Pascal Mayalla,
Pascal naunga mkono hoja yako.
Kuhusiana na swali lako kama Tundu Lissu akishinda atapewa ushindi au la, ni wazi kuwa kwa mazingira yaliyopo hatapewa.
Kwanza ni vizuri ieleweke kuwa CCM bado ni chama dola na Tanzania bado iko katika mfumo wa utawala wa udikteta wa chama (dola). Huu uchama dola na udikteta wa chama kimazingira vimesimikwa kikatiba na kisheria. Mapendekezo ya Jaji Nyalali yaliyokuwa na lengo la kuiondolea CCM hii hadhi ili vyama vyote vya siasa viwe na uwanja sawa wa mapambano ya kisiasa nchini yalitupiliwa mbali.
Sifa moja kubwa ya mfumo wa udikteta wa chama dola ni kukosekana kwa demokrasia ndani na nje ya chama. Hii maana yake ni kwamba, kwa mfano, wananchama hawana sauti katika maamuzi makubwa yanayohusu chama kama nani apeperushe bendera ya chama katika uchaguzi wa urais.
Nafasi ya kutoa maamuzi ambayo yangetolewa na wananchama kidemokrasia kuhusiana na nani awe mgombea urais kwa tiketi ya chama huporwa na kutekwa na kikundi kidogo cha vigogo (kinaitwa deep state) ambacho sio rasmi lakini ndicho chenye maamuzi ya mwisho. Na deep state ikiishamua ni nani awe mpeperusha bendera wa chama dola basi biashara imekwisha; huyo ndiye de facto rais wa nchi. Huu ndio utaratibu unaotumika kwenye mifumo ya kiutawala ya Kikomunisti/Kijamaa na ambao CCM imeurithi.
Kiufafanuzi, itakumbuka mwaka juzi wakati wa kinyang'anyiro cha kumpata mgombea urais wa CCM wajumbe wa kamati kuu (CC) ya CCM Sophia Simba na Emmanuel Mchimbi walishangaa na kuhamaki ni vigezo gani vilitumika "kuwakata" watia nia zaidi ya 30 akiwemo mtu wao. Hii maana yake ni kwamba hata CC kwenye hili suala ilikuwa ni rubber stamp tu!
Ni deep state pia ndio imeweka utaratibu unaofuatwa siku zote (ambao pia sio rasmi kikatiba) wa kupokezana urais kati ya waumini wa dini mbili kubwa nchini. Na haitoshi tu rais kuwa muumini ya moja kati ya hizo dini mbili kubwa nchini, pia ni lazima atoke katika kikundi/dhehebu fulani.
Pamoja na haya maelezo, ni muhimu sana kwa upinzani na hasa Cdm kuwa na mgombea urais mwenye nguvu za kisiasa zinazotokana na uthubutu wake, uwezo wa kujenga hoja, ushawishi na weledi. Kama ulivyosema katika kambi ya upinzani mwenye hizi sifa kwa sasa ni Tundu Lissu pekee.
Lakini ni muhimu zaidi kwa upinzani kuweka mikakati makhsusi ya kuhakikisha wanaongeza idadi ya wabunge na madiwani. Lengo kimkakati liwe ni kufikia uwiano wa idadi ya wabunge katika bunge na madiwani katika mabaraza utakaowezesha kuwepo kwa checks and balances; kitu ambacho ni muhimu kwa demokrasia kushamiri pamoja na kuwepo kwa uwajibikaji.
Nitarudi ili kujaribu kutegua hiki kitendawili: "Sijasema Lissu ni zaidi ya Magufuli kwenye nini, na nawaomba sana msiniulize!"