la maanaa ambalo ameliibua la kulisaidia selikali na watanzania kwa ujumla?
Taja hata hoja yoyote ambayo lisu ameshachangia bungeni au kuibua likawa msaada kwa taifa.
 
Hii ni dalili tosha ya mfa maji. Hana sera. Badala ya kusema atawafanyia nini Watanzania anakuja na mambo ya kufikirika. Mwaga sera TL kama huna basi kaa kimya.
Chadema inarusha mateke ya mwisho kabla ya kukata roho
 
Ivi anayefikiri kuongeza mishahara ya watumishi kama motisha ili apendwe kisiasa anapima mzani kwa dhati kweli?

Yaani aanze na kusema atatoa wapi fedha za kuongeza, kama chanzo ni Kodi kutoka kwa hawa wananchi wadogo, basi sio hoja kiviiiiile!!!
 
Eti kwamba anaiamini zaidi kauli ya ndugai kuliko ya magufuli mwenyewe ambaye amekuwa akisisitiza kuiheshimu katiba katika kuongoza..

Kwamba ameanza kumuamini sana ndugai..ila ndugai akimueleza yeye ukweli anakuja juu..
Raisi katiba ikimtaka aendeleze vipindi zaidi ya 10 hawezi kukataa.

Spika kwenye hili ana nguvu kuliko raisi maana yeye kupitia wawakilishi wa wananchi ndio wanaweza kusema miaka kumi haitoshi au inatosha.

Raisi yeye anatii. Kwa sasa raisi hawezi kusema ataongeza muda maana katiba haimruhusu na si kazi yake kubadili katiba, hiyo ni kazi ya wananchi kupitia wawakilishi.

Katiba itakapobadilika, Raisi ni ngumu kusema hapana ikiwa nchi inamuhitaji na atakapokubali haitamaanisha kuwa alisema uongo kuwa hatoongeza muda, maana anafata matakwa ya wananchi.

Swali ni, wananchi wanatakaje? Jibu litapatikana pale ambapo Raisi atachaguliwa tena na mswada ukaletwa bungeni na mambo yakabadilika halafu wananchi wakaafiki na wakatulia. Kimya maana yake hakuna tatizo. Propaganda kuwa wananchi ni waoga wa polisi na jeshi hazitakuwa na maana wala hazitabadili uhalisia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…