Tundu Lissu ndiye mtu Jasiri zaidi Tanzania tangu tupate Uhuru

Tundu Lissu ndiye mtu Jasiri zaidi Tanzania tangu tupate Uhuru

Acha tufanye utani kwa sababu ya ujinga wetu, lakini Tundu Lisu ni kiumbe kingine hata hapo CHADEMA sio mahàli pake. Mpaka kesho sidhani kama CHADEMA wanajue wanaishi na kiumbe cha amina gani. Walioamuru apigwe risasi wanamjua vizuri.
Hao waliotaka kumuua Mungu anawapa semina kidokidogo. Wengine wote waliufyata baada ya vitisho lakini Lissu yupo!
 
Jasiri anayeufyata na kukimbia kulelewa na wazungu
Ujasiri hautafsiriwi kwa kujipeleka mwenyewe kwenye kinywa cha simba...

Maana ukiliwa na simba huyo, hao hao waliosema "wewe siyo jasiri" mwishoni watasema;

"....aah, kumbe yule hana akili vile...."

au

"....aaah yule akiwa Rais wa Tanzania atatusukumiza watanzania wote kwenye tundu la simba ili waliwe, aaah hafai yule...!!"

Ujasiri na mkombozi wa kweli wa watu, siku zote silaha yake kubwa ni AKILI au MAARIFA na BUSARA. Sio bunduki na mabomu au jeshi kubwa au mahakama au magereza ...

Ukiona adui yako kajipanga kuua sisimizi kwa AK47 kijinga, una - retreat na kujipanga upya unamwacha na ujinga wake...

Ku - retreat katika vita/mapambano si WOGA bali it is always ni calculation ya AKILI KUBWA in order to win the war dhidi ya adui mjinga na mpumbavu...

MUSA aliyewakomboa wana wa Israel toka utumwani Misri, alifanya vile...

Alipoona Farao anamtafuta amuue, alikimbilia nchi ya Midiani na kujificha huko [Soma: KUTOKA 2: 15]

Farao alipokufa, Musa aliamriwa na Bwana Mungu kurudi Misri awakomboe ndugu zake Waebrania (Waisraeli) kwa maelekezo ya Mungu Yehova...

Yehova, alimwambia; "....mtesi wako Farao aliyekuwa anaitafuta roho yako ameshakufa[Soma: KUTOKA 2:20]. Sasa nenda kawakomboe ndugu zako..."

Soma hata historia na harakati za YESU KRISTO za kuukomboa ulimwengu huu na wanadamu wote toka mikononi mwa shetani...

Zilikuwa na ups & downs kibao. Mara nyingi alijificha na kuwakimbia watesi wake waliotaka kumuua au kumfunga gerezani kwa makosa ya kubumba kabla ya wakati wake...

Lakini hawa wote, mwisho wa siku ulikuwaje?

Walikuwa MASHUJAA walioandika historia isiyofutika vizazi vyote. Walishinda zaidi ya kushinda dhidi ya utawala dhalimu na wa kiovu wa watawala wa dunia hii wajifanyao miungu watu...

RETREATING IS NOT A COWARDNESS

Tundu Lissu ana akili na mwerevu kuliko ninyi nyote huko mnaotafuta roho yake. Roho wa Bwana yu juu yake. Amebeba kusudi la Bwana ktk nchi hii. Wewe ukikubali au ukatae, ukitaka au usitake, uamini au usiamini, it doesn't matter at all. Mission must be accomplished....

Sasa unaelewa nini?

Mtesi wa Tundu Lissu Mwendazake, (Farao) John Pombe Magufuli ameshakufa....

Na wengine waliosalia (labda ukiwemo wewe) watakufa mmoja baada ya mwingine kama akili zao hazitafunguka na kutubu makosa yao...

So, it's just a matter of time atarudi ktk nchi yake na kuwakomboa watu wake...!!
 
Baada ya Nyerere lissu ndiye anafuata kwa uzalendo na ujasiri
Huwezi kumlinganisha Nyerere na Lissu kwa ujasiri, Lissu anamzidi Nyerere mbali sana.
Nyerere alikuwa na sapoti kubwa almsost watanganyika wote wa wakati huo, na adui (mkoloni) alikuwa anajulikana kwa rangi yake.
Lissu anapambana katikati ya wakoloni weusi ambapo ni kazi sana kuwatambua na pia level ya ujinga na woga ipo juu sana.
HITIMISHO: Lissu ni jasiri kuliko nyerere.
 
Tundu Lissu mbabe wake ni Lowassa, maana pamoja na Lissu kujua hivyo na mwenyewe alishawahi kusema kwamba Lowassa ni fisadi na kuwashangaa ccm kumpa fomu ya kugombea urais fisadi, ila Lowassa alipokuja Chadema kutaka kugombea urais Lissu aliufyata hakuzungumza tena ufisadi wa Lowassa.
Na aliporudi CCM mkaufyata tena
 
Mtikila kiboko yake alikua fisadi Rostam Aziz.
Alienda kukopa kwa Rostam sh milioni tatu.
Rostam akamwandikisha maelezo.
Mtikila akasahau akaanza kuwaponda mafisadi pamoja na Rostam.
Rostam akatoa barua ya mkopo ya Mtikila.
Pamoja na Ombi la msaada ya fedha za kwaya ya kanisa la Mtikila.
Mtikila akaona aibu.
Rostam mafia
Naijua hiyo stori lakini alikuwa ni mpambanaji na aliwasha moto mzito kwenye issue ya mgombea binafsi wa Urais. Yule alikuwa ni jeshi la mtu mmoja. Issue ya Rostam ilimtia doa. Hawa wengine wa sasa madoa yao wamefanikiwa kuyaficha vizuri.
 
Nchi hii haikuwahi kupata mtu mpenda sifa na MUONGO kama Marehemu wa legacy.aka Jiwe,aka Mwendazake,aka Rais wa Malaika
Rais mchapakazi haijawahi kutokea tangu ziumbwe mbingu na ardhi .R.I.P jemedari ,mtu kama wewe lazima ulete izo fitna na huwezi ona mchango wke kwasababu wewe ni Mganda.
 
Makamu mwenyekiti wa Chadema Tundu Lisu ameshauriwa kama mtu mzima aombe msamaha kwa watanzania kwani mtu mzima akivuliwa nguo huchutama na siyo kukimbia uchi.

Ni miaka sita sasa tangu Tundu Lisu aitabirie Tanzania mabaya ikiwemo kushitakiwa MIGA , ndege kukamatwa, uchumi kufilisika, kunyimwa misaada mbalimbali. Mpaka sasa hakuna hata kitu kimoja kilichotabiriwa na Lisu kilichotimia maaana yake aliwadanaganya watanzania, yani licha ya kusoma kwa kodi za watanzania yeye anakuja kufanya kazi ya kuwadanganya watanzania!!!
Kinyume na utabiri wa Lisu ,Tanzania ya sasa imeingia uchumi wa kati, hatujashitakiwa MIGA na viwanda vya kuchenjua dhahabu vimejengwa Mwanza. Mapato ya madini yamepanda kutoka billioni 100 hadi billion 500, ndege hazikamatwi na watanzania ni wamoja zaidi kinyume na utabiri wake.
Baada ya kuona aibu Tundu Lisu na Lema badala ya kuwaomba msamaha watanzania wao wamekimbilia Ulaya kwenda kulishwa bure na wazungu!!

Lema na Lisu rudini nyumbani muwaombe msamaha watanzania muanze kuishi kwa jasho lenu kwa kufanya kazi na siyo kulelewa.
 
Nimefuatilia nyuzi zote! zile zinalitaja JINI lililokosea likaangukia duniani kupitia chattle ni nyingi ajabu. Sishangai kwa sababu binadamu hakuwahi kuona wala kupata uzoefu wa shetani. Bahati nzuri mashetani wote huja na kuua kwa kipindi kifupi kabla ya kurudi nyumbani kwao kuzimu. Ahsante Mungu kwa kutuondole lile JINI magu
 
Lisu Hana ujasiri wowote ,mbona hakumkosoa mbowe alipouza chama Kwa lowasa ,aliufyata
 
Tanzania hii hakuan mtu aliweza jumps makavu zaidi ya Lissu.

Tanzania hii nasema hakuna aliyeweza kumkosoa Mchato yule. Si wazee, si wabunge, si viongozi wa Kiroho, sio Makamanda, sio wanazuoni, sio mabalozi. Tundu Lissu aliweza kumjibu Lissu kwa hoja walishindwa.
Naona kama hili ni bandiko la kuabudu na kutweza, kama ni kumkosoa, JPM amekosolewa sana, na wengi, ila hili la ujasiri, ni kweli Lissu jasiri.
Ni kufuatia ujasiri huu ndio maana ni akina sisi tuliomchagiza agombee na JPM, hata kabla ya zile pyu pyu.

Alipotaka kurudi, aliandika barua kuomba kuhakikishiwa ulinzi, hakujibiwa, ni akina sisi tena ndio tulijitolea kumshawishi kurejea hivyo hivyo, Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!
P
 
Jemadari Tundu Lisu anastahili kutunukiwa cheo cha heshima cha “ SIR” kwa ujasiri aloonesha kipindi cha kabla na wakati wa Mwendazake lakini hususa kipindi cha Mwendazake.

Pamoja na kunusurika kuuawa ktk mazingira tatanishi eneo la bunge ,

Baada ya nafuu ya matibabu alirejea nchini kuja kugombea uongozi wa cheo cha juu kabisa nchini cha uraisi,


He is great [emoji106]

Campaigns zake zilikuwa za kuvutia kumsikiliza ,

Napendekeza aitwe SIR Tundu Lisu
 
Hakika huyo ni Jemadari wa wetu [emoji1944]

Ikumbukwe kuwa Jemadari hupatikana vitani.
 
Wanaume karibia wote waliufyata enzi za Kayafa lakini Jemadari huyu alijua kumkabili Goliath [emoji123]

Ni Mfalme Daudi wetu.

Mwenyezi azidi kujalia kuishi kwingi akiwa na amani na afya njema aone na vilembwe na vilembwekuzi.
 
Back
Top Bottom