Tundu Lissu ndiye mtu Jasiri zaidi Tanzania tangu tupate Uhuru

Tundu Lissu ndiye mtu Jasiri zaidi Tanzania tangu tupate Uhuru

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Nchi yetu pendwa, kipenzi cha nchi nyingi duniani, kilimbilio la watu wote waliokua wakikandamizwa kwenye nchi zao hakuwahi kutawaliwa na Rais wa ajabu kama Magufuli.

Rais ambaye hakuwapenda raia wake, hakusikiliza tulio hai, akitoa matamko ya kudhalilisha na kukejeli.

Rais ambae hakuheshimu wazee, wala maraisi waliomtangulia. Hakusikiliza ushauri wa mtu yeyote.

Wazee watatu, Mwinyi, Mkapa na Kikwete walipojaribu kushauri waliambiawa waache"kuwashwawashwa".

Wakuu wa vyombo vya kutoa haki walimwogopa, Mahakama na Bunge.

Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama walimwogopa.

Washauri wake kitaaluma walimwogopa.

Viongozi wa Kiroho walimwogopa.

Bora angekua Ana fanya ama kutoa maamuzi sahihi,lakini sehemu kubwa ya maamuzi yake yalikua ya HOVYO.

Lakini pamoja na kuogopwa kote huko, kijana Mtanzania Tundu Antipas Mugwai Lissu hakumuogopa asilani.
Tundu alikosoa, alitetea na alisema kile alichostahili kusema.

Tundu alianza kumsumbua Mkapa kutokana na baadhi ya Watanzania wenzetu wachimbaji wa madini kufukiwa,kuzikwa wakubwa hai, yaani wakubwa wazima wa afya.

Tundu aliendelea kutetea watu hao hata kipindi Cha Kikwete,na wakati Fulani wa uchaguzi Kikwete akiwa angombea Urais aliwahi Kumpigia Kampeni DK Wilbroad Slaa wa Chadema ambae nae alikua angombea Urais akichuana na Kikwete.Kikwete aliamua kusema kwenye Kampeni huko Singida.

"Msimchague Tundu Lissu, ni afadhali Dkt. Slaa awe Rais kuliko Tundu Lissu kuwa Mbunge.

Tundu Lissu aliendelea kuitesa serikali ya CCM kwa hoja zake.

Tundu Lisu hakumuacha Magufuli salama.

Kwa sababu ya Magufuli kutokuheshimu katiba aliupata wakati ngumu zaidi kwa Lissu bigwa wa sheria.

Katika maraisi hawa watatu Magufuli ndio amekufa sio mvumulivu kabisa kwa hoja za Lissu.

Lisu aliamka siku Moja na akaponea Tundu la sindano kwa kumiminiwa risasa 38 na zilizoingia mwilini Ni 16.

Lisu alitibiwa Dodoma, Nairobi na Belgium.

Uchaguzi Mkuu wa pili kwa Magufuli Lisu alirudu kibabe na kugombea Urais akipambana vikali na Magufuli.

Katika Kampeni hizo Lissu alionesha uwezo wa hali ya juu Sana kujenga hoja na ushawishi.

Kitu cha ajabu na cha kushangaza Lissu alikua pamoja na hoja za kiuchaguzi lakini alieleza mabaya na mapungufu yote ya rais aliekua anaogopwa kuliko Raisi yoyote Tanzania, Magufuli, Lissu alipenda kumwita Magufuli "mwovu"

Lisu haogopi bwana alikua anamchana Live dikteta uchwara yule, kamchana kwelikweli na dikteta akawa mpole tu.

Tanzania hii hakuan mtu aliweza jumps makavu Live dikteta yule zaidi ya Lissu.

Lisu kwanza kumchana dikteta yule akiwa hajapigwa risasi, akamchana alipopigwa risasi na akaendelea kumchana baada ya kupigwa risasi.

Lisu kamchana dikteta yule kwa hoja na hoja zake wakashindwa kuzijibu kwa hoja, badala yake kifo ndio ikawa majibu ya hoja za Lissu.

Baada ya Kampeni Lissu akaondoka kibabe.

Tanzania hii nasema hakuna aliyeweza kumkosoa Mchato yule. Si wazee, si mauaji, si wabunge, si viongozi wa Kiroho, sio Makamanda, sio wanazuoni, sio mabalozi. Tundu Lissu aliweza kumjibu Lissu kwa hoja walishindwa.

Kwa binadamu Lissu kaweza
Lakini Mungu Ni Fundi.
 
Absolutely, big YES...

Huyu jamaa katufungua ufahamu wengi sana juu ya siasa na utawala mwovu wa nchi hii chini ya CCM hususani nyakati za Mwendazake.

Tundu Lissu ni kiongozi anayefundisha somo la UJASIRI Wa KWELI na wa HAKI kwa vitendo.

Tundu Lissu hana makando kando kama vile ufisadi, wizi, kuonea mtu nk.

Ni mtu wa HAKI huyu. Na HAKI hushinda DHULUMA siku zote. Mungu muumba huwalinda wenye HAKI wake.

Ushahidi ni risasi 16 kuingia ndani ya mwili wa mtu huyu wa HAKI aliyebeba KUSUDI la Mungu kwa nchi hii lakini bila kuondoa UHAI wake!

Lakini mtesi wake mkuu Mwendazake John Pombe Magufuli, yaani akafa kwa kushindwa kupumua, kwa moyo wake ku - feli kufanya kazi, just like that!
 
Kama nijasiri akafungue au akafuatilie kesi yake ya kushambuliwa mahakamani. Ilitujue mbivu na mbichi.
 
Tundu Lissu mbabe wake ni Lowassa, maana pamoja na Lissu kujua hivyo na mwenyewe alishawahi kusema kwamba Lowassa ni fisadi na kuwashangaa ccm kumpa fomu ya kugombea urais fisadi, ila Lowassa alipokuja Chadema kutaka kugombea urais Lissu aliufyata hakuzungumza tena ufisadi wa Lowassa.
 
Mafanikio ya Samia ni habari mbaya sana kwa Lisu maana 2025 hana chake tena.

Ccm itaendelea kupeta
Mafanikio gani zaidi ya ngonjera za kila siku? Kitu cha maana mpaka sasa ni kuwaachia mashehe na kuwarudishia kina Mbowe pesa za faini; lakini nacho ni dosari kwani nchi inaongozwa kwa utashi wa rais au taasisi thabiti?
 
Lissu huyu aliekimbilia ubalozini baada ya kuisha kwa uchaguzi???

Lissu huyu aliejificha kwa mabeberu ubeligiji ?

Bhasi kwa muktadha huu naweza sema Jasiri ni Mange Kimambi kama ujasiri ni kutukana matusi na kuisema Serikali ukiwa umejificha kwa mabeberu
 
Mafanikio ya Samia ni habari mbaya sana kwa Lisu maana 2025 hana chake tena.

Ccm itaendelea kupeta
CCM na mama Ni vitu viwili tofauti.
Mama atataka haki itendeke,CCM watakataa,
Mama atataka katiba mpya,CCM watakataa,
Mama atataka time huru,CCM watakataa
Mama atataka uchaguzi huru kwa Rais wabunge,madiwani na serikali za Mitaa,CCM watakataa.
Mama atataka uhuru wa habari,CCM watakataa

Mwisho wa siku ataamua awe na tabia za ki CCM au abaki na ustaarabu wake.

Mwisho wa siku CCM Ni Ile Ile,ambayo itaichafua Tanzania
 
Lissu huyu aliekimbilia ubalozini baada ya kuisha kwa uchaguzi???

Lissu huyu aliejificha kwa mabeberu ubeligiji ?

Bhasi kwa muktadha huu naweza sema Jasiri ni Mange Kimambi kama ujasiri ni kutukana matusi na kuisema Serikali ukiwa umejificha kwa mabeberu
Hoja zenu mkaamua kumpiga risasi lakni kwenye kinywa mlishindwa.
 
Back
Top Bottom