...samahani dada. Nilisahau kuwa huwa mnafundishwa kukariri.
Mwalimu alisema UMMA wa WAZANZIBAR wakisema wanataka bila USHAWISHI TOKA NJE.. na sio WANASIASA wa ZANZIBAR wakitaka na USHAWISHI TOKA NJE...
Ugumu wa lugha kuelewa uko wapi hapo...
Huyo Tundu Lissu alikuwepo wakati baraza la Mapinduzi walipokataa hoja ya Jumbe? anajua kwamba Jumbe tayari alikuwa anataka kutoroka nchini kwenda.. na akanyang'anywa passport, treason maana yake nini? Kama Serikali ya Mapinduzi ambayo ndiyo iliungana na TANU wamekataa na kutaka akamatwe, Nyerere angefanya nini kuwalazimisha? Na kwa nini basi walimchagua Mwinyi baada yake wasifanye vikao ama maandamano kumpinga Nyerere!Tundu Lissu anadai, Mwl. Nyerere hakukataa hoja ya Muungano kwa sababu safi kabisa, bali aliwaweka kizuizini wale waliohoji Muungano. Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uwongo na hakuweza kusema kweli.
Chanzo - Post #1
Huyo Tundu Lissu alikuwepo wakati baraza la Mapinduzi walipokataa hoja ya Jumbe? anajua kwamba Jumbe tayari alikuwa anataka kutoroka nchini kwenda.. na akanyang'anywa passport, treason maana yake nini? Kama Serikali ya Mapinduzi ambayo ndiyo iliungana na TANU wamekataa na kutaka akamatwe, Nyerere angefanya nini kuwalazimisha? Na kwa nini basi walimchagua Mwinyi baada yake wasifanye vikao ama maandamano kumpinga Nyerere!
Tundu Lissu ni mpayukaji hana hekima zaidi ya kufundishwa kubishana maana ndio kazi ya mawakili..
Sio tu kupoteza muda ni ukosefu wa nidhamu, jeuri na Ulimbukeni.. alistahili kuwajibishwa na Chadema kwanza kabla ya yote!Kwanini Tundu Lissu hakujitia uchizi na kutamka haya maneno kabla Mzee hajafariki. Kutoa lugha kama hizi wakati mlengwa ameshakuwa mfu ni sawa na kupoteza muda na pumzi zako.
Lissu omba radhi. Kumtukana Nyerere ni kuwatukana watanzania
Kwa heshima na taadhima bibie futa maneno haya kwa sababu swala la UAMSHO limezingatia Uislaam dhidi ya Ukristu na sii haki wala njia nzuri ya kuomba kujitenga, ila ina ushawishi ambao sio tu kwamba hawa wanataka kujitenga isipokuwa kuzalisha fitna. na ya Masheikh hata bara wametendewa hayo toka kina Sheikh Kassim bin Juma kwa madai ya Bakwata tu, Rais alikuwa Mwinyi Muislaam na Mzanzibar! Nyerere alihusikaje? haya ya Ponda rais nani? naye tusubirie yalomkuta huko. Lakini bado wapo watu wanataka kumhusisha Nyerere kwa kila kitu, we do have the facts..Wapinge walawitiwe? hivi hujui jinsi Wazanzibari wanaopinga wanafanywa nini? mpaka leo hii uamsho hata Zanzibar hawafungwi wala hawahukumiwi kwa "makosa" wanayoyafanya Zanzibar, tumeona Masheikh na wengineo juzi tu wakiletwa kuhukumiwa bara kwa "makosa" ya Zanzibar, mpaka wanalalamika kulawitiwa. Huyajuwi hayo?
Ukimuona Mzanzibari kaamuwa kusema ukweli ujuwe kishajitoa mhanga huyo. Kama kulawitiwa haya, kama kufa haya.
Nilipokwenda Canada, hata CUF ilikuwa haijukani, nimeondoka kwa njaa kweli iliyokuwepo Tanzania, hapo mwalim wako analijuwa hilo na hajakosea.
Hata sukari ilikuwa foleni, kama si njaa nini hicho.
Tundu Lisuu anasema kuwa "matatizo ya kiutawala toka mwaka wa 62 mpaka leo hii ni ya mwalimu".
Canada hii hii ya makafiri?
Canada hii hii ya makafiri?
Kwa heshima na taadhima bibie futa maneno haya kwa sababu swala la UAMSHO limezingatia Uislaam dhidi ya Ukristu na sii haki wala njia nzuri ya kuomba kujitenga, ila ina ushawishi ambao sio tu kwamba hawa wanataka kujitenga isipokuwa kuzalisha fitna. na ya Masheikh hata bara wametendewa hayo toka kina Sheikh Kassim bin Juma kwa madai ya Bakwata tu, Rais alikuwa Mwinyi Muislaam na Mzanzibar! Nyerere alihusikaje? haya ya Ponda rais nani? naye tusubirie yalomkuta huko. Lakini bado wapo watu wanataka kumhusisha Nyerere kwa kila kitu, we do have the facts..
Swala la Jumbe nalijua vizuri sana na nashukuru Mungu mimi sii msahaulifu. Jumbe sii tu alokwenda kinyume cha Baraza la Mapinduzi toka nyuma kama unakumbuka kina HH na AB. Huyu Salim ni majuzi tu baada ya ukali wa BLM kupunguza makali lakini zamani alikuwa wanted na kina Babu, BLM walikuwa hawachezi na mtu. Nyerere kawaokoa wengi ambao kama wangepelekwa Zanzibar basi leo wasingekuwa hai. Leo watu mnasahau kwamba Zanzibar ilifanyiwa Mapinduzi na dhana ya utawala huo una nguvu kubwa hadi kesho.
Maswala mengi watu wanamsema Nyerere lakini wanashindwa kuelewa kwamba wakati ule Usalama wa Taifa ulikuwa sii mchezo wala sii kitu cha kuchezea na haswa Zanzibar. Ukipingana na AfroShiraz maamuzi wanayo baraza la Mapinduzi wala sio makamu wa rais au rais wa Zanzibar. Vikao vya BLM ndio vilikuwa na maamuzi yote na Nyerere ni mtekelezaji tu tena aidha awakimbizie Bara au akubali yaishe. Hata swala la katiba Mpya tujiulize kwa nini wajumbe wa CCM Zanzibar (BLM) hawataki serikali 3? kwa nini hawakuwa pamoja na UKAWA ikiwa kweli wanataka kujitenga kwani Nyerere bado yupo?
Wapinge walawitiwe? hivi hujui jinsi Wazanzibari wanaopinga wanafanywa nini?
Katika mwendelezo wa kupinga mawazo na mfumo wa utawala wa Mwl. Nyerere. Tundu Lissu amepasua jibu ambalo wengi huwa wanaogopa kulipasua pale aliposema kuwa Mwl. Nyerere alikuwa ni "msanii wa kisiasa" kwa sababu aliyokuwa anayasema siyo yale aliyokuwa anayatenda kuhusiana na suala la Muungano. Haya ameyabainisha wakati akitoa hoja kwenye Bunge Maalum.
Mh. Tundu Lissu ameenda mbali na kusema, Mwl. Nyerere alizoea vya halamu na vya halali hakuviweza. Katika kuthibitisha maneno yake, Mh. Tundu Lissu alisema, mwaka 1968, Mwl. Nyerere aliudanganya ulimwengu pale aliposema kupitia gazeti la Observer la UK, Iwapo umma wa Zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa Muungano una hasara kwa uhai wao, sitawapiga mabomu kuwalazimisha......Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea iwapo washiriki wake wataamua kutathmini na kuthibitisha jambo hasa tukio la kihistoria kama Muungano'.
Mwaka 1984, Wazinzibari walipohoji Muungano, Alhaji Aboud Jumbe akafukuzwa kazi kwa amri ya Mwl. Nyerere na amewekwa kizuizini Mjimwema mpaka leo. Wolfgang Dourado akawekwa kizuizini, Bashiri Swanzy akapakiwa kwenye ndege ya kwanza akapelekwa Ghana.
Mh. Tundu Lissu aliendelea kusema, kwa vile Mwl. Nyerere alizoea vya kunyonga, kwenye Kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Mwl Nyerere alisema, 'huko nyuma baadhi ya viongozi wapinzani wa Muungano wameishawahi kusema tufanye referendum kwa Zanzibar kuhusu Muungano, tukakataa kwa sababu safi kabisa'.
Tundu Lissu anadai, Mwl. Nyerere hakukataa hoja ya Muungano kwa sababu safi kabisa, bali aliwaweka kizuizini wale waliohoji Muungano. Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uwongo na hakuweza kusema kweli.
Kitu muhimu kabisa cha kujiuliza na kufikiria. Kama kweli Mwl. Nyerere alikuwa anaishi kwa uwongo na udanganyifu, ina maana hata hati ya Muungano haipo na kama haipo, ina maana amewaingizwa 'mkenge' wananchi na hasa wanaCCM kwa kusimamia hoja ambayo kiuhalisia haipo. (Muungano wa serikali mbili).
Tukikubaliana na hoja ya Tundu Lissu, inabidi tujiulize, Kwa nini Baba wa Taifa alikuwa anaishi maisha ya uwongo na udanganyifu?. Alikuwa anafanya hivyo kwa manufaa ya nani?.
Kama hoja ya Tundu Lissu ni kweli basi hatuna budi kusema, kweli uwongo hupanda lifti wakati ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa!.
Hoja hii inanipeleka kwenye angalizo la sababu ya baadhi ya wajumbe wakiongozwa na Leticia Nyerere kushauri bunge kwa nguvu zote liweke mipaka kwenye kanuni za bunge zikiwataka wabunge kutowadharirisha waasisi wa Muungano. Kumbe nyuma ya hoja zao walikuwa wanaogopa ukweli usijulikane!.
Mpaka katiba mpya ipatikane, tutaona na kusikia mengi!.
Kauli mbiu ni serikali moja au kila nchi ichukue fito zake kwa sababu watu tuliowatuma kwenda kumalizia mchakato wa katiba kwa sasa wanahoji uharali wa Muungano huku wakitaka mpaka makaratasi yenye sahihi za waasisi wa Muungano. Hawa wabunge wameshindwa kufanya kazi ya kumalizia mchakato wa Katiba badala yake wanaanza kuuliza kama Muungano ni halali au batili. Yaani baada ya Miaka karibia 50 ndiyo tunaanza kuuliza Muungano kama ni halali huku waasisi wa Muungano tukiwasema ni waongo na wadanganyifu.
Ninadhani kuna kitu hakiko sawa kwenye baadhi ya hoja za Wabunge!.
[video=youtube_share;bB7BxxMepR8]http://youtu.be/bB7BxxMepR8[/video]
[video=youtube_share;jE7oTPXtpas]http://youtu.be/jE7oTPXtpas[/video]