Yerusalemu30
Member
- Feb 23, 2025
- 17
- 19
Tutakomaa lini ikiwa Viongozi wanahamasisha zaidi kutatua matatizo ya ndani kupitia wa watu wa nje.Wakuu,
Kumbe Heche na Lissu walikuwa na mpango wa kando kuendeleza kampeni yao ya No Reforms No Election ukiachana na kuwaambia watu walale barabarani
Erythrocyte nimeanza kukuelewa sasa
===================================================
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche amesema yeye na Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu wanatarajia kupeleka ajenda ya no reform, no election hadi nje ya nchi.
Akizungumza na wanachama wa chama hicho wa Kanda ya Kaskazini, mkoani Arusha leo Heche amesema tayari chama hicho kimewashirikisha wadau mbalimbali kuhusu ajenda hiyo na kwamba wataipeleka mbali zaidi.
“Ajenda yetu no reform, no election inazungumzika hata kama wanaizungumzia negatively (kwa mtazamo hasi) lakini wanazungumza ajenda ya CHADEMA, tumetoka na ajenda hiyo ndiyo kila siku Wasira anaimba na leo ndio Makala alikuwa anaizungumza” amesema Heche.
“Sisi ni watu tunatumia brain (akili) tume engage (kushirikisha) tumeandika mapungufu 16 ya uchaguzi ambayo hayamuwezeshi mpinzani yoyote kushinda uchaguzi, nani miongoni mwenu anaweza kusema kwamba anaweza kushinda uchaguzi kwa utaratibu huu tulionao?” amehoji Heche
Source: Nipashe
Hao wa nje ni WEMA sana kwetu au ndio mianya ya baadae kuwa watumwa wa sera zao kama ilivyo Sasa.
Wananchi wanafurahishwa kwa maneno matamu wanayotaka kuyasikia kisa ya changamoto wanazipitia badala ya kuangalia vyema njia ya utatuzi wa tatizo, we can't solve the problem through same mind created.
We obsessed to rule but not ending the problems.
Tuepuke maneno ya Viongozi wasio leta hoja zenye tija. Hatupendwi hata na nchi zinazotuzunguka sembuse za nje.