Tundu Lissu ndiye mwanasiasa anayeongoza kwa wafuasi Tanzania kwa sasa; ni msema kweli na anafanya mindset reform ya wananchi

Upo sahihi sn mkuu
 
Huyu ndo Nyerere Halisi

The man standing with TRUTH!!!
 
Wenye akili tunamwelewa lisu
Yule dada muhuni na wenzie 18 hatuna muda wa kuwafuatilia
 
Jidanganyeni .

Mwenzenu si raia wa Tz na hata familia yake haipo Tanzania.

Lissu NI kibaraka wa mabeberu.
Mabeberu wanamtegemea Lisu, kwani ni kipi wanakikosa hadi sasa hapa nchini hadi wamtumie Lisu?

Hata Mimi ningepata nafasi ya kupeleka watoto wangu ulaya ningewapeleka hata Leo, mtabaki nyie mnaaona sifa kuitwa wanyonge huku viongozi wakisomesha watoto wao shule Bora.
 
Hatutaki mwanasiasa mwenye mvuto.
Tunataka mwanasiasa atakaeweza kuisukuma TANZANIA kimaendeleo.
Maendeleo yanaletwa na wananchi kwa kufanya Kazi, huku wakilipa kodi.
 
Lisu ni mharakati aliyobobea. Hilo apewe maua yake.

Walakin

Na kwa maoni yangu-Haitatokea hata siku moja, akawa Raisi wa Tanzania.

Itakuwa ni hatari kwa Usalama wa Muungano na Taifa letu.
Muungano wa matambiko ni WA kupigwa chini na watu wasioamini ushirikina.
 
nashkuru kwa kuelewa hilo kwamba maendeleo hayataletwa na lisu
Ni kweli,.ndio maana tunataka kiongozi mwenye mvuto kwa ajili ya hamasa kwa wananchi kuchapa kazi.
 
Ni kweli,.ndio maana tunataka kiongozi mwenye mvuto kwa ajili ya hamasa kwa wananchi kuchapa kazi.
Hatutaki kiongozi mwenye mvuto
mvuto peleka kwenye biashara
 
Wafuasi wake wengi ukiwapima afya ya akili zao zina mushkeli!
Nyani haoni kundule! Wenye afya ya akili mdororo ni ccm wanaogawa kanga na kofia kwa wapigakura maskini ambao nao akili zao zimeozeshwa na umaskini usiomithilika uliosababishwa na sera mbovu za ccm!
 
Huyu TUNDU LISU mnayepigia debe na kumpamba sana humu,kiuhalisia alishapoteza sifa ya kuaminika muda mrefu sana.Ni kweli Lisu na washirika wake wamekuwa waibuaji wa madudu na maovu mengi ya utawala huu wa CCM, lakini alitushangaza na kutukatisha tamaa wengi wetu pale alipokinzana waziwazi na JPM alipoamua kuivunja mikataba iliyokuwa kero ya miaka mingi, matokeo yake Lisu aligeuka kuwa mtetezi wa hayo makampuni, kesi zilifunguliwa dhidi ya serikali na tulishuhudia ndege zetu zikishikiliwa huko nje ,hivyo alitufundisha wengi kuwa hatupaswi kumwamini mwanasiasa yeyote naye akiwemo.
 
Muungano wa matambiko ni WA
kupigwa chini na watu wasioamini ushirikina.
Kwa mtaji huo unadai yanayonekana kwenye picha👇🏿 ni matambiko ya ushirikina?

🤔 hatari aisee🤦🏾‍♂️
 
Kwa mtaji huo unadai yanayonekana kwenye picha👇🏿 ni matambiko ya ushirikina?

🤔 hatari aisee🤦🏾‍♂️
Haya ndio yalifanywa hadharani, nyuma ya pazia ulikuwa uchafu mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…