Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Wakudadavua amekimbia maswali yako . kuna watu katika maisha yao mabadiliko ni ngumu Kuya kubali. UnamuwekeA lift kwenye ghorofa afike haraka juu.yy anaendelea kutembea kwa ngazi..Ili ujue uwezo wa mtu lazma umpe nguvu ya kuongoza. Sasa kuna wale waliozoea kula kwa mfumo uliopo hawa ndy wapinga mabadiliko!!
 
Tundu Lissu naona amekaa kisheria sheria zaidu, nina wasi wasi na uwezo wake wa kusimamia maendeleo ya wananchi, ila all in all sidhani kama ana ushawishi mkubwa kwa wananchi. Kiufupi hafai na wala hafit hapo
Mkuu ubarinolutu , nina maswali madogo 6 kwako
  1. Kwanini una wasi wasi na uwezo wa Tundu Lissu wa kusimamia maendeleo ya wananchi?
  2. Kwanini all in all hudhani kama ana ushawishi mkubwa kwa wananchi?
  3. Kwanini unasema kuwa kwa kiufupi Lissu hafai na wala hafit hapo?.
  4. Katika waliopo, nani ana uwezo kusimamia maendeleo ya wananchi?.
  5. Nani ana ushawishi mkubwa kwa wananchi?
  6. Jee nani anaefaa na anae fit kwa urais wa Tanzania katika uchaguzi huu?.
p
 
Umeongea ukweli Mchungu ambao chama Chetu Pendwa sana CCM hakitaki kuusikia.Ukiniuliza nitasema hivi,kama siyo Lissu basi 2020 tunatakiwa tumeweke RAIS ambaye ni purely mwanasheria,siyo mwalimu wa chekechea wala wa secondary tunahitaji mwansheria.

Ukiangalia nchi nyingi duniani zimeendelea kwa kuwa na Rais mwanasheria,tukiangalia Zimbabwe first Lady wa enzi zile alikuwa Mwanasheria na alimsaidia sana Mugabe kuiweka Zimbabwe kwenye mstari,alipokufa Mama yule na Mzee kuchukua chicken & Chips,uchumi wa Zimbabwe ulidondoka kama mvua ya mawe.

Angalia Clinton na Obama wote ni wanasheria ona walivyojenga Uchumi wa Marekani,na leo muone Trump anachofanya kutwa kucha kugombana na wanaomkosoa,hana tofauti na Baba J.

Kama tungekuwa na Tume huru hakika TL fits for presidency.
Mkuu shemeji Tetty, duh...!.
Hivyo utampa?.
P
 
Kwa trends zinavyokwenda kuna uwezekano mkubwa hata wabunge wa kambi ya upinzani watapungua baada ya uchaguzi 2020 bila kujali nani atakuwa mgombea Urais kwa tiketi ya upinzani.
Mkuu MsemajiUkweli , huo uwezekano wa wabunge wa kambi ya upinzani watapungua baada ya uchaguzi huu wa 2020 kutokana na nini?.
Nini kitawapunguza?.
P
 
Hakika ni zaidi ya Magufuli, kwanza hana mascandle yule mwenyekiti wenu si ndiye aliyekwapua nyumba za serikali akagawa kwa wadada na nduguze?
Shemeji Tetty, acha hizo.. !. Hakuna nyumba ya serikali iliyo kwapuliwa, ule ni uamuzi wa serikali na waliogaiwa ni watumishi wa serikali haijalishi ni wadada au wakaka, au ndugu, jamaa na marafiki, the bottom line ni watumishi wa serikali!.
P
 
Paskali, si vema kumlinganisha mtu ambaye ana matatizo ya akili na Dkt Magufuli. Lisu ana matatizo yake binafsi kiakili.
Mkuu Mudawote , jee hili la Tundu Lissu kuwa na matatizo ya akili una uhakika nalo?. Miongoni mwa sifa za kugombea ni pamoja na kuwa na akili timamu, unaweza kuthibitisha kuwa Tundu Lissu ana matatizo yake binafsi ya kiakili?.
P
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali tuu, Ili uchaguzi wa 2020 usiwe ni igizo tuu la uchaguzi, Je tumchagize na kushinikiza Tundu Lissu ndiye asimamishwe na upinzani kumkabili John P. Magufuli? kwa sababu mpaka sasa, Tundu Lissu ndie mwanasiasa pekee wa upinzani ambaye so far, ameonyesha ana uwezo wa kumkabili Magufuli kwa vile uwezo wake ni zaidi ya Magufuli?

Kama kawaida yangu, kwenye kila mijadala yenye kuhusisha maoni ya kisiasa, mimi hupenda kuanza kwa declaration of interest kuwa mimi, japo ni mwana CCM, lakini kwenye kutanguliza mbele Maslahi ya taifa ni kama sina chama, sina kambi na sina upande, kwangu ni maslahi ya taifa mbele.

Baada ya rais Magufuli kuingia madarakani na kuanza na zile amsha amsha za uwajibikaji kwa ziara za kushtukiza , zilizofuatiwa na tumbua tumbua, nikauliza humu kama kweli Tanzania tunataka maendeleo ya kweli, je tuna haja ya kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?,
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020

Hivyo nikashauri, kufuatia Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kuonyesha uwezo wa kuibadili Tanzania, overnight, toka nchi masikini ya kutupa uliyodharaurika, hadi nchi tajiri inayoheshimika, Magufuli aachwe tuu hadi 2025 na hata ikibidi, hiyo 2025 tunaweza tubadili katiba yetu ili rais Magufuli aendelee tuu kama Nkuruzinza, Kagame, Museveni hadi awe kama Mugabe?.

Pia kufuatia trend ya chama kikuu cha upinzani kwa huku bara, Chadema kutoonyesha any seriousness yoyote kuelekea 2020,
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible
nikaconclude kuwa Uchaguzi wa 2020 kwa upande wa urais, litakuwa ni igizo tuu la uchaguzi kwa ushindi wa kishindo cha walkover kwa CCM.
In 2015 Election, Tanzania had A Choice To Choose From. Je Kwa

Lakini kwa mwenendo na matamshi ya Tundu Lissu ya hivi karibuni kumhusu Magufuli, kwa maoni yangu, kwa hapa tulipo, ukimuondoa Zitto ambaye he looks a bit compromised, Tundu Lissu ndie mwanasiasa pekee wa upinzani aliyeonyesha angalau uwezo wa kuweza kumkabili mgombea wa CCM kwa Uchanguzi Mkuu wa 2020, Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwenye Uchaguzi huo wa 2020 na Magufuli ukapata pata angalau kaji joto joto cha uchaguzi, vinginevyo wapinzani wakimsimamisha mgombea mwingine yoyote, mgombea wa CCM, Dr John Pombe Joseph Magufuli, hahitaji kufanya kampeni yoyote, ni ushindi wa kishindo straight forward kwa kwenda mbele kama ameokota embe dodo bivu chini ya mti wa mwambe!.

Kwa jinsi nilivyomsikia Tundu Lissu na namna anavyoongea, then huyu Tundu Lissu ni typical yuko kama Magufuli type tena yeye ni zaidi ya Magufuli!.

Hivyo kwa vile Watanzania huwa hawachagui sera wala hawachagui vyama bali huchagua watu, kama, Magufuli ameweza kuchaguliwa kihalali na kumshinda Edward Lowassa, kwenye uchaguzi Mkuu huru na wa haki, then you cannot tell about Watanzania huwa wanachagua nini, hivyo Tundu Lissu ambaye ni zaidi ya Magufuli, akisimama na Magufuli, you can never tell what will happen!, Magufuli naweza akaachwa mbali sana! , ila litabaki swali moja tu dogo, with reference ya kilichotokea Zanzibar, hata huku bara, je ikitokea kweli Chadema ikamsimamisha Tundu Lissu na ikatokea Tundu Lissu akishinda, jee atapewa?.

NB. Sijasema Lissu ni zaidi ya Magufuli kwenye nini, na nawaomba sana msiniulize!.

Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali

=======
Hoja za wadau
Duh kweli....
 
Pascal Mayalla,

Tundu LISU kumpima uwezo wake mpime kwanza kama mbunge. Je jimboni kwake kafanya nini la maana Tangible linaloonekana? NawMkasifu wachaga wana msemo kuwa mtu akikuambia ana akili akuonyeshe vitu vinavyoonekana kama vile biashara aliyonayo, nyumba ya kuishi aliyonayo na pesa alizonazo na mali mbali mbali vinginevyo ni mjinga tu sababu akili kwa mchaga haipimwi kwa uwezo wa kubwabwaja maneno kama Lisu afanyavyo.

Ni baadhi tu ya makabila mengine yanayoamini kuwa mtu kuwa na akili ni uwezo wa kubwabwaja maneno ndio waunga mkono Lisu.
Mkuu YEHODAYA , duh...yaani una maanisha Tundu Lissu hajafanya lolote na chochote cha maana kule kwenye jimbo lake?. Kwani wewe ni mtu wa kule?.

Wanabodi, kama kuna mtu yoyote wa kule jimboni kwa Tundu Lissu, naombeni ajitokeze na kutueleza Tundu Lissu amefanya nini kule jimboni kwake, hata jambo moja tuu kabla hajashambuliwa, ili tulitumie kama a yard stick ya kumpa madaraka makubwa zaidi.
Nani anaweza kututajia?.
P
 
"Kwa jinsi nilivyomsikia Tundu Lissu na namna anavyoongea, then huyu Tundu Lissu ni typical yuko kama Magufuli type tena yeye ni zaidi ya Magufuli!.

Hivyo kwa vile Watanzania huwa hawachagui sera wala hawachagui vyama bali huchagua watu, kama, Magufuli ameweza kuchaguliwa kihalali na kumshinda Edward Lowassa, kwenye uchaguzi Mkuu huru na wa haki, then you cannot tell about Watanzania huwa wanachagua nini, hivyo Tundu Lissu ambaye ni zaidi ya Magufuli, akisimama na Magufuli, you can never tell what will happen!, Magufuli naweza akaachwa mbali sana! , ila litabaki swali moja tu dogo, with reference ya kilichotokea Zanzibar, hata huku bara, je ikitokea kweli Chadema ikamsimamisha Tundu Lissu na ikatokea Tundu Lissu akishinda, jee atapewa?." - Pascal Mayalla, July 24 2017

Mkuu YEHODAYA , duh...yaani una maanisha Tundu Lissu hajafanya lolote na chochote cha maana kule kwenye jimbo lake?. Kwani wewe ni mtu wa kule?.

Wanabodi, kama kuna mtu yoyote wa kule jimboni kwa Tundu Lissu, naombeni ajitokeze na kutueleza Tundu Lissu amefanya nini kule jimboni kwake, hata jambo moja tuu kabla hajashambuliwa, ili tulitumie kama a yard stick ya kumpa madaraka makubwa zaidi.
Nani anaweza kututajia?.
P
 
Back
Top Bottom