Uchaguzi 2020 Tundu Lissu na Dkt. Magufuli wajiandae kisaikolojia, lolote linaweza kutokea

Anachokosea mgombea wa CCM ni kudhani wananchi wanastahili kutishwa ilihali yeye yupo ikulu anakula, kuvishwa, kulindwa, kutibiwa n.k kwa kodi za wananchi hao hao, alipaswa aendeshe nchi kama nchi na sio kama familia yake.

Leo ni kipindi cha kampeni lakini ukimsikia kwenye majukwaa unagundua kabisa kwamba hakujianda vizuri kisera nadhani ni kutokana na kudanganyika kwamba huenda upinzani ungekuwa umekufa kifo cha mende kumbe ndo ameupalilia na kuuwekea mbolea ya kuuotesha vizuri kwa wakulima tunasema ameweka DAP.

Kutokana na hali halisi anayoiona ndo anakumbuka shuka kumekucha kwa hiyo anakosa mbinu za kiplomasia za kushawishi wapiga kura na kuomba radhi pale aliposhindwa kutekeleza anabaki kuongea kwa jaziba za waziwazi sawa na simba aliejeruhiwa.
 

Nisikukatishe tamaa ila nadhani humjui Lowasa vizuri, anyway! Kulinganisha uchaguzi wa 2015 na huu wa saahv wala sio kazi ngumu,
wala haihitaji maelezo mengi msikilize mgombea mwenyewe utajua mwaka huu wanatoka na asilimia ngapi
 
Bado,tena bado sana kwa upinzani kuitoa madarakani CCM.
kuna wapiga kura wengi sana mijini na vijijini ambao bado hawajafikiwa na ushawishi wa kubadilika na kuwa wapinzani na wakakubali,watu wanamna hii wapo wengi hasa vijijini.

hata nguvu ya upinzani mijini inaonekana kwa hamasa na mlipuko wa muda mchache tu kwenye mikutano ama mapokezi.
Ili ushindi upatikane kunamipango nje ya juu ya jukwaa la kampeni na mapokezi ya mgombea, jambo ambalo wapinzani wamepwaya sana.

Viongozi wa vijiji na wenyeviti wa mitaa (kwa sasa hawa wote ni wa CCM)ni angle mojawapo nzuri sana ya kufanikisha mikakati ya ushindi kwakuwa wanaijua vizuri jografia ya mitaa/vijiji pamoja na kuwatambua watu wao.
mengine sitosema kiundani zaidi hayo machache yanatosha kuipa ushindi wa kimbunga CCM.
JPM mitano tena,ushindi mwaka huu zaidi ya 90%
 
Reactions: 120
Kuna maandiko kama haya zaidi ya kumi humu JF. Is it a coincedence? Au ni mkakati? Anyway tukutane 28 Oktoba tuone ukweli wa haya maandiko.
 
Naomba kuuliza uchaguzi uliopita upinzani walisema wameibiwa kura sasa hawa Ccm hzi kura wanaiba muda gani au maeneo gani wakati kule vituoni matokeo yana kuwa safi kabsa.
 
*ASASI YA KIRAIA YA DEMOKRASIA TANZANIA (TDO)*

_*TAARIFA KWA UMMA*_

*TDO* ni asasi ya kiraia isiyokuwa ya kiserikali (NGO) ililosajiliwa kisheria kwa lengo la kulinda demokrasia nchini.

Asasi hiyo ni moja ya Taasisi zilizosajiliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya kuangalia (observe) uchaguzi ili kuhakikisha unakua huru na wa haki.

Tunautaarifu umma kuhusu vitendo visivyokua vya kidemokrasia vinavyofanywa na viongozi wa CHADEMA.

Waangalizi wetu wamethibitisha kwamba viongozi wa CHADEMA wanapita usiku na kuwaambia wanawake kwamba watoe vitambulisho vyao vya kupigia kura ili wapate mikopo.

Viongozi hao wanachukua hizo kadi na kwenda kuzidurufu (photocopy).

Tuna taarifa kwamba hizo kopi wanakwenda kuzitengenezea vitambulisho feki ili wavitumie mapema asubuhi kujipigia kura.

Baadhi ya wanawake walioahidiwa mikopo tayari wameshatoa vitambulisho vyao.

Asasi yetu bado linaendelea na utafiti ili kubaini maeneo yote yaliyoathiriwa na vitendo hivyo. Waangalizi wetu wanaamini kuwa huenda uovu huu umefanyika nchi nzima.

_*Kufuatia vitendo hivyo tunatoa wito ufuatao:*_

Watanzania wote wajiepushe kutoa vitambulisho vyao kwasababu huenda vikatumiwa kufanya uhalifu.

CHADEMA iache vitendo hivyo ambavyo vinakiuka sheria, kanuni na maadili ya uchaguzi.

TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Mamlaka zingine zihakikishe kwamba rushwa (adui wa haki) inadhibitiwa ili uchaguzi uwe huru na wa haki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusubir October mana uzi Sasa ivi zimesha kua nyingi mpaka zinakera ila tundulisu akijitaid Sana ni asilimia 3

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Ikiwa hali itaendelea hivi Dr Magufuli ajiandae kisaikolojia, kushindwa kwa 49% au kushinda kwa 51% huenda akaipoteza Ikulu, na Tundu Lissu ajiandae kushindwa kwa 49% au kushinda kwa 51%
Sahau hii ndoto yako.
Magufuli atamshinda Lissu kwa ushindi unao anzia 60%.
Mark my words.
 
Subilini 28, halafu muludi hapa mtueleze nini kimewa sibu.
 
Tathmini mujaarabu kabisa. Mgombea mmoja anaongea na wananchi na kuomba kura lakini mgombea mwingine anawafokea wananchi, kuwatukana kwa dharau kubwa huku akionesha dhaahir kuwa hahitaji kura zao. Mimi naona wagombea wetu wawili wanaoonekana wapo katika mchuano mkali ni "uncomperable". Hapa hakuna cha 51% kwa 49%. Mgombea aliye serious aliyeamua kuomba kura za watanzania kwa dhati ataibuka na 80% dhidi ya 20% za mtesi, mtukanaji, mdhalilishaji na mwenye kudharau umma wa watanzania. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Chadema hii ya Lissu ni ndembe ndembe kuliko ile ya mabadiliko lowasa. Mnafeli kuanzia udiwani mpaka Urais.
 
Ha ha ha Lissu huyu kibaraka wa mabeberu,apate kura 80%?.Unacheza wewe, chama cha Mbowe kina washabiki tena mitandaoni tu huko kwenye field hata hao 20% ni wengi mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…