Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Mkimchagua Magufuli, ana lengo la kubadili Katiba kuondoa ukomo wa vipindi vya kutawala

Wamrarue mara ngapi..? Alipowaaminisha watu kwa nguvu atagombea watu walijua ana kitu kipya tofauti..sera zake zimeegemea zaidi watu wa mjini tena waliojiriwa.. ukimuambia mkulima au mfugaji nitaongeza mshahara wa miaka mitano atakuelewa nini? Sana sana ni kama unamtenga maana yeye hana pa kuongezewa mshahara.

Unamueleza mtu bima ya afya kabla hujamjengea hospital na kumletea wataalam hiyo bima atajitibia kwa mganga wa kienyeji?

Kuna mambo ambayo watu yanawagusa kwa pamoja..ukisema uboreshaji wa usafiri wa ndege, maji, reli na barabara nzuri tayari umegusa kila kundi, ukisema elimu bure, ujenzi wa madarasa, mikopo elimu ya juu, viwanda na ajira hapa umegusa wote, ukisema zahanati, vituo vya afya, hospital za mikoa..hapa napo umegusa mtu wa kijijini hadi wa mjini...ukisema uhakika wa maji..hapa umegusa mjini na kijijini..uhakika wa umeme (JNHPP) na REA..hapa umewagusa wa mjini na vijiji..

Ukianza kusema ooh kingereza ndio lugha, ooh bima ya afya, ooh nitaongeza mishahara, ooh maendeleo sio vitu wakati mkulima wa ndizi bukoba kule alikuwa anasafiri tani ya ndizi kwa 120000 na leo anasafirisha tani hiyo hiyo kwa elf 25 baada ya kupelekewa kitu ambacho ni meli..sidhani kama jamii itakuelewa.
 
Ivi anayefikiri kuongeza mishahara ya watumishi kama motisha ili apendwe kisiasa anapima mzani kwa dhati kweli?

Yaani aanze na kusema atatoa wapi fedha za kuongeza, kama chanzo ni Kodi kutoka kwa hawa wananchi wadogo, basi sio hoja kiviiiiile!!!

Sisi si ni matajiri
Tuna mihela mingi
Sasa kwa nini tuwe makatili tuvunjie watu nyumba kikatili wakati kuna zuio la mahakama kisha tusiwalipe?
 

Narudia tena, hivyo vyombo vya habari haviko huru ndio maana wanaogopa kuandika yanayosemwa na Lisu dhidi ya Magufuli. Siasa sio hesabu useme 2+2 ni 4, na ukiweka jibu lingine ni makosa. Hilo suala la Magufuli kutaka kujiongezea muda wa kukaa madarakani halina kificho, linasemwa wazi wazi hadharani na hata bungeni. Mfano rais Mstaafu Mwinyi amewahi kulisema, waziri mkuu mstaafu Pinda amewahi kulisema, huko bungeni ni zaidi ya mara moja limesema, tena kibaya zaidi limesemwa na spika na wabunge wa ccm. Kwa dalili kama hizo kwanini Lisu asitoe tahadhari kwenye kampeni?

Ifahamike kwenye kampeni ni pamoja na kusema mapungufu ya mpinzani wako, hasa hayo ya mifumo ya kiutawala kupitia katiba. Ingekuwa vyombo vya habari viko huru vingeandika, maana hiyo ni tahadhari halali kwa wapiga kura, labda kama hujui siasa ni nini?
 
Toka lisu akiwa bungeni mpaka Leo, zaidi ya kutengeneza maigizo na KIKI ,kunalolote la maanaa ambalo ameliibua la kulisaidia selikali na watanzania kwa ujumla?
Taja hata hoja yoyote ambayo lisu ameshachangia bungeni au kuibua likawa msaada kwa taifa.

Omba Hansard za bunge, kisha fuatilia sakata la Escrow. Ukishamaliza kusikiliza uje tuendelee na mjadala.
 
Nyie kila siku mnasema muhimili wa bunge hauna nguvu..sasa hivi tena unasema spika akitaka..ina maana hata kama magufuli hataki spika akitaka itakuwa hivyo..

Basi muifute ile kauli yenu ya kusema ooh bunge dhaifu..halina nguvu ya maamuzi..vinginevyo mtakuwa mnajitekenya wenyewe na mnacheka wenyewe.
 
Omba Hansard za bunge, kisha fuatilia sakata la Escrow. Ukishamaliza kusikiliza uje tuendelee na mjadala.
Inje ya kupayuka payuka na KIKI zake hajawahii ibua lolote la maana ambalo limekua msaada kwa taifa. Sasa hivi hana Sera yoyote zaidi ya kulazimisha apewe uraisi kama kifuta machozi .

Wapo mashujaa kama akina zito kabwe, kafulila na wengine wengi, waliibua ufisadi wa taifa hili hadi mtoto mdogo akafaham. Sasa huyo jamaa yenu inje na kushuhudia KIKI zake za miujiza ana lipi la maana kwa taifa letu?
 


chama chenyewe mmeshindwa kuchagua mwenye kiti mpya
 
Mzee anapanic mpka kaamua kujificha Shato kwanza
 

Kwa taarifa yako rais kupitia vyombo vya dola ana nguvu zaidi ya 80%, hiyo kuwa wananchi ndio wenye maamuzi ni porojo za kinadharia. Ukitaka kujua ninachosema, angalia sasa hivi ni wakati wa kampeni, ni wapi rais anajibu maswali ya wananchi zaidi ya kuwahutubia? Hao wabunge angalia kwenye kampeni, mkutano una masaa matatu, masaa mawili ni burudani, nusu saa ni wapambe wa mgombea wanaongea, kisha dakika 10-15 mgombea anaongea akitakacho bila kuulizwa swali lolote. Kisha dakika zilizobaki ni kuagana na Viroja.

Huo ndio mfumo wa kupata viongozi waitwao wawakilishi wa wananchi, na wanachoenda kujadili huko bungeni ni utashi wa rais aliye madarakani. Chochote atakacho rais, ndio kinapewa kipao mbele na viongozi waliopatikana kutokana na matamasha ya burudani. Wananchi wanaweza kupiga kura tu, tena hakuna uhakika wa matokeo ili kuhalalisha rais kuendelea kukaa madarakani, lakini hawana maamuzi yoyote ya kumuweka kiongozi madarakani, labda walete machafuko. Hizo porojo za kuwa wananchi ndio wanaweka viongozi madarakani ni porojo kwa wasiojua lolote.
 
sawa kabisa mkuu aanzie kwa mwenyekiti wake kumuuliza kwanini hana kikomo jpm alishasema hataongeza hata siku moja yeye hayo maneno anayatoa wapi aache wendawazimu wake amuulize mbowe atang'atuka lini uenyekiti
 

We robot hebu rudi studio wakakuprogram upya, au ufanyiwe updates ya taarifa kisha uje tuendelee na mjadala.
 
Mzee anapanic mpka kaamua kujificha Shato kwanza

Alikuwa anakimbizana na kasi ya Lisu, baada ya kuona kuwa kuna mgawanyo wa awamu za kampeni, na yeye kaona afanye hivyo. Huko sasa wale wazee wa gamboshi lazima waitwe, yapigwe Mazindiko ya hatari.
 
We robot hebu rudi studio wakakuprogram upya, au ufanyiwe updates ya taarifa kisha uje tuendelee na mjadala.
Matusi hayaondoi uhalisia wa kitu, kiukweli jamaa yenu inje ya KIKI hanamchango wowote kwa taifa hili, zaidi ya kuliangusha na kujipendekeza kwa mabebeluu.
 

Udhaifu wa bunge ni hivyo kushindwa kuhoji wanayoletewa na serikali wanageuka rubber stamp. Hii maana yake ni kuwa azma ya Jiwe ya kuongeza ukomo wa madaraka kama alivyotudokeza Ndugai itapita tu
 
Ingekuwa vizuri, akawambia hata atakapotoa pesa ya kuyafanya hayo anayowaahidi.
 
Nzi wa kijani watabisha weee. Ila siku yakitimia, Hataonekana hata mmoja kwenye huu uzi.
 
Katiba tutaibadilisha sisi wananchi ili awe president wa milele...

Na ni haki yetu kutoa maoni

Viva JPM
 
Amekurupuka angesubiri 2025, kwa sasa ajipange upya kujenga chama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…