Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Huyo wa kupambana na lisu muulize kwanza pambano la kwanza alishinda? Kama c kubebwa na refa angeshinda? Yaan huyo ata nikisimama Mimi kama refa atachezesha fair basi namwacha mbali sana.... Sema ndo ivyo tena refa mwenyewe kawekwa na yy kwann asitetee ugali.
 
Kweli Magufuli alianza vizuri kwa kutumbua wala rushwa, lakini sasa ameishia kutetea wasio na vyeti kama bashite huku akikejeli wenye njaa na wenye matatizo
 
Bado mteule wa uraisi ni mgonjwa mheshimiwa mzee kiongozi wa kijadi Lowassa, hatukubali kusimamishwa mwengine yoyote tutakua ngangari kama CUF kwa kumsimamisha mzee SAWASAWAA??
 
Umeirudia rudia sana kuwa Tundu Lissu ni zaidi ya Magufuli ila hujasema ni nini kinamfanya awe zaidi ya Magufuli, kuwa specific uzaidi wake uko wapi!!

Tundu lissu ktk nyadhifa za uongozi alizo nazo sasa kama urais wa TLS, mwanasheria mkuu wa chadema, waziri kivuli wa katiba na sheria, hajaonyesha upekee ktk maeneo haya. ILA NI MLALAMIKAJI MZURI kama EMPTY VESSEL.
Mimi nahitimisha, uchaguzi wa 2020 utakuwa ni kiini macho na itakuwa hivyo sababu watanzania wengi watamchagua kihalali JPM.
 
Hili neno "lazima" naona kama lina ukakasi fulani!. Kwa nini ni lazima awe Lissu?. Ulazima wake ni upi na ulazima wa nini?. Isije kuwa hata zile pyu pyu ni friendly fires ili kuondoa huo ulazima?.

P
I disagree na wewe mkuu, the way hili jambo linavyokuwa treated mpaka sasa hamna hata washukiwa ni wazi walijaribu kufanya hilo tukio la kumuondoa ni watu untouchable. Ila wangekuwa sio wao!!!! mbona ungeona watu wanapatikana kesho yake na silaha zinaoneshwa laivu kweny presi konferesi. Acha niishie hapa mwaka 2018 haujaisha bado, nisije nikaulia segedansi
 
Ha ha ha ha.. Lissu ni mzuri sana, ana akili sana, ni mpambanaji sana, na anaijua sheria sana.. Kwa kifupi yuko vizuri sana..
Ila kwa uraisi kwa maoni yangu hapana..

Kama Tundu Lissu ni hapana, napenda kukuhakikishia kuwa, basi John Pombe Magufuli ilikuwa na bado ni HAPANA kubwa 1,000,000 times!!

Nakubaliana na mleta hoja, kwamba, mtu pekee kwa sasa wa kukabiliana si tu na Magufuli ama CCM bali na mfumo wote wa kidola kwa hoja na kinguvu katika uchaguzi mkuu wa 2020 ni Tundu Lissu na si mwingine yeyote!!

Huyu jamaa akigombea Urais kupitia chama chochote (ukiiondoa CCM) ktk uchaguzi wa 2020, nakuambia hamasa na amshaamsha ya uchaguzi huo ujao, itakuwa si ya kawaida na ari na purukushani za ule wa 2015 baada ya Lowassa na wenzake kuikimbia CCM ulikuwa ni cha mtoto.....

Na pace hiyo kwa TL itakuwa hivyohivyo hadi anaingia Ikulu ya CHAMWINO huku wapinzani wake CCM na dola kwa ujumla wakiwa wamepigwa bumbuwazi kwa kutoamini yanayotokea mithiri ya wana wa Israel walivyoangusha ukuta wa Yeriko kwa mzaha tu wa kuuzunguka mara saba!
 
Ha ha ha ha.. Lissu ni mzuri sana, ana akili sana, ni mpambanaji sana, na anaijua sheria sana.. Kwa kifupi yuko vizuri sana..
Ila kwa uraisi kwa maoni yangu hapana..
U Rais ni taasisi kwa tabia na hulka za Waziri was ujenzi ungetegemea awe Rais?
 
Kisukuma na Kizinza hapo naona kuna kitu unaficha ili kupata kile unachopata.

Umekuwa kigeugeu kabisa ulisema hana mpinzani leo unamtaja Zitto kwa mashaka mashaka na kuinua Tundu Lisu kwamba ana faa kukabiliana na mheshimiwa na umeenda zaidi kwa kusema Yeye ni zaidi ya Mheshimiwa.


Hii mbinu uliyotumia ni mzuri sana kwa watoto watoto lakini kwa watu wazima umekosa ndugu. test and errors.
 
U Rais ni taasisi kwa tabia na hulka za Waziri was ujenzi ungetegemea awe Rais?
Uraisi ni taasisi pale katiba na sheria za nchi zinafuatwa.. Lakini anapopatikana raisi dikteta, dhana ya uraisi taasisi inakufa.. kwa serikali hii ya awamu ya tano, uraisi sio taasisi, uraisi ni mtu, Jiwe..

Lissu is too good to be a president.. Tunamuhitaji awe upande wa wananchi always..
 
TL anajua sana siasa za ushawishi.Vipi kuhusu Dkt.Membe?
 
Ndugu Paskali, mheshimiwa Lisu ni mtu jasiri na mwenye hoja makini lakini kwa kupewa kugombania nafasi ya urais ni bado kwanza, kwani lazima aangalie afya yake mpaka pale itakapoimarika vizuri na hali yake ya kisaikolojia ikawa vyema kwani lile shambulio la kutaka kumuua bado liko kwenye akili yake na waliyotaka kuuondoa uhai wake rasmi hawajulikani hivyo si vyema kuwa mgombea wa urais. Naona Chadema wakitaka kutoa upinzani kwa CCM bora wamsimamishe Profesa Abdallah Safari, ambaye ni mtu asiye na jazba na ni mwenye hekima za kiuongozi.
 
Tundu Lissu ni zaidi ya Magufuli tatizo la Magufuli akizidiwa hoja anaweza chukua maamuzi makali saana maana ana hasira sana huyu baba,wakati ye akikasirika mwenzie atakuwa akicheka,kwani ugumu utakuwa pale azam tv au bbc itakapowaweka pamoja kuwahoji baadhi ya hoja zao na matarajio yao sidhani kama magu atweza stahimili ya huyu tundu,tundu si wa dunia hii ipo siku mtanielewa
 
Back
Top Bottom