Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Katika mwendelezo wa kupinga mawazo na mfumo wa utawala wa Mwl. Nyerere. Tundu Lissu amepasua jibu ambalo wengi huwa wanaogopa kulipasua pale aliposema kuwa Mwl. Nyerere alikuwa ni "msanii wa kisiasa" kwa sababu aliyokuwa anayasema siyo yale aliyokuwa anayatenda kuhusiana na suala la Muungano. Haya ameyabainisha wakati akitoa hoja kwenye Bunge Maalum.

Mh. Tundu Lissu ameenda mbali na kusema, Mwl. Nyerere alizoea vya halamu na vya halali hakuviweza. Katika kuthibitisha maneno yake, Mh. Tundu Lissu alisema, mwaka 1968, Mwl. Nyerere aliudanganya ulimwengu pale aliposema kupitia gazeti la Observer la UK, “Iwapo umma wa Zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa Muungano una hasara kwa uhai wao, sitawapiga mabomu kuwalazimisha......Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea iwapo washiriki wake wataamua kutathmini na kuthibitisha jambo hasa tukio la kihistoria kama Muungano'.

Mwaka 1984, Wazinzibari walipohoji Muungano, Alhaji Aboud Jumbe akafukuzwa kazi kwa amri ya Mwl. Nyerere na amewekwa kizuizini Mjimwema mpaka leo. Wolfgang Dourado akawekwa kizuizini, Bashiri Swanzy akapakiwa kwenye ndege ya kwanza akapelekwa Ghana.

Mh. Tundu Lissu aliendelea kusema, kwa vile Mwl. Nyerere alizoea vya kunyonga, kwenye Kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Mwl Nyerere alisema, 'huko nyuma baadhi ya viongozi wapinzani wa Muungano wameishawahi kusema tufanye referendum kwa Zanzibar kuhusu Muungano, tukakataa kwa sababu safi kabisa'.

Tundu Lissu anadai, Mwl. Nyerere hakukataa hoja ya Muungano kwa sababu safi kabisa, bali aliwaweka kizuizini wale waliohoji Muungano. Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uwongo na hakuweza kusema kweli.

Kitu muhimu kabisa cha kujiuliza na kufikiria. Kama kweli Mwl. Nyerere alikuwa anaishi kwa uwongo na udanganyifu, ina maana hata hati ya Muungano haipo na kama haipo, ina maana amewaingizwa 'mkenge' wananchi na hasa wanaCCM kwa kusimamia hoja ambayo kiuhalisia haipo. (Muungano wa serikali mbili).

Tukikubaliana na hoja ya Tundu Lissu, inabidi tujiulize, Kwa nini Baba wa Taifa alikuwa anaishi maisha ya uwongo na udanganyifu?. Alikuwa anafanya hivyo kwa manufaa ya nani?.

Kama hoja ya Tundu Lissu ni kweli basi hatuna budi kusema, kweli uwongo hupanda lifti wakati ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa!.

Hoja hii inanipeleka kwenye angalizo la sababu ya baadhi ya wajumbe wakiongozwa na Leticia Nyerere kushauri bunge kwa nguvu zote liweke mipaka kwenye kanuni za bunge zikiwataka wabunge kutowadharirisha waasisi wa Muungano. Kumbe nyuma ya hoja zao walikuwa wanaogopa ukweli usijulikane!.

Mpaka katiba mpya ipatikane, tutaona na kusikia mengi!.

Kauli mbiu ni serikali moja au kila nchi ichukue fito zake kwa sababu watu tuliowatuma kwenda kumalizia mchakato wa katiba kwa sasa wanahoji uharali wa Muungano huku wakitaka mpaka makaratasi yenye sahihi za waasisi wa Muungano. Hawa wabunge wameshindwa kufanya kazi ya kumalizia mchakato wa Katiba badala yake wanaanza kuuliza kama Muungano ni halali au batili. Yaani baada ya Miaka karibia 50 ndiyo tunaanza kuuliza Muungano kama ni halali huku waasisi wa Muungano tukiwasema ni waongo na wadanganyifu.

Ninadhani kuna kitu hakiko sawa kwenye baadhi ya hoja za Wabunge!.
[video=youtube_share;bB7BxxMepR8]http://youtu.be/bB7BxxMepR8[/video]
[video=youtube_share;jE7oTPXtpas]http://youtu.be/jE7oTPXtpas[/video]

Kumtukuza nyerere ni maamuzi na kumkosoa ni utashi
 
FaizaFoxy,

Wewe wafuata maneno ya Mohamed Said, hapa kafika na anajua. Muulize hao alowataja hawakuwa na mpango wa kuipindua nchi kwa udini? na aloitonya serikali ni Sheikh Kassim Bin Juma wakati Nyerere akiwa ktk mkutano Arusha.. Muulize kama yeye ni msema kweli akane maneno haya.

Hao babu huna cha kuniambia, namjuwa mmoja mmoja, Mohamed Said kaandika, watu walikuwepo.

Wampindue? kwa lipi zaidi?

Unamjuwa aliyemwokoa Nyerere wakati tayari alishapinduliwa na telegram ilishatumwa Umoja wa Mataifa kwa U Thant?

Sidhani kama utayaelewa hayo.
 
Mkandara,

Kwanza nashukuru kuwa yule MKANDARA wetu JF amerudi tena. Umeshusha point nyingi na maswali mengi ambayo FF usitegemee atakujibu. Atatafuta kipande tu cha kutokea na akujibu, mengine yote atayakimbia kama ukoma na kujifanya hakuliona hilo. Kwamba kuna watu wamenyanyaswa wakati wa Mwinyi na Kikwete, hilo yeye halioni. Atalazimisha kuwa Nyerere hadi leo bado mzimu wake unatawala, kisa tu Tundu Lissu kasema "katiba ya Nyerere ya mwaka 1962 bado inatumia." Ni mpotoshaji ambaye anajua kabisa ni nini anakitenda.

Mie leo nilisikiliza mahojiano ya Tundu Lissu kwenye Mkasi na kukuta kama nilivyoandika, kachukua kipande tu na kuondoa neno muhimu sana katikati na akampandikiza hiyo sentesi Tundu Lissu.

Huyu Mdada ni mtu hatari sana ku-deal naye na nisingelishangaa kuwa alikuwa Canada kama Usalama wa Taifa na hata hapa yupo kikazi zaidi. Watakuwa ni wale mafisadi ambao wanaona mkate wao unatiwa chumvi kila siku. Wanamchukia Nyerere kwa sababu aliweka Azimio la Arusha na wakashindwa kuiba.

Mhhh, ngoja niishie hapa maana Cybercrime laws around the corner.

Porojo ndefu zisizo na maana yanini kuzijibu?

Najibu hoja sijibu porojo - kumbuka hilo.
 
Tundulisi hana tofauti na hitila.the guy is poison his ability to deceive cdm followers is like what hitila deed to his follower. Take care CDM followers
 
nyerere mwenyewe alishawahi kusema kua awamu yake ilifanya mema na ya kijinga na akawaomba watanzania wafuate yale mema tu,, anapowashindia watu weng ni ile kwamba alikufa masikin kama mimi kitu kinachodhihirisha ile hoja ya kwamba hata hayo mabaya aliyofanya ilikuwa ni katika kulinda maslahi mapana ya nchi. nyerere hakua mjinga hizi hoja zote zinazokua risen leo alishazipatia majibu ya msingi zaman sana. huyu tundu lissu ni mpumbavu, ni limbukeni najiskia kumdharau sana
 
Hao babu huna cha kuniambia, namjuwa mmoja mmoja, Mohamed Said kaandika, watu walikuwepo.

Wampindue? kwa lipi zaidi?

Unamjuwa aliyemwokoa Nyerere wakati tayari alishapinduliwa na telegram ilishatumwa Umoja wa Mataifa kwa U Thant?

Sidhani kama utayaelewa hayo.
Unajua mwanzo sikukusoma vizuri ila nimerudi nyuma na kukusoma na nadhani wewe unachanganya vitu kati ya chama cha Waislaam AMNUT na Jumiya ya waislaam EAMWS maana haya mambo yametokea wakati tofauti. Pengine wasema kweli maana mimi katika historia ya Tanganyika sikuwahi kusikia AMNUT walifanikiwa kufanya mapinduzi na ajabu limeorodheshwa hata jina la AbdulWahid katibu wa TANU ati naye alitiwa ndani. Hii habari kidogo ina mushker maana ingekuwa tukio la kihistoria na wengi wetu tungelijua. By the way, niko close sana na Familia ya AbdulWahid na ndio maana nasema haya.

Sasa mimi nitatoa Ushahidi hapa juu ya Nyerere kuwa na Waislaam hadi 1968 kabla ya kuvunjika kwa EAMWS na baada ya kugunduliwa njama nilizoandika mimi hapo juu ndio yakawakuta. Sasa basi nakuomba bofya HAPA, kisha shuka chini hadi ukurasa wa 25, Utaona Picha ya Nyerere akimpokea Sheikh Hassn Bin Amir mwaka 1968 na nyingine wamekaa pamoja kisha unambie hawa viongozi wa Kiislaam waliweza vipi kukaa kiti kimoja na Nyerere baada ya kufanyiwa yote yale uloyataja?
Tusiendelee kubishana pasipo ushahidi..
 
Wewe unamjuwa Nyerere au unamsikia tu?

Nimekuuliza swali juu huko, Jee, unamjuwa aliyemuokoa Nyerere alipopinduliwa na wanajeshi Tarehe 20?

Sasa hao unaosema wewe uko karibu nao waulize kama watakupa jibu.
 
Imekuwa wanajeshi tena duuuh mwanamke wewe mbona hueleweki. Sasa imekuwa tena tunazungumzia walimuokoa Nyerere ama tunazungumzia Waislaam ambao Nyerere alowaweka ndani? yale ya Jeshi yabakie ya jeshi tunazungumzia ya Waislaam kama ulivyodai. Usipindishe hoja..
 
Si unaona, hata huelewi kuwa Nyerere alipinduliwa na wanajeshi na Waislam wakamuokoa, Jee unawajuwa ni akina nani?

Uko finyu sana, hivyo vijukuu vya akina Skes haviyajuwi hayo kwa hiyo hata ukiwauliza kazi bure tu.

Labda umuombe Alama Mohamed Said akusaidie, mimi sikufungulii, ntakuwacha na duku duku mpaka ujuwe kuwa uyajuwayo wewe ni ya kubabiababia tu.
 
CHA MOTO TUNACHOKIONA HIKI WAISLAM,NI MSINGI ULIOJENGWA NA NYERERE.Kuuwa TANGA,TABORA,LINDI,UJIJI nk,dah!haki ipo kwa MUNGU.
 
Si unaona, hata huelewi kuwa Nyerere alipindiliwa na wanajeshi na Waislam wakamuokoa, Jee unawajuwa ni akina nani?

Uko finyu sana, hivyo vijukuu vya akina Skes haviyajuwi hayo kwa hiyo hata ukiwauliza kazi bure tu.

Labda umuombe Alama Mohamed Said akusaidie, mimi sikufungulii, ntakuwacha na duku duku mpaka ujuwe kuwa uyajuwayo wewe ni ya kubabiababia tu.
Alaa ebu rudi nyuma ukasoma uloyaandika huko mwanzo maana ndiyo tulokuwa tukijadiliana na sii ya maasi ya Wanajeshi Nyerere akaokolewa na Waislaam. Wewe umesema Waislaam walimpindua Nyerere baada ya Uhuru, wengine wakasweka ndani hata AbdulWahid ndio nikapinga. Ukasogeza mbele sasa imekuwa maasi ya wanajeshi ya mwaka 1964, waislaam ndio hero! na bado utasogeza tena kwenda 1968 bila shaka.

[SIZE=+2]Alichokifanya Nyerere baada ya uhuru[/SIZE]
Kilichofuata baada ya kupatikana uhuru ilikuwa ni kukamatwa, kuwekwa kizuizini na kuhamishwa kwa masheikh na Waislamu wengine waliodhaniwa kuwa wanapinga utawala wa Nyerere.
 
Alaa ebu rudi nyuma ukasoma uloyaandika huko mwanzo maana ndiyo tulokuwa tukijadiliana na sii ya maasi ya Wanajeshi Nyerere akaokolewa na Waislaam. Wewe umesema Waislaam walimpindua Nyerere baada ya Uhuru, wengine wakasweka ndani hata AbdulWahid ndio nikapinga. Ukasogeza mbele sasa imekuwa maasi ya wanajeshi ya mwaka 1964, waislaam ndio hero! na bado utasogeza tena kwenda 1968 bila shaka.

Hapana sikusema Waislam walimpindua Nyerere baada ya Uhuru, wapi nimesema hayo? tafadhali usinizulie na usijaribu kutia maneno yako kinywani mwangu.

Hao Masheikh nimekuwekea hiyo link kukuonesha walitiwa ndani na Nyerere baada ya Uhuru, wewe ulisema walitiwa ndani wakati wa Mwinyi, mimi nikakuonesha kuwa Nyerere ndiye aliyewatia ndanoiwengi zaidi na Mwinyi kama kawatia ndani na yeye si alikuwa kikaragosi tu cha Nyerere.
 
Viongozi wangu
Raisi: A.lipumba
Makamu: mbowe
Waziri mkuu: zitto kabwe
Mwanasheria mkuu: tundu lisu

ASANTE TUNDU LISU KWA KUTHUBUTU KUSEMA UKWELI.
sema ukweli hata kama itawama
 
adui wa nyerere mzee mtei atakuwa alimtuma tundu lisu amtukane nyerere

Inaonekana watu wanapenda sana kudanganywa.uongo ni uongo tu haijalishi kadanganya nani mkuu!

Usitake kusema uongo wa nyerere ni ukweli kwa umma...
Utakua kama wale wanaosema,UPUMBAVU WA MUNGU NDIO AKILI ZETU!
sema tu yeye ni binadamu,aweza kukosea kubinadamu,nasi tulioona kosa tusahihishe!
 
nyerere mwenyewe alishawahi kusema kua awamu yake ilifanya mema na ya kijinga na akawaomba watanzania wafuate yale mema tu,, anapowashindia watu weng ni ile kwamba alikufa masikin kama mimi kitu kinachodhihirisha ile hoja ya kwamba hata hayo mabaya aliyofanya ilikuwa ni katika kulinda maslahi mapana ya nchi. nyerere hakua mjinga hizi hoja zote zinazokua risen leo alishazipatia majibu ya msingi zaman sana. huyu tundu lissu ni mpumbavu, ni limbukeni najiskia kumdharau sana

Tundu Lissu anadhani ataufuta Umaarufu wa Nyerere uhamie kwake? Kila kukicha anatafuta wafuasi wa kumwunga mkono ili wafute yote aliyofanya Nyerere. Kwa hilo anapoteza muda wake atafute kitu kingine cha kufanya. Ngoja tumtonye ili aache kuhangaika. KTY tunajua sana mapungufu madogo madogo aliyokuwanayo Nyerere lakini tukishapima na kugundua kuwa yote aliyafanya kwa maslahi mapana ya walio wengi tunabaki kumsifia kuwa alikuwa JEMADARI. Kajinyonge ikiwa hilo litakukera.
 
Tundu Lissu ni smart lawyer na very good mwanaharakati but he is a lousy politician....huwezi mtukana Nyerere na isi ku cost

HajamtukanA boss! Ila kaeleza ukweli jinsi nyerere alivyoendesha mambo ya muhimu kijanjakijanja.
Sema ni kweli watamuandama....KWA KUWA UKWELI KWA ASILI YAKE UNAUMA.
Ila tunahitaji wanasiasa wengine wasio waoga kama tundu lisu.na sio kumtia hofu na kumvunja moyo.
Jua maisha tunayoishi yanatokana na misingi iliyowekwa na viongozi wa awali wa kiserikali wa nchi.
Ni kweli nyerere ana mazuri yake,ila kama kuna sehemu alikosea ndio asiambiwe??
Tutarekebisha vipi makosa kama tusipojua wapi walikosea waliotangulia?
KIP IT UP T.LISU
 
nyerere ndio role model wa dr.slaa, mbowe , yericko nyerere,bensaanane halafu tundu lisu anamtukana.. lisu hana adabu kwa viongozi wake wa chama

Kwa iyo hata uwongo WAIGE???
Mazuri yake wataiga mabaya wataachana nayo.
Msimfanye nyerere kuwa alikuwa PERFECT!!
 
Back
Top Bottom