Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ni mwarobaini wa Upinzani kumng'oa Magufuli

Nani aliekudanganya kuwa mwanachama wa chama cha siasa ni sawa na kuhukumiwa kifungo gerezani, kwamba hakuna kutoka mpaka utakapomaliza hukumu yako?

Anyway, sijui kama utakuwa umeelewa mantiki ya swali langu.
Naam!

Najua mfungwa anaweza kutoka gerezani ama kwa msamaha ama kwa kutoroka ama kwa kupoteza uhai. Lakini, inapotokea mfungwa huyo akashupalia nia ya kutoka gerezani kwa njia ya kutoroka, unashindwaje kujiuliza kuwa gereza hilo lina matatizo na ama mfungwa huyo aliwekwa gerezani kimakosa hivyo anaona bora toroke kuliko kutumikia adhabu ambayo si sahihi kwake. Waweza usinielewe, Mkuu.
 
Ndio maana nikakwambia sijui kama umeelewa mantiki ya swali langu.

Hakuna popote panapomzuia mwanachama yeyote wa chama chochote cha siasa kujiondoa kwenye chama chake na kujiunga na chama kingine, siku na wakati wowote atakaohitaji, sasa wewe unavyowalaumu Chadema eti ni uzembe wao kwasababu wanakimbiwa na wanachama wao sijui kama kuna mwenye akili timamu humu atakuelewa!.
 
Ujinga mbaya kabisa kuliko wote, ni pale mtu anaposhindwa kutofautisha upepo wa Lori na bajaji

Huo ndio Ujinga ulioko Kwa machadema karibu wote,

Bajaji ndio iwe kigingi cha kulizuia Lori lisipite barabarani kweli?

Mnachekesha kweli nyie,
 
Fact uko vizuri
 
Wewe mwenyewe huamini ulichoandika. Bila tume huru na mwenzenu amepiga kampeni miaka 5- non stop mnategemea mtafanikiwa? Hata kupata wabunge uchaguzi huu itakuwa ngumu sana.
 

Hivi wewe ndiye au kuna mwingine? Uwezi kuwa serious ukaandika hivi. Kwa mambo aliyofanya JPM, na staili yake yake ya kupiga kampeni miaka 5 nchi nzima peke yake, hata asipofanya kampeni mwaka huu, atashinda asubuhi ya saa mbili. Pia kumbuka, kwa jinsi watu walivyokatishwa tamaa na siasa za uanaharakati za chadema, katiba mbovu, na issue ya EL na wote waliojisalimisha ccm, wengi wetu hatukujiandikisha japo sare za vyama tunazo na kampeni tutasaidia lkn hatutapiga kura. Kwa ufupi, ACHENI NDOTO ZA MCHANA NA KUHARIBU PESA, UCHAGUZI HUU UMEISHAISHA KABLA YA KUANZA. Tusubiri kuserebuka na nyimbo kibao za wasanii- nadhani staili ya kampeni za ccm za mwaka huu zitavunja rekodi.
 
kweli
kazi ipo jogoo kwa jogoo na unene uleule he makubwa haya
 
mkuu mbona jamaa kaandika vizuri na kwa uchambuzi kwa yote aliyoyandika anawambia ccm msirelax mkajiona mko salama so ukimuona yerco hajaandika vyema sawa but kaeleweka vizuri mkuu ametoa taa nyekundu kwamba uchaguzi huu sio wa kitoto kama mnavyofikilia hebu jitahidin kuwa mna mnatafuta codes za kila msg
 
Huyu magufuli anapaswa kuondoshwa hata kwa nguvu,anatuharibia nchi yetu.
 
Anaharibuje? Elelezea
Hivi kwa sasa uchumi wetu unakuwa kwa kasi ya asilimia ngapi? Je masoko ya mazao yetu Kama kahawa,korosho na mbaazi ipoje mwaka huu?Je mahusiano yetu kimataifa yakote,yaani tumepoteza ushawishi Sasa tunatumia mabavu kwa kila kitu
 
Wewe mwenyewe huamini ulichoandika. Bila tume huru na mwenzenu amepiga kampeni miaka 5- non stop mnategemea mtafanikiwa? Hata kupata wabunge uchaguzi huu itakuwa ngumu sana.
Ccm wanatakiwa kutolewa madarakani kwa nguvu,huu uchaguzi tufanye tu ili kutafuta kasababu ka kuwaondoa madarakani kwa nguvu Kama walivyofanya wamalawi
 
Safari ni mwendo wa kuandika lakini ukweli ni kwamba Magufuli atashinda kwa zaidi ya 80% .
Chama kuondolewa madarakani na upinzani tena upinzani wenyewe wa akina Lissu ni ndoto za alinacha na pia ni kosa ambalo halitakiwi kusameheka Duniani na Mbinguni.
 
Chadema wana kazi moja tu sasa nayo ni kupanga mikakati yao ya mambo ya kuyafanya baada ya kuchukua nchi hapo October 2020.
Njia ni nyeupe sana kwa Lissu. Amini nakwambia njia ni nyeupe sana kwa Lissu. Ajipange tu
Naomba tuombe uzima hiyo oktoba 28/10/2020 kwanza kushinda hamshindi hilo liko wazi, pili tunaenda kuhakikisha hampati hata kiti kimoja cha ubunge.

Kwa ufupi tarehe 28/10/2029 hatutaki kusikia habari za kuibiwa kura maana umesema akisimamishwa Lissu ni Ikulu tu.
 
Hawa jamaa wanajua kutengeneza propaganda na kulishana matango pori, mwaka jana walisema hakuna kura ya Lowassa itakayoibiwa mara Lowassa ana watu wengi kwenye mfumo wa nchi, tulivyomaliza kumfyatua wakaja na story ya the heague.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…