Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

adui wa nyerere mzee mtei atakuwa alimtuma tundu lisu amtukane nyerere

Na bado kijana we subiria tu jumatatu atakapopewa fursa nyingine ya kuongea ndo utajua kuwa alikuwa anamtukana au alikuwa anamkosoa kwa madudu aliyoyafanya ya muungano huu usio hata na udhibitisho wa hati..
keeeep on, tukutane jumatatu tatu kamili..
 
katka mahojiano mengi ya Tundu Lissu anaonyesha kama ana chuki binafsi na mwalimu Nyerere,Nakubali Mw. Kama mwanadamu yeyote alikuwa na mapungufu fulani lakini chuku za Tundu lissu zimevuka mpaka angeweza kutumia lugha ya kistaarabu kuonyesha mapungufu yake ,lakini pia nimewahi kusoma mahojiano yake ya nyuma kwenye gazeti la ----------- pia alikuwa akimshambulia Mw.wakati mtu anayemshambulia ndie aliweka mazingira ambayo mtu wa kawaida kama yeye aliweza kusoma na kufika hapo alipo.
Jumbe hakuwekwa kizuizini sababu ya kuleta serikali tatu bali kwa kuvunja katiba ya jamhuri ya muungano ambayo leo hii wakina Tundu Lissu wanaqlalamikia juu ya mabadiliko ya Zanzibar kuwa yamevunja Muungano kwa hilo amuulize Seif Sharif Hamad kwani ni miongoni mwa watu walioleta vielelezo vya kuonyesha jinsi gani Jumbe alikuwa akifanya mambo kinyume cha katiba lakini kama anaona Jumbe alionewa kwanini Tundu Lissu alishiriki kuwashambulia kina Zitto Kabwe kuwa walikuwa wanataka kumuondoa Mbowe kinyume cha taratibu angewaacha maana isiwe haramu kwa mwenzako ila ikiwa kwako iwe halali
 
Nakubaliana na maoni yako kwasababu Mwl. Nyerere ameondoka madarakani miaka 28 iliyopita. Watawala waliofuata licha ya kuhufamu upungufu na makosa yaliyo fanyika wakati wa kuunganisha nchi zetu walishindwa kurekebisha makosa. Hata wakati huu ambako wamepata fursa nzuri kuyarekebisha wanagoma na kuja na stori za kisiasa.

Binafsi ni mkereketwa wa siasa za Mwl. Nyerere lakini kwa kusoma hotuba ya Lissu na vielelezo ni dhahiri shairi mambo hayakuwa sawa ktk kuunganisha nchi zetu na hata baada ya kuungana haikufanyika juhudi ya kurekebisha mapungufu. Hii kitu licha ya nia yake njema kabisa haikua sawa!

Tume nyingi ziliundwa kufikia hii ya Jaji Warioba. Wote waliliona hili kwamba limekaa vibaya lakini Watawala wakakataa ushauri. Mpaka jana Lissu akatema nyongo ambayo kwa propaganda rahisi wana CCM watasema amemkosea heshima Mwalimu Nyerere lakini kiukweli wao walioshindwa kurekebisha makosa ndiyo wamesababisha sasa sisi wote tukajua nini tulifichwa!

Tunako endea tutasikia wajumbe wakitaka kujua kina nani walimuuwa Karume na walimuuwa kwa nini na walichukuliwa hatua gani au kwa nini hawakuchukuliwa hatua.hayo yote nikatika hayoyasema.
 
katika academic arguments sio lazima uandike kitu unachokiamini - hata theology nayo haiko hivyo!!
 
lissu ni kichwa, na kwenye suala la Muungano anaujua vizuri sana na cxcm wanajua, ndio maana akiongea anaoneshwa kichwa kingine cha Tanganyika Mh Mtikila akitabasamu kabla TBCCM kukata matangazo kwa kisingizio cha kitoto cha hali ya hewa, na kuweka hotuba ya JK. hongera TL kwa elimu uliyokuwa unatupa, si ya yule Dr mwenye mawazo mgando.
 
hapo nyerere anatukanwa au anaambuwa ukwel....na yeye ni nan hasa mpaka akikosea asiambiwe? ni vitu vingap vya kipuuz kafanya nyerere mpaka leo watu wanalumbana na kaishakufa..ni viongoz wangap wabov nyerere kaiandalia tanzania hii...hana uspecial wiwote ni mtu kama wewe kama tundu lisu..akizingua anapewa black and white

escherencounter.jpg
 
wanatukanwa mitume na manabii...sembuse huyo aliekuja mjini na kaptura mpaka the bank Dossa Aziz alipomtunuku Suruali ili ajistiri, lakini bado alikuwa anazikunja mpaka mapajani...

Wacha maneno yako wewee

Duh kweli laana imefika hapa nimeona hata mwana ccm akimsifia mama wa huyu jamaa kuwa ni mtu mwema atakana tu hata kama ndio ukwel
 
Tundu Lissu alifata ushauri wangu nilioutoa humu JF 14th April 2014, wiki iliyopita:

Ha ha ha FaizaFoxy, umenifurahisha sana. 14th April 2014 ni kesho sio wiki iliyopita.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Tuache uoga , Nyerere alikuwa mnaffiki , m binafsi , na jeuri .!
 
Duh kweli laana imefika hapa nimeona hata mwana ccm akimsifia mama wa huyu jamaa kuwa ni mtu mwema atakana tu hata kama ndio ukwel

mwambie SHIFTA enzi zile walimu wlikuwa na style yao ya kuvaa - KAPTULA NA STOCKINGS NDEFU NYEUPE - WAKIFUTIKA PEN NYEUSI NA NYEKUNDU YA KUSAHIHISHIA - NA MAXIMUM DISCIPLINE - Sio siku hizi hajachamba anaingia darasani kufundisha!!
 
Tundu Lissu ni smart lawyer na very good mwanaharakati but he is a lousy politician....huwezi mtukana Nyerere na isi ku cost
Mkuu kama huyu Lissu kweli kamtukana Mwalimu basi maji yako jikoni, he has got it coming!
Hakuna aliyemtusi Mwalimu na hakulipia matamshi yake, amwulize Mtikila aliyepata chumba cha bure Ukonga kwa mwaka mzima.
 
Mimi nipotoshe ili inisaidie nini?.

Mh. Tundu Lissu alianisha mambo manne katika muktadha wa makundi ndani ya CCM na kila jambo lilikuwa na kundi lake. Jambo la nne lilikuwa linamhusu Mwl. Nyerere na siasa za Zanzibar kama nilivyobainisha hapo juu.

Jaribu kuangalia video yake ili upate ukweli na kubainisha vizuri ninachokisema.
Nimeangalia video sijaona Lissu aliposema Nyerere alizoea kuishi kwa uongo, nadhani una ajenda yako ya siri ya kutaka kupotosha aliyoyasema lissu baada ya kuona amewashika pabaya.
 
In the rudimentary annals of political science, there is political expediency and principled stance. This post of yours, inherently, is the classic - if perhaps not entirely conscious- juxtaposition of the politics of convenience versus the politics of conviction.

You seem to put a higher premium on the politics of convenience than the politics of conviction.

Political expediency, at least to me, ranks lower in merit than a principled stance and the pursuit for a semblance of truth. For this reason, following the given context, any cost that Tundu Lissu will incur due to a genuine pursuit - if genuine indeed it is- will be honorable and exalted in my books.

The devil is in the details.

We need a paradigm shift that will humanize Nyerere and examine him critically beyond the calcified lionization of a common folklore.

To me, Nyerere remains a statesman to be afforded the benefit of doubt beyond most Tanzanian leaders, there are valid utilitarian cases to be made to justify his somewhat tyrannical shades. An apologist could almost always resort to the now cliche-like justification for any shortcomings on the human rights front for example, by countering that the man was stitching together a nation out of more than 120 tribes, a Herculean task given the artificiality of the colonial borders.

But to what extent were these perceived abuses of power far and beyond any noble -if dirty- duty?

If Nyerere needed to break a few eggs in order to make an omelette, where is that omelette? Please spare me the "muungano" and "peace and harmony" talk, as that is a given, given our history.

Or is it?

To what extent was Nyerere morally justified in invoking his legal rights to the despicable "indefinite detention" laws in the name of the behemoth monstrosity that is "national security"?

How much of this was a ruse to sustain undemocratic rule and Draconian oppression?

Tundu Lissu is certainly not the most polished lawyer with the gift of suave savoir faire, nevertheless he gives me hope that there is room for discourse in Tanzania, crucial discourse that will leave no sacred cow untouched. Nyerere was surely grappling his way in the dark, charting uncharted waters. Take the Union apart and you will see a unique Frankenstein, the world over. It is inconceivable that he would have emerged from this largely experimental process unscathed by scandal and blame.

To this day, one of my most damning disappointments from Nyerere is the way he helped flip the Zanzibar election. For a Fabian socialist, self professed principled statesman, staunch Catholic and dubious democrat, this contradicted some core principlles that calls to question all of his elections, if not the outcome, at least the margin.

Again, the devil is in the details.

We need some sort of "Freedom of Information" act to declassify the Nyerere Ikulu archives, make them public, at least on a need to know basis for Tanzanians, and dig for a comprehensive look at the man versus the legend.

Mr. Lissu, as an abled and passionate parliamentarian, is the natural choice to champion this move.

Cc: EMT Anheuser

Very soon huyu mtu atakushangaza na kuku dissapoint. Siamini kama ana conviction .mimi namuona ni mwanasiasa ambae anahangaika tu kutafuta pa kusimamia...I hope he proves me wrong.
 
Last edited by a moderator:
Tundu Lissu ni smart lawyer na very good mwanaharakati but he is a lousy politician....huwezi mtukana Nyerere na isi ku cost

kama ni kutukana, SI sawa kwa Nyerere Tu Ila haifai kwa kila binadamu. ILA kukataa kumkosoa Nyerere au mwanadamu mwingine mwenye makosa ni dhambi ya ushiriki.
 
mwambie SHIFTA enzi zile walimu wlikuwa na style yao ya kuvaa - KAPTULA NA STOCKINGS NDEFU NYEUPE - WAKIFUTIKA PEN NYEUSI NA NYEKUNDU YA KUSAHIHISHIA - NA MAXIMUM DISCIPLINE - Sio siku hizi hajachamba anaingia darasani kufundisha!!

kumbe kaptula ndo umbumbu wa Mwl duh huyu jamaa anatakiwa aamke ucngzn
 
Tundu Lissu ni smart lawyer na very good mwanaharakati but he is a lousy politician....huwezi mtukana Nyerere na isi ku cost


hahaha!

mimi pia namuheshimu mwalimu nyerere, lakini natambuwa kuwa hakuwa malaika, na kama kinachosemwa na lissu ni kweli na haki, acha im-cost. mambo yote yatapita lakini ukweli utasimama.
 
Huyu Lissu ni mropokaji, bila Mwalimu Nyerere ajiulize leoangekuwa wapina anafanya nini? Hata afanye nini hawezi kubadili historia ya Mwalimu Nyerere katika Taifa na Dunia kwa ujumla.

wewe una element za ujinga kumukichwa.
nikwambie, katika vitu alivyokosea nyerere ni pamoja na muungano wa tanganyika na zanzibar, sisi tulio na akili hatuwezi kuendelea kuishi kwenye makosa ya juliasi, mbona azimio lake la arusha hamlipiganii mnang'ang'ania limuungano tu!!!!!!!!! au kwa kuwa limuungano linahusu uongo uliovuka mipaka mpaka UNO come UN.

Hamuyapiganii mashirika aliyoyaanzisha juliasi sijui mmekumbwa na wazimu gani kutuzingua kwenye limuungano.

TAFADHALI TENA TAFADHALINI SANA MSITUAMBUKIZE UJINGA.
 
Tundu Lisu yupo makini sana katika kujibu hoja. Katika mambo mengi amenivutia. Lakini kuna mambo katika hoja yake ya muungano (hoja hii) ninatofautiana naye kwa heshima na upole wote.

Kuhusu Wasomi kuwa na misimamo tofauti na ile waliyoiandika katika maandiko yao tofauti kitambo. Hoja ya kwanza, kuna utofauti kati ya kile ambacho mtaaluma anakifafanua na kile anachokiamini. Kufafanua ni suala la kiuhalisia, kimuundo na kimtindo, wakati kuamini jambo fulani ni suala la dhamira. Ninaweza nikaandika kuwa Muungano uliopo una kasoro, napia nikaandika kuwa wachache wanapenda muungano wenye serikali tatu, lakini mimi binafsi nikawa muumini wa serikali moja au mbili.

Hoya ya pili ni suala la uhuru wa binadamu kubadili misimamo na imani. Hivi ninachokiandika leo na nikakifafanua leo ni lazima nibaki hivyo hivyo kwa miaka kumi au miaka ishirini ijayo hata kama kwa wakati huo mambo yanaonekana tofauti? Lisu, nadhani hakuna binadamu mwenye uhakika kuwa misimamo yake ipo sahihikwa asilimia 100 siku zote. Shivji na mwakyembe wana haki ya kubadili misimamo yao.

Kuhusu Nyerere. Tundu Lisu anasema Nyerere alikataa misimamo ya wazanzibari walipohoji muungano mwaka 1984, nakwamba Jumbe aliwekwa kizuizini hata leo. Tunajuaje kuwa kuhoji muungano lilikuwa ni suala la Jumbe peke yake, aulilikuwa ni suala la wazanzibari wengi? maana nijuavyo mimi kama lilikuwa ni suala la wazanzibari wengi, hata kama wangekuwa robo isingetosha kumzuia Jumbe peke yake. huwezi kuzuia mawazo ya wengi kwa kumzuia mmoja. Naomba kutofautiana na Mheshimiwa Lisu

Pia Nyerere, kwa jinsi nilivyomfuatilia, alikuwa ni mtu wa kufuata fikra huru. sidhai kama alikuwa ni mnafiki kiasi cha kupenda vya kunyonga. Tumpe heshima yake. Naheshimu sana uhuru w Mheshimiwa Tundu Lisu kuweka mawazo yake hadharani, hususan mawazo ya wachache.
 
Back
Top Bottom