Tundu Lissu na CHADEMA kama chama, sikiliza ushauri huu wa Ansbert Ngurumo

Sikiliza, CHADEMA wasingeshiriki uchaguzi wa 2020 hata kama CCM wanaendelea na mambo yao ingekuwa sauti tofauti na unayoisikia leo, CHADEMA wasiposhiriki na CCM wakaleta tule tu vyama haitawazuia CHADEMA kupaza sauti.Uchaguzi wa Mitaa vijiji na vitongoji 2024 ulishuhudiwa hata na viongozi wa dini kuwa maovu yalifanywa CCM wapate ushindi,4r za Samia na maovu ya uchaguzi wa wenyeviti 2024,hali itakuwaje 2025? Kukosa kila kitu na kupata kila kitu unahakikishaje kwa katiba na sheria za tume hiyo yenye wasimamizi hao wanaowekwa na
Mwenyekiti wa CCM na imeongezewa kaneno,HURU,ndiyo kusema hakuna kususia ila tuzuie uchaguzi usifanyike, viongozi wa dini,asasi mbalimbali,vyama vya siasa na wananchi. Tukishindwa sisi leo, kesho tutawaambia watoto wetu.
 
Wakati wa kampeni za uchaguzi wa Chadema nilisema wazi kabisa kuwa chaguo la CCM ni Lissu maana wanajua madhaifu yake. Udhaifu mkubwa ni kuwa ni emotional ( wafuasi wake watasema passionate), asie samehe (bado anarusha vijembe kwa watu kama Aidan na inaelekea amemweka pembeni Sharifa na kila siku anakumbushia risasi alizopigwa) na vitu vya kila siku vya uongozi huwa vinam'boa ( kutafuta pesa, kuandaa mikutano ya kiutawala, kuisimamia secretariat n.k.).

Mbowe ni tofauti. Yeye ni ruthless inapobidi lakini haruhusu emotion zake zimtawale katika maslahi ya chama. Yuko tayari kumsamehe mtesi wake au mtu waliowahi kukoseana ili mradi lengo lake linafanikiwa. Tumeona alivyoshiriki majadiliano kuhusu maridhiano na wale ambao wamemfunga na kumsababishia hasara kubwa. Angeshinda uchaguzi, angewapa nafasi za uongozi watu waliokuwa wakimpinga hata kama angekuwa na kinyongo nao.
CCM wanajua Mbowe ana uwezo mkubwa wa kutafuta pesa za kuendesha chama, kitu alichodhihirisha wakati wamesusia ruzuku.

Aidha, ni administrator mzuri sana. Saa hizi angekuwa Kigaila yuko vijijini akihamasisha watu kujitayarisha kwa ajili ya uchaguzi.

Ushauri wangu kwa Chadema ni kuwa wajiandae kwa ajili ya uchaguzi kwa ku recruit watu wanaokubalika ili wagombee nafasi zote. Wakati huo huo waendelee na mass mobilization kuhusu " No Reform No Elections". CCM wakiona jinsi watu wanavyokikubali kwa hali na maki wanaweza kukubali kufanya mabadiliko muhimu katika sheria ya uchaguzi.

Kushiriki katika uchaguzi ni muhimu kwa sababu ni njia kubwa ya kupata pesa za kuendesha na kutangaza chama. Uchaguzi pia ni platform kubwa ya kuwaelimisha wananchi kuhusu mapungufu ya chama yawala. Kama Lissu atagombea urais, sidhani kama Samia anaweza kutangazwa mshindi wa asilimia 99. Wabunge wachache watakaowapata watakuwa wanawasha moto bungeni kushinikiza mabadiliko.

Amandla...
 
Suala ni kwamba hatutapiga kula,
bas maana ata ukipiga kula itapotea na kuibiwa km za wenyeviti so ni vema iyo sku uitumie vzr kwa kulala kujiandaa na kesho yake sku ya kazi.
Ukipiga zinaibiwa na ata usipo piga ni vema zaid
 
Ni Moja ya ushauri wa hovyo wa Ngurumo
 
Ngurumo ni mpumbafu, chaguzi zote tatu zilizopita bado ana imani na tume hii ya rais Samia? Matokeo ya uchaguzi 2025 tayari yapo inasubiliwa tarehe tu yatangazwe. Upinzani wakishiriki au wasiposhiriki hakuna jipya litakalobadilisha maamuzi ambayo tayari yapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…