Tatizo lako na Tundu Lissu ni moja!
Ukurupukaji! Hujasoma hata hoja yangu umeshakurupuka!
Mimi nimembeza Tundu Lissu anavyo approach mambo na hasa jambo kubwa kama hili!
Hapo juu nimesema Nina sympathize naye ktk masaibu yake lakini unanilaumu!
Najua hujui maana ya Sympathize na masaibu na kwa kifupi wewe ni mediocre au kilaza tu!
Wewe pia umekurupuka.
Na kwa kuwa umekurupuka, umeshindwa ku-'capture' hoja yenyewe.
Kesi iliyopo Uingereza siyo Kesi ya JINAI, ambayo yaliyomo yanasubiri Uamuzi wa mwisho.
Hii ni Kesi ya Madai, ambayo yaliyomo ni 'disclosures' ambazo zilikuwa zimefichwa Kabatini.
Swali hapa ni kwamba, hayo yaliyo wasilishwa Mahakamani na Bw. Michael Clifford yanatosha?
Katika kulijibu hili, Bw. Tundu Lissu amesema wataomba Bw. Clifford atoe taarifa za ziada kwa kuwa amesema Kampuni ya Tigo Tanzania iliwasiliana kwa WhatsApp na Watumishi wa Serikali walio iagiza (Tigo) kutoa taarifa za 'surveillance' za Simu za Lissu.
Kwa mara ya kwanza, taarifa sasa zipo hadharani kuhusu waliokuwa wanataka kujua mwenendo wa Bw. Tundu Lissu.
Watu wa Serikali.
Kwa miaka Saba, tulikuwa na hisia tu.
Sasa ushahidi uko hadharani.
Kumbuka, Mwanasheria wa Bw. Tundu Lissu, aitwae Bw. Bob Amsterdam, ametuma Wanasheria Mahakamani London kufuatilia Kesi hii ya Bw. Clifford.
Wamekwenda kuona na kusoma Nyaraka zilizowasilishwa.
Kampuni mama ya Tigo [Millicom] ilikwenda hadi "Court of Appeal of UK" ili Kesi isikilizwe "Faraghani" [Chambers], lakini Mahakama hiyo ya Rufaa ya Uingereza ikaamua kuwa hii Kesi ina Maslahi ya Umma, kwa hiyo isikilizwe katika Mahakama ya Wazi, "Open Court", lengo likiwa hata akina 'Kalimanzila' wajue kinachoendelea.
Kuna Kabila Nchini Tanzania wanao msemo usemao, "Umufa w'iMbwebwe wunyobwa wugishushe" yaani, 'Mchuzi wa Mbweha hunywewa ukingali wa moto.'
Nimeamini kwamba Damu ya Binadamu haimwagiki bure.
Hata kama ilimwagika Miaka Saba iliyopita.
Yajayo yanafurahisha.