Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

wewe una element za ujinga kumukichwa.
nikwambie, katika vitu alivyokosea nyerere ni pamoja na muungano wa tanganyika na zanzibar, sisi tulio na akili hatuwezi kuendelea kuishi kwenye makosa ya juliasi, mbona azimio lake la arusha hamlipiganii mnang'ang'ania limuungano tu!!!!!!!!! au kwa kuwa limuungano linahusu uongo uliovuka mipaka mpaka UNO come UN.

Hamuyapiganii mashirika aliyoyaanzisha juliasi sijui mmekumbwa na wazimu gani kutuzingua kwenye limuungano.

TAFADHALI TENA TAFADHALINI SANA MSITUAMBUKIZE UJINGA.


Kumbe na wewe ni kama yeye.
 
Tundu Lissu, kwenye ili la kumponda Nyerere, pro-Chadema wapo kimya masikini.

Natambua sana mchango wa nyerere kwa nchi, lakin haya anayosema lissu si kumponda liko wazi kwa yeyote anaetaka kujiita mkweli na msomi. Hakuna shaka nyerere alikua m2 kama ww, kukosea ama kufanya jambo kwa utashi binafsi ipo hata kwake. Nikuulize tu swali rahis, Unadhani nani kamponda nyerere kwanza, Prof shivji ktk kitabu chake, au dr mwakyembe ktk iyo paper yake? Kama ni muungwana jibu sahihi unalo
 
Katika hoja yako hii. Je, unakubaliana na Mh. Tundu Lissu anaposema Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu.

Tunaweza kucheza na maneno kwa mitindo kadhaa. Binafsi, sifurahishwi na uwasilishaji hoja wa Lissu; una jazba isiyo na ulazima. Bila shaka hiyo ndiyo hulka yake ambayo si rahisi kutibika katika umri aliofikia. LAKINI ana hoja nzito ambayo ni muhimu kwa yeyote yule anayetaka kuwa mshiriki mzuri wa jukwaa hili. Kwanza, katika masuala ya siasa na uongozi hapa duniani mantiki hairuhusu mtu "kuabudiwa" kama wengine wanavyotaka kuwafanya Nyerere, Sokoine, Mandela, n.k. Ukiisha ingiza "ibada ya binadamu" basi umeshakufuru misingi ya mantiki na hata ya Mwenyenzi Mungu (ambaye pekee anastahili kuabudiwa - kwa imani zetu wengine). NA huwezi kuwa na michango ya maana katika jukwaa hili kama unataka kuabudu binadamu.

Pili, mahsusi kwa Mwalimu Nyerere, tukubaliane kuwa alikuwa mkuu (a great person) ambaye aliyekuwa na picha rasmi (vision) ya nchi yake aliyoitaka yeye kwa malengo mazuri kabisa (hata kama picha hiyo ilikuwa na kasoro). Sio kama wengi waliomfuatia waliokuwa wakiangalia zaidi maslahi mafupi hususan ya mifuko yao na familia na marafiki zao. Ili kutimiza picha aliyokuwa nayo akawa mtu wa mikakati. Ukishakuwa mtu wa mikakati basi tukubaliane si nyakati zote utakuwa mkweli na muwazi. Wakati mwingine mikakati huhusisha ulaghai (kwa nia njema) ili malengo yake hatimaye yafikiwe. Manake lengo la mikakati ni "kuwaweka watu sawa" waendane na mipango yako - ama iwe mizuri ama iwe mibaya. Cha maana katika mikakati ni uzuri wa lengo lako la mwisho.

Wengi tunachomheshimu Nyerere ni kuwa mikakati yake haikuwa ya kujenga taifa la kujinufaisha yeye na familia yake binafsi. Hakuwa na tamaa nzito za kibinadamu za mali na mengineyo. Malengo yake bila shaka yalikuwa mazuri kwa wote na kwa taifa zima. Tatizo kubwa la dhahiri ni kuwa na ubinafsi wa fikra uliokithiri; hakuwa tayari sana kukubali mawazo mbadala ya wengine. Ushahidi wa kukosa subira na mawazo mbadala ni mwingi kuanzia kwenye mitafaruku na akina Kambona, Kassanga Tumbo, Jumbe, Mtei, n.k. Wakati mwingine alikuwa sahihi hasa kwa wale waliokuwa na mipango ya kujikweza kwa elimu na nafasi zao lakini ushahidi unaonyesha pia aliishia kujenga uongozi wa kujikomba sana (bootlickers).

Kwamba aliendesha masuala ya muungano kimkakati sana halina ubishi. Aidha hatuwezi kusema kuwa alikuwa na nia mbaya katika muungano huu. Hakuna ushahidi wa "nia mbaya". Tatizo kubwa ni kuwa alitwisha uongozi wa pande zote maudhui yake pekee na kutosimamia taratibu kamilifu na za wazi katika mchakato mzima wa muungano. Ni kama vile kwake yeye hoja likuwa ni "muungano kwa gharama yoyote ile". Ni dhahiri basi kuwa mahangaiko tunayopata leo (kuanzia wakati wa Jumbe) kuhusu muungano ni matokeo (consequences) za mapungufu ya "mikakati" ya Mwalimu katika mchakato aliousimamia. Ukitaka kuwa mkorofi (usiye na mikakati kabisa) kama Lissu unaweza kumpa vigezo vya "uongo na udanganyifu". Lakini ukiwa mtu mstaarabu huwezi kutumia lugha hiyo kwa Mwalimu; utamchukulia kama mtu aliyekuwa na mikakati dhaifu (upungufu wa kibinadamu!).
 
Ndiyo unapotosha tena unajaribu kumingo akili za watu wamuone lisu mtukutu,

-hukusikiliza wala kuisoma hotuba ya Lisu peke yako,


Jitafakali kwa kutumia hekima sisi sio wapuuzi wakukubaliana na propaganda zako kupindisha maneno nakuchomekea neno Nyerere pasipostahili ilikukidhi malengo yako.
Vip mkuu ni nini kinakuchanganya?
 
acha kupotosha ukweli wewe aliposema kuwa kuna uwongo na udanganyifu alikuwa anamaanisha wana ccm wa hivi leo kama akina HARRISON MWAKYEMBE alipotamka wazi huko nyuma mwaka 1995 katika kitabu chake cha kupatia hiyo Phd aliyonayo huko ujerumani kuwa muungano pekee ambao utaleta usawa zanzibar na bara ni wa serikali tatu tu leo kapewa cheo kageuka

Hivi watu wanaelewa nini maana ya PhD? Yanayoandikwa katika PhD siyo vifungu vya bibllia au aya katika korani. Muda unavyoenda tafiti zaidi zaibuka na vitu ambavyo vilidhaniwa ni kweli wakati huo vinaweza kubadilika. ndiyo maana ya sayansi katika utafiti.

Mtu anaweza kuigeuka hoja yake mwenyewe lakini lazima kuwe na sababu za msingi kufanya hivyo na wanasayansi/watafiti wengine wazione hizo hoja.
 
Lissu omba radhi. Kumtukana Nyerere ni kuwatukana watanzania
Acha kutusemea watanzania na akili zao mfu hizo, Nyerere mwenyewe alikili kwa kinywa chake kuwa kuna mambo mengi tu ya kijinga yalifanywa katika utawala wake sasa wewe unamuona kama mungu wa watanzania wote ?
 
Ukisema dunia nzima utakuwa haujaitendea haki hoja yako.

Nadhani kwa kiwango kikubwa, historia inaonyesha muungano wa nchi mbali mbali zamani ulikuwa mara nyingi wa kisiasa, na siasa mara nyingi zilikuwa zinaendana na nguvu na ubabe.

Kwa sasa imebadilika kwa vile nchi nyingi zinaungana kwa sababu ya kiuchumi ambapo maridhiano yanakuwa ndiyo kiunganishi cha muungano.


1 Kwa kweli inauma mm napenda sana s3 ila sipendi mtu yoyote anaetaka kuvunja muungano wetu huyo tumkabili kwa hali na mali ikibidi tumzibiti hata kwa dola

2 muungano ule liopo duniani lazima ubabe uwepo ndiomana ukienda usa huruhusiwi kuoji muungano wao kwa namna yoyote kwa upole au kwa shari kwa kulinda maslai ya nchi husika na uchumi wake

3 simpendi mtu anaekashifu au kutukana viongozi wetu wote waliojitolea kwa nguvu zao zote kupigania uhuru wa nchi yetu japo na wao walikuwa na makosa yao yakibinadamu lakini si kwa kashfa au tusi siuungwana kwani nae anaeshima na pia na familia yake itajisikiaje kwa kuwakashfu ndugu yao mwenye hadhi ya kitaifa?
 
mi naona Ni vizur kila mtu ajibebe mzigo wake,,,, hawa wa Zanzibar so watu wazuri kabisa wala,,, he mnamfahamu john okello,, mganda aliyepigania mapinduzi ya Zanzibar,,, yeye ndiye chanzo had Zanzibar walisucceed revolution but after revolution,,,,,,,,

Very good point,mara nyingi huwa nasema haya mambo,unakuta kuna wazalendo lukuki waliojitoa kupigania uhuru lakini hawakumbukwi kabisa,ni bonge la usaliti.Utasikia,MANDELA DAY...kwa nini hakuna Oliver wa Katambo day? Our leaders are really betrayers! R.I.P mzalendo wa kweli,komrade John Okello,wewe ni mfano wa kuigwa,kwani ni nani awezaye kujitoa tena na si mzaliwa wa nchi husika?

Back to Topic;niaminicho mimi Nyerere alikuwa na dikteta wa kupindukia kwani alikuwa hataki ushauri katika maamuzi yake hivyo hoja ya kamanda Lissu imeshiba sana.Swali ambalo huwa najiuliza,kama Nyerere hakuma fisadi,alishindwa nini kumwajibisha Mkono pasi na kumruhusu akimbie? Ni wizi mtupu,hakuna mwema chini ya jua.
 
Sikutegemea kwa mtu mzima Kama lisu kumtusi muasisi Wa taifa. Alitakiwa kujenga hoja,na kwa njia ta matusi. Tumesononeka sana sisi watanzania,kauli ya mtusi mwalimu haivumiliki. Ningekuwa mimi ndio mkono Wa dola, ningechukua hatua mathubuti.

Si kila kitu kazima useme, pima tumia hâta busara ya kawaida. Tunamheshimu mwl na bado tunampenda. Amani unayoiona si kwa bahati mbaya. Karibu kujizuia kwa baadhi ya mambo. Huwezi hâta kidogo wewe lisu kujilinganisha na mwl. Linda heshima yako na chama chako. Kila kona wanasema umekosea.

KAzi njema.

----------------------------

Maelezo kutoka kwa Mzee Edwin Mtei

Nilisikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu. Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972. Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.

Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke: Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao. Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!

With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE.


Edwin Mtei
Founder Chairman of CHADEMA.
 
Sikutegemea kwa mtu mzima Kama lisu kumtusi muasisi Wa taifa. Alitakiwa kujenga hoja,na kwa njia ta matusi. Tumesononeka sana sisi watanzania,kauli ya mtusi mwalimu haivumiliki. Ningekuwa mimi ndio mkono Wa dola, ningechukua hatua mathubuti. Si kila kitu kazima useme, pima tumia hâta busara ya kawaida. Tunamheshimu mwl na bado tunampenda. Amani unayoiona si kwa bahati mbaya. Karibu kujizuia kwa baadhi ya mambo. Huwezi hâta kidogo wewe lisu kujilinganisha na mwl. Linda heshima yako na chama chako. Kila kona wanasema umekosea. KAzi njema.
Mkuu sitaki kupinga au kukubaliana na hoja yako mimi ninakusudia hapo kwenye Red
sijui amani hiyo ni kwa kina nani? Maana mimi natembea na Mkongojo kwani nimewekewa
chuma kwenye mguu wangu baada ya vipigo vya polisi, si hivyo tu kuna ndugu yangu ambaye
alikuwa mjamzito pale Mtwara mjini alipigwa risasi na polisi na akapoteza maisha sijui ni
amani gani unaizungumzia?
 
wewe ndo umekosea na wala kujitoa kwako sdm si jambo lolote, kwani unamsujudia huyo mwl ili iweje? amani iliyoko safrica, botswana angola ghana na sehemu zingine kapeleka mwl watu wenye akili finyu km ya kwako ndo wanadhani kuwa wana amani je wafngwa na mahabusu wako kimya wana amani kiasi gani? hauwezi kutofautisha ukimya unaosababishwa na ujinga wa kutojitambua dhidi ya watu wanaojitambua na kudai haki kamanda Lisu oyeee haujakosea kitu chapa mwendo tunakfuatilia.
 
Barabara nyeupe kama ulikuwa chadema bila kujifahamu. Nendwa huko kunakokupasa.
 
AMANI gani unaongelea katika mgodi wa North mara vijana wapatao 300 wameuawa na askari kwa muda wa miaka 10 tu.
 
Kwa hiyo unaishi kwa kumtegemea hayati mwl. Nyerere? Je wewe lini utaenziwa wewe? Hii ni haki yako kikatiba!
 
Sikutegemea kwa mtu mzima Kama lisu kumtusi muasisi Wa taifa. Alitakiwa kujenga hoja,na kwa njia ta matusi. Tumesononeka sana sisi watanzania,kauli ya mtusi mwalimu haivumiliki. Ningekuwa mimi ndio mkono Wa dola, ningechukua hatua mathubuti. Si kila kitu kazima useme, pima tumia hâta busara ya kawaida. Tunamheshimu mwl na bado tunampenda. Amani unayoiona si kwa bahati mbaya. Karibu kujizuia kwa baadhi ya mambo. Huwezi hâta kidogo wewe lisu kujilinganisha na mwl. Linda heshima yako na chama chako. Kila kona wanasema umekosea. KAzi njema.

Mbona wengine tumeona sawa tu.Alichosema Lissu kilitakiwa kusemwa siku nyingi.Inawezekana ni maneno makali tu aliyotumia lakini siwezi kumlaumu Mwalimu sababu inawezekana alikuwa na sababu zake za msingi za kuficha ukweli,na alisema kuwa kuna mengi walikosea kama viongozi hakusema nini walikosea,sasa kama kuna mtu anasema hayo ndiyo alikosea basi tukiri alikosea,hata kama hakusema ukweli kuhusu Muungano basi waache waliotafiti na kuona kilichotokea tusiwahukumu.
 
Back
Top Bottom