Ndugu zangu,
Tulianza kwa kuonya tangu mwaka 2019 ambapo Tundu Lissu alipita kwenye media za kimataifa kumwaga sumu dhidi ya Tanzania na watawala wake kuwa ajiandae, aepuke kuzungumza hoja za jumlajumla zisizo na uthibitisho.
Mwezi January 2019 Tundu Lissu alipata fursa ya kuzungumza katika kipindi cha "Hardtalk" kinachorushwa na runinga ya BBC nchini Uingereza. Matokeo ya mahojiano yalimwacha Tundu Lissu hoi kwani alishindwa kuthibitisha madai yake. Na Stephen Suckur alimueleza kinaga ubaga kuwa "kama wewe ni mwanasheria kwanini unapenda kuongea mambo yasiyo na uthibitisho" hii ilikuwa ni nyundo ya utosini kwani Tundu Lissu alishindwa vibaya na hata wafuasi wake pia walionekana wanyonge kutokana ya matokeo ya mahojiano hayo.
Ajizi nyumba ya njaa, Jana tarehe 31.03.2021 huku Tundu Lissu na Chadema wakiwa wametahadharishwa kuzingatia weledi kwenye mahojiano hayo mambo yakaenda tena arijojo.
Mkenya PLO Lumumba alionekana kumjua vema Tundu Lissu na hata kuijua Tanzania zaidi ya Tundu Lissu. Kama kawaida alianza "lopolopo" kwa kuponda kila lilifanyika nchini huku akitaka kuaminisha ulimwengu kuwa Chato imejengeka kuliko Dar. Zaidi alienda mbali kwa kutoa taarifa za uongo kuhusisha hospitali za Kenya na matibabu ya Marehemu Rais Magufuli bila kuzingatia kuwa taarifa hizo zilishakanushwa na taasisi hizo.
Mbaya zaidi akaenda mbali
kumzushia kifo mlinzi wa aliyekuwa Rais wa JMT Marehemu Magufuli (RIP), anaongea haya macho yakiwa makavu huku siku chache zilizopita mlizi huyo alionekana kwenye runinga katika shughuli za msiba na maziko ya Rais JPM.
Zaidi akaenda mbali kumuita mlinzi huyo "dark person" hii ni kauli ya kibaguzi (xenophobic).Kwa hadhi ya Tundu Lissu kutumia kauli kama "dark person" kama alama ya utambuzi wa mtu inaonyesha jinsi gani ambavyo hafai kuwa kiongozi.
Baada ya mahojiano yote haya wafuasi wa Lissu na baadhi ya wafuasi wa Chadema wameanza kumdhihaki na kumtukana Prof.PLO (Lumumba) eti "kwanini kaenda kwenye usaili huo" kibaya zaidi "wanamwogesha" matusi ya kila aina.
Itoshe tu kusema kwenye hili tusiwalaumu Suckur wala Lumumba mngefanyia kazi udhaifu wa Tundu Lissu hususana tabia ya jazba na "lopolopo", ajifunze kutuliza akili la sivyo mtaanza kuzitukana media zote.
Nawasilisha!