Jasiri anayeufyata na kukimbia kulelewa na wazungu
Ujasiri hautafsiriwi kwa kujipeleka mwenyewe kwenye kinywa cha simba...
Maana ukiliwa na simba huyo, hao hao waliosema "wewe siyo jasiri" mwishoni watasema;
"....aah, kumbe yule hana akili vile...."
au
"....aaah yule akiwa Rais wa Tanzania atatusukumiza watanzania wote kwenye tundu la simba ili waliwe, aaah hafai yule...!!"
Ujasiri na mkombozi wa kweli wa watu, siku zote silaha yake kubwa ni AKILI au MAARIFA na BUSARA. Sio bunduki na mabomu au jeshi kubwa au mahakama au magereza ...
Ukiona adui yako kajipanga kuua sisimizi kwa AK47 kijinga, una - retreat na kujipanga upya unamwacha na ujinga wake...
Ku - retreat katika vita/mapambano si WOGA bali it is always ni calculation ya AKILI KUBWA in order to win the war dhidi ya adui mjinga na mpumbavu...
MUSA aliyewakomboa wana wa Israel toka utumwani Misri, alifanya vile...
Alipoona Farao anamtafuta amuue, alikimbilia nchi ya Midiani na kujificha huko [
Soma: KUTOKA 2: 15]
Farao alipokufa, Musa aliamriwa na Bwana Mungu kurudi Misri awakomboe ndugu zake Waebrania (Waisraeli) kwa maelekezo ya Mungu Yehova...
Yehova, alimwambia; "....mtesi wako Farao aliyekuwa anaitafuta roho yako ameshakufa
[Soma: KUTOKA 2:20]. Sasa nenda kawakomboe ndugu zako..."
Soma hata historia na harakati za
YESU KRISTO za kuukomboa ulimwengu huu na wanadamu wote toka mikononi mwa shetani...
Zilikuwa na ups & downs kibao. Mara nyingi alijificha na kuwakimbia watesi wake waliotaka kumuua au kumfunga gerezani kwa makosa ya kubumba kabla ya wakati wake...
Lakini hawa wote, mwisho wa siku ulikuwaje?
Walikuwa MASHUJAA walioandika historia isiyofutika vizazi vyote. Walishinda zaidi ya kushinda dhidi ya utawala dhalimu na wa kiovu wa watawala wa dunia hii wajifanyao miungu watu...
RETREATING IS NOT A COWARDNESS
Tundu Lissu ana akili na mwerevu kuliko ninyi nyote huko mnaotafuta roho yake. Roho wa Bwana yu juu yake. Amebeba kusudi la Bwana ktk nchi hii. Wewe ukikubali au ukatae, ukitaka au usitake, uamini au usiamini, it doesn't matter at all. Mission must be accomplished....
Sasa unaelewa nini?
Mtesi wa Tundu Lissu Mwendazake, (Farao) John Pombe Magufuli ameshakufa....
Na wengine waliosalia (labda ukiwemo wewe) watakufa mmoja baada ya mwingine kama akili zao hazitafunguka na kutubu makosa yao...
So, it's just a matter of time atarudi ktk nchi yake na kuwakomboa watu wake...!!