Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndani ya Mwendokasi kuelekea Kariakoo

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndani ya Mwendokasi kuelekea Kariakoo

Habari wanajf, kama ilivyo kawaida nimejitolea kuwajuza kila linaloendelea kuhusu chama chetu na kushauri nini kifanyike ili tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea.

Nimeshtushwa sana na kushangazwa kwa jinsi ambavyo tunavyorudia mbinu zilezile kama zilizotumiwa na Lowassa 2015
Hii ya mgombea wetu kupanda mwendokasi haijakaa vizuri kwa kuwa wote tunafahamu ni kitu ambacho sio halisia(hajawaho kupanda kabla iweje sasa?)

Hii kwa watu wenye ufahamu tunaweza kuwakwaza kwa kuwa watajua hatupo serious.

Ninaomba chama kishauri na kitekeleze vitu ambavyo vinaweza kuleta tija na kuvuna watu wengi na wapiga kura wengi ila hili la kupanda mwendokasi HAPANA.

Kuna namna nyingi ya kuvuta attention za watu na kujizolea kura za bure kabisa. Mfano; kuna mechi ya somba vs yanga tarehe 18.

Hapo anaweza kwenda uwanjani kama shabiki tu wa mpira na akavuna wapiga kura wengi tu kwa kuwa tukio la yeyr kwenda uwanjani ni halisi, sio hili la kupanda daladala/mwendokasi.

Pia bado ninaendelea na kushangazwa na watu wa Dar, kwa kuwa humo kwenye mwendokasi ni kama watu hawana habari vile, hii naweza kusema ni dharau kubwa sana watu wa dar mnayoionyesha na nashauri muache mara moja.

Chini nimeweka picha na video za humo kwenye mwendokasi

IMG_20201007_122258.jpg
IMG_20201007_122235.jpg
 
Ni mwendo wa kukutana na kila raia kila kona, wakifunga mlango mmoja watu wanafungua mingine kumi na moja, CCM mtupishe mwaka huu, tumewachoka.

Kila anaekutana na Lissu lazima atabasamu, huo ndio mpango wa Mungu muweza alie juu asieshindwa na chochote.
 
Back
Top Bottom