Uchaguzi 2020 Tundu Lissu na Dkt. Magufuli wajiandae kisaikolojia, lolote linaweza kutokea

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu na Dkt. Magufuli wajiandae kisaikolojia, lolote linaweza kutokea

Mwaka 2015 CCM walipata kura 8.8M na Chadema 6M kulikuwa na tofauti ya 2.8M. CCM waliweza kuikamata kanda ya ziwa.

Kipindi hiki upepo umegeuka na kanda ya ziwa haipo kama wakati ule na inategemewa vijana wengi watapiga kura kwa mara ya kwanza . Pia kuna presence kubwa ya watanzania mitandaoni kuliko 2015 na ndio maana pamoja na kukosa mabango ujumbe wa TAL bado unafika tu.

Mikoa ya Kagera , Mara, Kigoma, Mtwara,Lindi,Geita, Shinyanga, Iringa, Mbeya, Dar, Kilimanjaro, Arusha na maeneo ambayo JPM hataweza kwenda yanaweza kupiga kura Chadema. Na kule Zanzibar sio siri CCM inazidi kupoteza umaarufu.

Mchuana wa Dodoma, Tabora, Tanga unaweza kuwa key.Na CCM wakichapwa kwenye maeneo hayo ndio shughuli imeisha!!
 
Acha na koma kumlinganisha Raisi wetu na takataka, ...
Safi sana mkuu,kumlinganisha Rais wetu Mh.Lissu na matakataka ni kumkosea sana heshima.Leo umeongea point tangu umekuwa humu jukwaani.Naona fahamu zinaanza kukurejea KUELEKEA Oct 28.
 
Hakuna wajinga wakat wew umeshavuka viwango vya ujinga na kuwa mpumbavu . Hebu angalia utopolo ulioandika.
Lisu hawezi kushinda uchaguzi huu.ccm Na kiongozi wetu tukubali kubadilika baada ya uchaguzi Na tuache propaganda za kitoto.watanzania sio wajinga kama tunavyofikiria
 
Bado hoja ni zile zile nyepesi!

Kwanini uchguzi huu ni mgumu?

Jibu: Lisu ni jasiri sana!

. Vituko Vya chadema hivi
Huna hoja acha wenye vichwa vinavyofikiri kwa weledi km mleta post wafikiri kwa niaba yko.Ni nn ulichoandika sasa.Busara ungesoma halafu ukapiga kimya.Hizo hoja ngumu ulizoleta wewe ziko wapi.mpuuzi tu.
 
H
Bado,tena bado sana kwa upinzani kuitoa madarakani CCM.
kuna wapiga kura wengi sana mijini na vijijini ambao bado hawajafikiwa na ushawishi wa kubadilika na kuwa wapinzani na wakakubali,watu wanamna hii wapo wengi hasa vijijini.

hata nguvu ya upinzani mijini inaonekana kwa hamasa na mlipuko wa muda mchache tu kwenye mikutano ama mapokezi.
Ili ushindi upatikane kunamipango nje ya juu ya jukwaa la kampeni na mapokezi ya mgombea, jambo ambalo wapinzani wamepwaya sana.

Viongozi wa vijiji na wenyeviti wa mitaa (kwa sasa hawa wote ni wa CCM)ni angle mojawapo nzuri sana ya kufanikisha mikakati ya ushindi kwakuwa wanaijua vizuri jografia ya mitaa/vijiji pamoja na kuwatambua watu wao.
mengine sitosema kiundani zaidi hayo machache yanatosha kuipa ushindi wa kimbunga CCM.
JPM mitano tena,ushindi mwaka huu zaidi ya 90%
Huna hoja.Subiri Oct 28.
 
Bahati mbaya sana kwa wafuasi wa Magufuli mambo kama haya ni matusi kwao.
Nileteeeni Gwajimaaaaaa
Nileteeeni Gwajimaaàaaaaaaaaaa
Nileteeeni Gwajimaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Nileteeeeni gwajimaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Nileteeeeni gwajimaaaaaàaaaaaaaaaàaaaaàaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Hamnionei hata huruma sauti hadi inakauka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wenye vyeti halali mmewaajiri?
Wewe utopolo
Hawajaajiriwa.

Sasa kipi bora kuwa na wafanyakazi wenye vyeti feki, halafu na wenye vyeti halali wakose kazi.

Na kuwa na wafanyakazi halali walio na vyeti halali. Alafu vyeti visivyo halali wakakosa?
 
Na: George Kabadi

Nimekuwa miongoni mwa wafuatiliaji wazuri wa kampeni za mwaka huu 2020, Naomba kupigana moja kwa moja na hoja za watu wanaodai uchaguzi wa mwaka huu siyo mgumu kama ule wa mwaka 2015. Napigana nao kwa sababu kuu mbili.

MOSI, Uchaguzi wa 2015, Edward Lowassa alikuwa na watu wengi lakini hakuwa bora, hivyo siasa ya 2015 ilikuwa siasa ya upepo usio na mikakati.

PILI, Lowassa alibebwa na nguvu ya umaarufu kwa maana hata wasio wapiga kura waliohudhuria kampeni zake.

Tofauti kubwa iliyopo katika uchaguzi wa mwaka huu na uchaguzi uliopita, ni kuwa Mgombea wa CCM, ni Mgombea ambaye tayari jamii ishauona Mwelekeo wake, na Mgombea wa Upinzani ni Mgombea halisi zao halisi la upinzani.

Tazama kampeni za Tundu Lissu, na tazama kampeni za John Magufuli utagundua kuwa kuna Mgombea Urais anaongea na wananchi na kuna Mgombea Urais anawafokea wananchi.

Kuna mapungufu mengi kwa Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi kuliko Mgombea Urais wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, nalisema hili bila kificho.

Baada ya TUME YA UCHAGUZI kuidhinisha Wagombea 15 wa kiti cha Urais wa JMT, kwa tiketi ya vyama mbalimbali, kadri muda unavyozidi kwenda ni vyama viwili tu ndiyo vimeonyesha nia ya kushika hatamu, nadhani wengine wamekata moto, sasa ni Chama Cha Mapinduzi-CCM na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema.

Wakati chama Cha Mapinduzi kikijinandi kuwa Mgombea wake ametekeleza mambo mengi katika Uongozi wake wa serikali ya awamu ya tano, chagamoto za uhalisia wa maisha ya mtanzania, bado zinamhukumu hivyo hana budi kukubaliana na chagamoto nyingi atakazo kutana nazo katika kampeni zake, kuna makosa mengi na mara kwa mara yamekuwa yakijirudia, sifahamu ni kwa nini, ama Chama cha Mapinduzi hakina meneja kampeni?

Sifahamu! kwa maana Mgombea wa chama hicho akikosa ubunifu pindi anapokuwa jukwaani na kujikuta akitoa matamko badala ya kumwaga sera. Binafsi hukuona haja ya Dr Magufuli kujibu hoja ya Tundu Lissu kuhusu vitambulisho vya wamachinga.

Jibu alilolitoa ni mtihani kwake mwenyewe, unaposema vitambulisho vya wamachinga havina maana wakati wewe ndiye uliyevitoa unatoa mwanya wa mpinzani wako kukuhoji zaidi.

Najaribu kufikri Mgombea wa CCM anapowaambia wananchi, wakimchagua Mbunge wa Upinzani hatowapelekea maendeleo.
Lakujiuliza hapa ivi CCM wanashindwa kumkanya Mgombea wao kuwa tuko kwenye nchi ya Demokrasia? Watanzania wananahaki ya kumchangua kiongozi wamtakaye na Maendeleo ni haki ya kila mwananchi kwa sababu ndiye mlipa kodi?

Nasema kauli, kauli, kauli, kauli za namna hiyo ni ishara ya kiongozi kushindwa

Upande wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, chagamoto yao kubwa ni watu wanaomzunguka Mgombea, ni watu wanaoendeshwa na hulka, kinachoibeba Chadema ni uwezo binafsi wa Mgombea kucheza na akili ya wananchi na mpinzani wake wa karibu.

Akili ya Tundu Lissu inaufanya uchaguzi uwe mgumu, kukosekana kwa fikra mpya ndani ya Chama cha Mapinduzi, kunatoa mwanya kwa Lissu kulitawala jukwaa atakavyo katika kampeni, naweza kusema Tundu Lissu yuko kwenye ubora wa kimataifa

Kinachompa chagamoto Dr Magufuli ni yeye kuamini ndiye anaweza kuliko watu wanaomzunguka, sijui kwanini Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dr Bashiru anashindwa, kutengeneza muunganiko wa jamii moja ndani ya Chama kimoja ili kutuliza hali ya hewa.

Ikiwa hali itaendelea hivi Dr Magufuli ajiandae kisaikolojia, kushindwa kwa 49% au kushinda kwa 51% huenda akaipoteza Ikulu, na Tundu Lissu ajiandae kushindwa kwa 49% au kushinda kwa 51%

Kitendo cha Dr Magufuli kushindwa kuwapa hamasa watu wa Bukoba wakati wa tetemeko la aridhi kumempunguzia kura za kanda ya Ziwa, na kuendelea kudhani watanzania bado ni jamii ya kuendeshwa huenda kukamtia katika promoko la karne.

Kabla ya 28 October 2020 anapaswa awaunganishe wana CCM, ambao hadi sasa wamepasuka, idadi kubwa ya viongozi wa ngazi za juu ndani ya CCM hawamuungi mkono Dr Magufuli, Japokuwa machoni wanampa tabasamu huku nyuma wanamchinja.
Kabla hata ya wapiga kura million 29,188,347 hawamchinja.

Huu ni mtazamo na hoja yangu, binafsi naona.

"Kuna Mgombea Urais anaongea na wananchi, kuna Mgombea Urais anawafokea wananchi"

Sijui mtazamo wako!

Kalamu Ya Mwebrania
Na: George Kabadi
MgombeaUrais2035
Ulichokinena ndicho nilichokiona mimi tokea siku ya kwanza ya kampeni, Lissu kwa kiwango kikubwa na nadhani amefanikiwa sana kutumia mambo makubwa ambayo ccm wamefanya katika haya wanayoita maendeleo ikiwemo kununua hizo ndege, flyover kuyatumia katika kampeni zake na kuonekana "It is good for nothing" yanaonekana ni mambo ya kifisadi uliokubuhu.

Lakini jengine sijuw niseme ccm nao hawakutarajia au hawakujipanga kujengea hoja hayo maendeleo wanayodai mana Magufuli alipojaribu kujibu vitambulisho vile sio lazima halafu akaja akasema unaweza kuombea mkopo Lissu ndio amekuja kuwakata roho kabisa kabisa alipokishika kitambulisho kumbe hakina jina wala anuani wala chochote.

Lakini jengine linalofurahisha kwa upinzani Lissu saivi kwenye kampeni tayari ameshajua yale mambo yanayooumiza zaidi upande ccm na yeye anakuwa akirudia mara mara ili kuzidi kushawishi watu na sasa watu naona kila aendapo ni kuliko alikotoka.

Mimi nilijuwa kwenye kampeni hizi ccm watataradadi sana kwenye maendeleo ya ujenzi, na ununuzi wa hizo ndege na mabarabara nk na nilidhani upinzani kwa kweli hawatakuwa na hoja na hata ccm wenyewe wamekuwa wakisema kabla ya kampeni kwamba mara hii uchaguzi utakuwa rahisi sana mkuu amefanya mambo mengi nadhani hapa ndipo walipobweteka.

Kama hicho kiwanja cha ndege Chato watanzania wengi walikuwa hawajui lakini sasa imeonekana yule jamaa pale juu amefuja sana hela za walipa kodi kwa kweli huu uchaguzi upo katika position ambayo ni very interesting. Yuou never know lakini Lissu amefika mbali sana kuliko viongozi wote waliowahi kuwa wapinzani kwenye ngazi ile ya urais wa JMT. Chochote kinaweza kutokea.

Lakini jengine Lissu ananiacha hoi akiwambia wananchi na kusisitiza kwamba uchaguzi ni muhimu kuliko wowote ule anawajenga wananchi kisaikolojia katika kiwango cha juu kwenda kumpigia kura. Anatumia akili sana kuiba uwezo na mawazo ya watu waone kuna haja ya mabadiliko kwa namna yoyote ile. nampongeza sana.

Na hili la Magufuli kupiga magoti naamini hapigi tena magoti Lissu amemuua sana alipopiga magoti.

Jana namuona Mafuguli anawatahadharisha wana ccm tu wasjiingize kwenye maandamano sikuona hoja za msingi kushawishi achaguliwe tena.
 
Back
Top Bottom