Uchaguzi 2020 Tundu Lissu na timu nzima ya CHADEMA, kura nyingi sana ziko kwa akina mama na wanawake, nendeni na kauli mbiu hii "Mama Mwokoe Mwanao"

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu na timu nzima ya CHADEMA, kura nyingi sana ziko kwa akina mama na wanawake, nendeni na kauli mbiu hii "Mama Mwokoe Mwanao"

Wapwa,
Ni ukweli usiopingika kuwa wanawake wamekuwa ndio kimbilio la CCM kujichotea kura lukuki tangu kupatikana kwa uhuru.
Wenzenu wanatumia wasanii kushawishi wakina mama kupigia kura chama chao, hii tumeiona tangu 2015 kwenye kampeni zao kama 'MAMA ONGEA NA MWANAO' ambayo bila shaka ilifanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90%. na mwaka huu tena wameamua wapite godoro kwa godoro kuomba kura za akina mama na wanawake

Ningeshauri wagombea wa Chadema na ACT kwa Zanzibari watumie mbinu hizi kupata kura kutoka kwa akina mama
  1. Nendeni na kauli mbiu, MAMA MWOKOE MWANAO
  2. Mnaweza kuandaa mikutano ya ndani ya wanawake hata kama ni asubuhi kabla ya mkutano wa kampeni, kuongea na akina mama na wanawake wote ndani ya mkoa husika
  3. Kama alivyokua anafanya Mama Lowassa 2015, mtumieni mke wa Lissu, apite mikoani kuelezea ushuhuda pamoja na kuongea na akina mama
  4. Baraza kuu la wanawake ( Halima Mdee na wenzako ), waanze haraka sana kupita mikoani, wajigawe kikanda. hii itasaidia kuongeza ushawishi kwa akina mama
  5. Tumieni madhaifu ya CCM ya udhalilishaji dhidi ya wanawake, yapo mengi sana.
  6. Piganieni kwa nguvu zote wagombea wote wanawake waliokatwa warudishwe, hi itaongeza kura zenu maradufu
  7. Kuna sababu zaidi ya 1000 za kumwambia mama amwokoe mwanae
View attachment 1554876

Ila msikengeuke, mkapata madaraka na kuwasau wanawake na akina mama, kama walivyosahauliwa na kudharauliwa ndani ya miaka 5 ya utawala wa mkoloni mweusi

Bado mna nafasi kubwa ya kubadilisha duru ya siasa ndani ya siku 57 zilizobaki.

MAMA MWOKOE MWANAO
Wazo zuri , nadhan watalifanyia kazi ASAP
 
Mtaji wa CCM haupo kwa wakinamama pekee, upo kwa wakinababa, na vijana pia lakini bila kuwasahau chipukizi. CCM unamtaji mkubwa sana kwa wasanii wa bongo movie, bongo fleva na wasanii wengine wengi wa ngoma za asili n.k

Hamna namna nyingine ya vyama vya upinzani kuweza kukishinda CCM, kwanza ni chama kilichokomaa katika siasa za kidunia na kwa siasa za Tanzania, CCM ndio mwalimu mkuu. Chama hiki kina wanachama wengi wenye kusema na kutenda, hiki chama kinanyumbulika wakati wo wote na kwa sababu hiyo, ikiwa vyama vya upinzani vinatanuka chenyewe kinasinyaa, na upinzani ukisanyaa chenyewe kina kinatanuka. CCM hakijawahi kukaa levo moja na vyama vya ruzuku.

Ni ndoto ya mchana kufikiri CCM kina mtaji wa wakinamama pekee. Rejea kauli ya Lisu mwenyewe, wakati anazunguka kutafuta wadhamini na huku akifanya kampeni uchwara. Alikiri wazi kuwa CCM ni chama kikubwa na chenye nguvu, hatujaweza kukishinda kirahisi. Na kwa kweli aliwaongopoea pia kwani ilimpasa aseme ukweli wazi kwamba ni chama ambacho hatuwezi kukishinda katika uchaguzi wa mwaka huu kwani Mzee Lowasa na umoja wa UKAWA ulishindwa na yeye ni kama Nani hata aweze!

Mtaji wa CCM ni watanzania wenye kutaka maendeleo, amani, utulivu, umoja na wenye kuheshimiana.
Mtaji WA CCM ni wajinga ambao ndio wengi zaidi tz
 
Kuiga ni kuzuri je mnatumia mbinu gani kuiboresha hicho mlichokiiga ndo shida inapoanza hapo
 
Mtaji WA CCM ni wajinga ambao ndio wengi zaidi tz
Huna uwezo wa kutaka watu wote waamini kile ambacho wewe unakiamani, ambacho kinakufanya wewe ujihisi sio mjinga. Huo uwezo sio wa kibinaadamu na nafikiri hiyo kazi hata Mungu hakuifanya.
 
Naamini wahusika wamesikia na kuelewa, pia watafanyia kazi.
 
Lakini hatulazimishi walimu waende kwenye kampeni
Zaidi ya kubumba barua na kuchongesha mihuri feki sidhani kama mngeweza kuishi mjini.

Hizo barua zote mnazosambaza ni feki
 
Back
Top Bottom