1. Lisu kusema kwa ukali na makeke hakutaitisha CCM. CCM ni waovu, hawatishwi na maneno!
2. Mama yuko agressive supreme of power! hatishiwi na maneno makali/kelele za juu kama za Heche na Lisu!
3. Watanzania mnaowategemea kushinikiza NO REFORMS, NO ELECTION, ili kuleta REFORMS, hawako kama mnavyowafikiria, bado kabisa kujitoa "mhanga" kutafuta haki!
SIKILIZA USHAURI:
View: https://www.youtube.com/watch?v=ANA3rytxn0Q
Erythrocyte please take note!
Kamati kuu ya CHADEMA kabla hata Lissu hajashinda uenyekiti ilikosea kuweka hili azimio ambalo hata wao wanajua halitekelezeki.
Nchi hii nlliishasema huko nyuma nara kadhaa kuwa : hakuna nwanasiasa nwenye watu kwa sasa,hapa Tanzania zaidi ya kuwa na mashabiki wa key board tu. Zanani Maalim Seif na Nyerere ndio wakikuwa na watu ambao walikuwa wana uwezo wa kuwashawishi wakaingia barabarani.
Uchaguzi utafanyika tena bila rabsha; hakuna mfuasi wa CHADEMA hata viongozi ararisk kuzuia uchaguzi.
Hivyo CHADEMA watachelewa ,kujiandaa na uchaguzi kwa kuteua wagombea au hawatashiriki kabisa. ACT wao wamekuwa wajanja kwa sasa wanaandaa wagombea huku pia wakisema watashirikuana kuzuia uchaguzi maana yake ikishindikana kuzuia watashiriki na watakuwa hawajachelewa tofauti na CHADEMA.
Kauli hii No reform no election itadhihirika ni paper tiger na itashusha sana heshima ya CHADEMA na itaonekana wao ni watu wa maneno tu. Pi kauli zijazo za CHADEMA hazitatiliwa,maanani.
Lissu hakumbuki baada ya uchaguzi wa 2920 akiwahimiza wananchi kujitokeza barabarani na hawakutokea?
Kwa sasa vyama vingejikita kudai mambo haya ambayo ni rahisi serikaki kuyafanya.
1. Wagombea wa vyama wasikatwe hata kukiwa na kasoro muda utolewe kurekebisha kasoro.
2. Mawakala wa vyama wasiapishwe na DED bali wawe na barua ya utambulisho ya vyama vyao tu.
3. Uchaguzi usianze hadi mawakala wa vyama wawepo vituoni kama inajulikana kituo husika kina hao mawakala. Hii itazuia mawakala kufanyiwa figisu kuingia vituoni huku upigaji kura ukianza bila wao kuwepo.
4. Kura zihesabiwe vituoni, kila wakala apewe nakala ya matokeo iliyosainiwa na pia matokeo ya kila kituo yabandikwe katika hicho kituo.
Haya yakifanyika wapinzani watashinda baadhi ya maeneo kwa asilimia kati ya 30 - 45. CCM itashinda kati ya asilimia 55 - 70.
Natoa rai kwa CCM wasilazimishe ushindi wa asilimia 90, siku hizi wapiga kura wamegawanyika sana kimalengo hivyo haiwezekani tena chama kimoja kupata asilimia 90.
Hiki ndicho chanzo cha mtafaruku, mauaji na dhuluma zingine kwa wapinzani wao. Kwani CCM ikishinda kihalali kwa asilimia 55 kuna ubaya gani hadi muue raia wenzenu kisa mnatafuta ushindi wa asilimia 90?