Tundu Lissu ni clever but not Intelligent person. Ni Kiongozi mwenye papara sana na hana utulivu kabisa

Umesema neno!
 
Wewe pia umekurupuka.
Na kwa kuwa umekurupuka, umeshindwa ku-'capture' hoja yenyewe.
Kesi iliyopo Uingereza siyo Kesi ya JINAI, ambayo yaliyomo yanasubiri Uamuzi wa mwisho.
Hii ni Kesi ya Madai, ambayo yaliyomo ni 'disclosures' ambazo zilikuwa zimefichwa Kabatini.
Swali hapa ni kwamba, hayo yaliyo wasilishwa Mahakamani na Bw. Michael Clifford yanatosha?
Katika kulijibu hili, Bw. Tundu Lissu amesema wataomba Bw. Clifford atoe taarifa za ziada kwa kuwa amesema Kampuni ya Tigo Tanzania iliwasiliana kwa WhatsApp na Watumishi wa Serikali walio iagiza (Tigo) kutoa taarifa za 'surveillance' za Simu za Lissu.
Kwa mara ya kwanza, taarifa sasa zipo hadharani kuhusu waliokuwa wanataka kujua mwenendo wa Bw. Tundu Lissu.
Watu wa Serikali.
Kwa miaka Saba, tulikuwa na hisia tu.
Sasa ushahidi uko hadharani.
Kumbuka, Mwanasheria wa Bw. Tundu Lissu, aitwae Bw. Bob Amsterdam, ametuma Wanasheria Mahakamani London kufuatilia Kesi hii ya Bw. Clifford.
Wamekwenda kuona na kusoma Nyaraka zilizowasilishwa.
Kampuni mama ya Tigo [Millicom] ilikwenda hadi "Court of Appeal of UK" ili Kesi isikilizwe "Faraghani" [Chambers], lakini Mahakama hiyo ya Rufaa ya Uingereza ikaamua kuwa hii Kesi ina Maslahi ya Umma, kwa hiyo isikilizwe katika Mahakama ya Wazi, "Open Court", lengo likiwa hata akina 'Kalimanzila' wajue kinachoendelea.
Kuna Kabila Nchini Tanzania wanao msemo usemao, "Umufa w'iMbwebwe wunyobwa wugishushe" yaani, 'Mchuzi wa Mbweha hunywewa ukingali wa moto.'
Nimeamini kwamba Damu ya Binadamu haimwagiki bure.
Hata kama ilimwagika Miaka Saba iliyopita.
Yajayo yanafurahisha.
 
Nimekuelewa ndugu, niishie hapo Kwa sasa…
 
Well said mkuu…bandiko kuntu
 
Pamoja na ukurupukaji wake... Sidhani kama wewe hapo ungevumilia.
Make inavoonekana umeleta post yako chap sana bila kujiuliza maswali mengi kuhusu details alizonazo Tundu Lisu na pengine amaekuwa nazo kwa muda mrefu!
This is between his life and death. Sidhani kama hajafanya yampasayo kufanya!
 
💯👊Watu wanajitoa sana ufahamu hapa!
 
Kwa ushahidi huu tundu lisu ataishitaki serekali yenu chovu na itamlipa hela nyingi kwa lazima nasema kwa lazima,


na ikibainika kwenye mahakama za kimataifa kwamba serekali ili m terrorise lisu mtawekwa kwenye black list

Kwa hiyo usilete mbwembwe za za ki uvccm tuendako siyo kuzuri
 
Unaongea hivi ukute huna jeraha hata la wembe mwilini mwako tulia mtoto mlaini wewe acha wanaume wajipambambanie.
 
Kesi bado inaendelea, hakuna judgement imetoka! Mimi ni Legal Brain najua ninachoongea!
Umechanganya Kesi za Madai na Kesi za JINAI.
Judgement itakayotoka itasema moja ya mawili;
Akishindwa, itasema Bw. Clifford alifukuzwa kwa haki kwa kosa la kuuliza kwa nini Tigo iliipa Serikali ya Tanzania taarifa za mwenendo wa Bw. Tundu Lissu.
Akishindwa, hukumu itasema Bw. Clifford hakutendewa haki kwa kufukuzwa kazi baada ya kuuliza kwa nini Tigo iliipa Serikali ya Tanzania taarifa za mwenendo wa Bw. Tundu Lissu.
Katika hali hii, kwa nini isubiriwe 'Judgement'?
Vyovyote itakavyotoka Hukumu, utambulisho wa waliotaka kufanya "Political Assassination" ya Bw. Tundu Lissu umeanza kuwa wazi.
 
Nomefurahia kauli yako ya kujinasibu kwamba wewe ni Legal Brain.
Shirika la Habari, Reuters, jana muda wa 16:20GMT, iliandika ifuatavyo;
"In its own Court Filings this month, Millicom said it had learned in late August or early September 2017 of concerns 'about a local politician's mobile phone data being passed to a government agency.'
It said the individuals involved were disciplined and additional training was provided to Millicom subsidiaries about how to respond to requests for Company data.
The Company denied allegations in a Lawsuit filed by former employee, Michael Clifford, that Clifford had been dismissed for raising concerns about the tracking of Lissu's location data".
Hayo ni maelezo ya Millicom, ambayo ni Kampuni mama ya Tigo Tanzania, KWA MAANDISHI, katika Mahakama Nchini Uingereza.
Mimi ni Fundi Mchundo, na wala siyo Legal Brain, lakini najua kusoma, na kusikiliza kwa utulivu, bila kukurupuka.
Sasa jiulize; "NANI KATI YA WEWE NA Bw. TUNDU LISSU AMEKURUPUKA"?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…